SABASABA ilikua ni sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwa TANU. Ambapo tanu ilizaliwa tarehe 7 Julai 1954. Na TANU ikaungana na ASP ikazaliwa CCM. Kwa mara ya kwanza sikukuu hii iliazimishwa mwaka 1963, Na mpaka leo hii bado sikukuu hiyo inaadhimishwa nchini, japokua ni kama imevalishwa koti la maonesho ya kimataifa ya biashara. Maswali ya kujiuliza.
- Sikukuu ilikua ya TANU katika mfumo wa chama kimoja. Kwann sikukuu iendelee kuazimishwa katika kipindi hiki cha vyama vingi na lengo lake ni nini.?
- Je, siku CCM ikitoka madarakani ndo itakua mwisho wa sikukuu hii au hao wengine watakaokuja nao wataendelea kuazimisha sikukuu hii ya TANU (CCM).?
- ASP iliungana kutengeneza CCM. Kwann kuzaliwa kwa ASP hakuazimishwi huku bara (sina uhakika kama znz nao wanaazimisha ASP yao) , kwa maana kule znz wanasherehekea kuanzishwa kwa TANU yetu.?
- Je, haya maswala ya mfumo wa vyama vingi sio geresha tu za kisiasa au koti la kuzugia hao wafadhili ilhali yanayotendeka ni yaleyale ya mfumo wa chama kimoja.?