Sababu za kupata uhamisho

FRUIT TREE

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2018
Posts
701
Reaction score
840
Habari za humu wanajukwaa?

Nina rafiki yangu ni mwajiriwa Halmashauri fulani hapa Tanzania. Ana mke wake ambaye pia na yeye ni mwajiriwa Halmashauri hiyo hiyo ila hawajafunga ndoa (hawana cheti cha ndoa).

Huyu jamaa ana miaka 5 kazini na mke wake ana mwaka 1 na ameshathibitishwa kazini. Jamaa anataka kuhama Halmashauri kwenda Halmashauri ya mkoa mwingine kabisa (Geita) ambapo kimsingi uhamisho unatoka kwa Katibu Mkuu Tamisemi.

Pia anataka kuhamia huko (Geita) na huyu mke wake (shemeji) ambaye ana mwaka 1 kazini ila ameshathibitishwa kazini.

Jana aliniomba ushauri ni jinsi gani ataweza kufanikisha uhamisho kwa wote wawili kwenda Mkoa mwingine wa Geita? Nilipomuuliza sababu za kuhama akasema mambo yake hayaendi na miaka inazidi kusonga. Nilichomwambia ni kuwa hakuna kitu kitashindikana. Nilivyofuatilia kwa wengine waliopata uhamisho wakasema wanatakiwa waandike barua ya kuhama kwenda kwa mwajiri wake.

Changamoto iliyojitokeza ni sababu zipi zinaweza kukubaliwa ili kufanikisha uhamisha huo ikumbukwe kuwa huko Geita siyo kwa wazazi wao?

Wanajukwaa kwa heshima na taadhima naomba kupewa sababu nyingi zitakazomwezesha huyu jamaa na mke wake kuhamia mkoa mwingine wa Geita.

Natanguliza shukrani,
Asante.
 
Atafute mtu wa kubadilishana nae akipata atahamia Kwanza yeye then waende kwa msajili wafunge ndoa ya serikali mke atamfata mume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…