Sababu ya report ya Tegeta ESCROW kuwasilisha bila kipingamizi

Niambieni

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
625
170
Nadhani ni lazima iwasilishwe hili tupate misaada iliyofungwa. Na sio kumtafuta mchawi au kutatua tatizo, bali lengo nadhani ni kupata kitumbua kilicho sitishwa.

Ulaya watapata taarifa ya kinachojiri na watatoa kitumbua, ili tupate ngawira za madawa au afya, elimu, .....

Ebu fikiria, jana na leo Tanga hospital wanatumia plastics badala ya gloves kutoa huduma ya kujifungua au ukunga. Bila misaada nchi haiendi.

Unapotembea juu ya yanayojiri, angalia mbali na sio chini au unachokiona karibu.

Chambua mwenyewe ujiridhishe. Au mnasemaje. Changia, kwanini ripoti imekubalika kusomwa.
 
Kusomwa ni hatua ya kwanza lakini wanachohitaji hawa wahisani ni kuona wote waliohusika wanachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha hizo.
 
Spika amenukuu kipengele kinacho mluhusu kuendelea na mjadala na kusema hawapokei mambo kama hayo wakati kikao kikiendelea na pia kasema kwamba hata leo asubuhi walikuja kuleta hiyo injunction na hawakuipokea...
 
Mimi hii nimeiona toka zamani lazima iwekwe wazi na mpunga urudi

Mpunga ukirudi utaliwa na wakina nani au wananchi watapewa asilimia ngapi na wajanja asilimia ngapi? Je kweli kuna uzalendo?
 
Kusomwa ni hatua ya kwanza lakini wanachohitaji hawa wahisani ni kuona wote waliohusika wanachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha hizo.

Kwenye wekundu kuna usemi usemao "kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi". Hivyo hata wakichukuliwa hatua nadhani wataendelea kuvjiijisent bila matatizo, na kurudi kwenye viwanja vyao.
 
Some truth mkuu...we have to think out of the box

Na kupata permanent solution, na sio kutafuta. Na sio maneno matupu yasio vunja mfupa. Tuna sifa ya kuzungumza sana bila ufumbuzi wa changamoto zetu.

Tunazungumza sana bila kutenda.
 
Sababu ingine ni wana... wakubalike na wananchi kwenye uchaguzi ujao, na sio kutatua tatizo lililopo la kutokuwa na uzalendo wa kweli.

Hivyo labda watakubalika na kuendelea kutawala au mnasemaje wana JF?

Je wakipita watawanufaishwa wananchi au? mimi sio mfuasi wa vyama bali ni mpenda uzalendo, upendo na haki.
 
Hapo kale kamfumo kasiko rasmi kanakonyonya serikali alikozungumzia Sheikh Ilunga kameguswa.

Udhalimu, uovu hauna dini (wahalifu wengine wanavaa kofia ya ukristo, uislamu wengine hawana dini), utawaona tu kwa matendo yao mabaya.
 
Jana kuna habari zilirushwa kwenye stations za TV za upotevu wa computers za thamani ya milion mia mbili zilizopotea toka muda mrefu. Wahisani walio donate walipokuja kutembea na kuzikuta zimepotea waliamua kusitisha kutoa msaada. Na Mkuu wa Mkoa akiwa na wazungu akatoa kauli kuwa lazima wahusika wata wajibishwa.....

Msaada huo ulilengwa kwa shule.

Kwanini hakujua hilo toka muda mrefu, hadi wazungu waje ndio apate ufahamu?

Mgeni uje mwenyeji apone, suala hili ni halina tofauti na la ESCROW. Hivyo tatizo lipo toka chini hadi juu.
 
Kusomwa ni hatua ya kwanza lakini wanachohitaji hawa wahisani ni kuona wote waliohusika wanachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha hizo.

Na hapo ndio patamu sana!! Hii sio sawa na RICHMOND watu wanajiuzuru baada ya wizi halafu wanatumia hela walizoiba kutoa misaada makanisani na misikitini ili kutengeneza mazingira ya 2015!
 
Na hapo ndio patamu sana!! Hii sio sawa na RICHMOND watu wanajiuzuru baada ya wizi halafu wanatumia hela walizoiba kutoa misaada makanisani na misikitini ili kutengeneza mazingira ya 2015!

Kuna ukweli.. pia kuna mwingine amerudi na kutunga kinachokataliwa. Amerudi bila kupitia makanisani na misikitini. :angry:

Na kuna mwingine alishatabiriwa kuwa ni anakubalika sana kuliko wengine wote. Na hakuna wakumpiku. Je ni kweli ni mzalendo?

Kwa lililotokea leo Mh. Makinda na Zitto wamepanda chart hivyo CCM pia imepanda chart, si ndio uchaguzi umekaribia? au sio. Mtaona tu watakavyo sifiwa. Pima je ni kweli au ni mchezo wa kuigiza?

Hili pia yaweza kuwa ni sababu ya ripoti kupita kiulaini bila ya pingamizi.
 
Jana kuna habari zilirushwa kwenye stations za TV za upotevu wa computers za thamani ya milion mia mbili zilizopotea toka muda mrefu. Wahisani walio donate walipokuja kutembea na kuzikuta zimepotea waliamua kusitisha kutoa msaada. Na Mkuu wa Mkoa akiwa na wazungu akatoa kauli kuwa lazima wahusika wata wajibishwa.....

Msaada huo ulilengwa kwa shule.

Kwanini hakujua hilo toka muda mrefu, hadi wazungu waje ndio apate ufahamu?

Mgeni uje mwenyeji apone, suala hili ni halina tofauti na la ESCROW. Hivyo tatizo lipo toka chini hadi juu.

Yaani uchafu umekithiri hakuna tena mahali pasafi nchi hii. Kuna zile 8bn zenye utata eti zilitumika wakati wa kumpokea rais Barack Obama wakati hata toilet papers alikuja nazo. Kuna 450 bn zilipotea hazina katika mazingira ya kutatanisha hadi leo kimya. Yaani we acha tu.
 
Nadhani kesho Professor atajiuzuru mwenyewe na watasema sasa tatizo limeisha tatuliwa. Hivyo hivyo tulifikiri wakati wa Mh. Lowasa alipojiuzuru. Matatizo nina uhakika kuwa hayatajiuzuru.
 
sababu kubwa ni kwamba ,rais kikwete amemwambia maikinda aruhusu iyo kitu bila kujali hata mahakama kwasababu misaada imezuiwa, serikali haina hela kabisa wafanyakazi wanaumia na bila suala hili kujadiliwa WAHISANI WALISEMA MSAADA HAUTOKI. ccm walishikwa pabaya.
 
Hali ya huduma za afya zinasikitisha sana. Na waganga wa jadi ndio nyakati zao za kujitangaza na kuvuna, pia mitume na wachungaji feki (eti kuombea wagonjwa ndio lengo lao kuu), utapeli mtupu.
 
Wakati ripoti ikisomwa Prof. Mhe. Waziri wa Nishati na Madini alikuwa anacheka na sio kutabasamu. Hii inamaanisha nini?
 
Back
Top Bottom