Hitimisho lako bila shaka ndio kilichoko mbeleni..itakuwa ni ujanja tu umefanyika pengine kumpumzisha na kumuandaa vyema zaidi nje ya OT!!Mtazamo wangu ni tofauti kidogo,
Kwanza nakubali kwamba Giggs ni moja ya ma-legend wakuheshimia pale OT, mchango wake ni jambo lisiloweza kufutika kamwe. Uwepo wa Giggs pale OT ulikuwa ni muendelezo wa uwepo wa falsafa za sir AF. Hivyo ilikuwa ni changamoto kwa timu kuweza kuondokana na falsafa za Sir. FA
Nionavyo mimi, ni jambo jema kwa maendeleo ya Manchester United kumuondo Giggs kwa sasa hasa kutokana na ukweli kwamba tayari kama timu wameshaamua kuchukua uelekeo mwingine. Misuguano iliyokuwepo wakati wa Moyes na pia wakati wa LVG ni ishara tosha ya ukinzani wa kifalsafa uliokuwepo.
Si vibaya kuanza upya, na sintashaangaa huko mbeleni Giggs kurudi kuchukua mikoba rasmi.