Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Taarifa za habari katika vyombo mbalimbali vimenukuliwa vikisema kwamba kuna wanachama wa chama cha mapinduzi CCM ambao walikuwa wamejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwapata wagombea nafasi za Ubunge wa Afrika mashariki (EALA) kwamba walitoa Rushwa ili wapitishwe na ngazi za maamuzi za chama cha mapinduzi CCM.
Amenukuliwa Msemaji wa chama hicho Ndugu Humphrey Polepole kwamba wanachama hao wa CCM watapewa adhabu, au kuwajibishwa na kamati ya maadili ya chama hicho; Kwa tafsiri nyingine, Bwn. Polepole amekubaliana na ukweli kwamba wapo wanachama waliotoa Rushwa.
Sote tunafahamu kwamba Rushwa sio suala la upande mmoja, bali pande mbili, mtoaji na mpokeaji, na hili liliwekewa mkazo hata muasisi wa Taifa letu hayati Mwl. Nyerere kwamba mtoaji na mpokeaji wa Rushwa wote wana hatia.
Maana yake ni kwamba, wanachama hao wanalo kosa la jinai la kutoa Rushwa, lakini pia viongozi waandamizi wa CCM pia wanalo kosa la Jinai la kupokea Rushwa, maana yake wote hawa wametenda makosa ya jinai, na wanapaswa kuwajibishwa mbele ya macho ya sheria za nchi yetu.
Chama cha mapinduzi CCM kimekuwa ni kichaka cha kuwafichia watoaji na wapokeaji wa Rushwa, Kwa kisingizio kwamba watawajibishwa na kamati za chama hicho za maadili, huu ni zaidi ya uhalifu, kwanini Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndiyo isiingie kuchunguza na kuwakamata wahusika wote kisha kuwafikisha mahakamani na sheria ichukue mkondo wake? Inamaana hata Chama hicho kikibaini wanachama wake wanajihusisha na Madawa ya kulevya, Ujangili, Ufisadi, n.k. kitawawajibisha kwenye kamati za chama na kuzuia mamlaka husika za nchi kuwawajibisha Kwa mujibu wa sheria?
Hii haikubaliki, na watanzania wanapaswa kufahamu kwamba nchi yetu inashindwa kuvishinda vita hivi dhidi ya Rushwa na Ufisadi, Kwa sababu Chama kilichounda serikali ndiyo wadau wa kubwa wa jinai hizo, na wanalindana vikali.
Wenu katika demokrasia na maendeleo