Rushwa imepanda bei

blo

Member
Joined
Mar 13, 2017
Posts
37
Reaction score
52
Rushwa hasa katika level za chini za watumishi waserikali hususani trafiki police, hospitalini, wizarani, TRA, Bandarani zimepanda bei kwa kasi sana mfano trafiki anakukamata anakubambikia makosa anakuambia akuandikie Tsh 60,000 au umpe Tsh 30,000 aweke mfukoni.

Rushwa ni adui wa haki, kataa kutoa au kupokea rushwa.
 
Kama unaona umebambikiwa kwa nini huripoti kwa RTO??? Kuna mwananchi mmoja aliona mambo yamezidi. aliripoti, ukawekwa mtego na jamaa akanaswa. Ukweli, sioni tija ya kulalamika maoni yangu ni kuwa aidha ingia kwenye mtego wa kuumizwa au ripoti hata takukuru
 
Unakataa mwende mahakamani tu
 

Mkuu fikiria nje ya box. Watu wako katika mazingira tofauti. Si kila mtu anaweza kufika kwa RTO kama inavyoweza kuwa rahisi kwako. Kuna watu wako mamia ya kilometa toka anakopatikana RTO. Kuna watu wako safarini. Mazingira yako tofauti sana.

Kimsingi askari trafiki ni kero kubwa sana asiyeiona hiyo labda kama yeye haguswi nao yaani labda yeye mwenyewe ni polisi au kiongozi mkubwa wa serikali.

Kuweza kuweka mambo sawa kulikuwa na haja ya kuainisha makosa kwa adhabu waziwazi na kuwaweka hawa jamaa wasiwe na uwezo wa kuja na makosa yao kama wanavyoona wao. Iweje misahafu iwe na amri kumi lakini makosa ya hawa jamaa ni indefinite? Kila uchao wanakuja na jipya. Yote hiyo ni kupembejea rushwa au kufikisha malengyo yao wanayojiwekea kinyemela kwa maslahi yao binafsi huku wakitoa machozi ya mamba kuwa wanapigania usalama wa raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…