Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 19,953
- 34,446
Dr J Magufuli tumbua jipu la askari wa usalama barabarani.
Kwa muda mrefu sana askari wa usalama barabarani wamekuwa wakichukua rushwa utafikiri nchi hii yao pekee yao.Ukisafiri kati ya Arusha mpaka Dar njia nzima imejaa trafic police wengine wana tochi kwaajili ya mwendo kasi,wengine kwaaajili ya kukagua bima,road licence,leseni ya madereva na nk.
Siku za hivi karibu hasa baada ya tukio la Kabuku trafic police wamekuwa na usongo wa kukamata hovyo magari kwa makosa mbali mbali.yakiwemo mwendo kasi,bima na nk.
Tatizo langu kubwa ni kama mapato yatokanayo na makosa ya usalama barabarani yanafikishwa sehemu stahiki (hazina ya serekali)Kuna siku nilikuwa natokea Moshi kufikka maeneo ya kambi ya chupa nikaovertake trafiki wakanikamata wakaniandika faini nikasema sawa lakini nikawaambia sina cash nitawaandikia cheque wakagoma ikabidi niagize cash toka mjini ndio wakachukua tsh 30,000/=.
Wakati nasubiri cash kama dk 20 hivi nikashuhudia magari kama 55 yakitozwa faini kwa makosa mbali mbali eg kutofunga mkanda,leseni,kadi ya gari,mwendo kasi na nk nikabaki nashangaa kama dakika 20 trafic polisi wa sehemu mmoja wameweza kuingiza tsh 1,650,000/ kwa dakika 20 kwa muda wa saa moja wataweza kuingizia serekali wastani wa tsh 5 million hicho ni kituo kimoja mkoa wa Arusha ukienda Njiro maeneo ya Relini wapo,Mbauda wapo,Sakina wapo,Uhuru road wapo chukulia wameweka kambi saba eneo ya jiji la Arusha wana wameamua kufanyakazi masaa nane trafic watakuwa na uwezo wa kukusanya tsh 280,000,000/= kwa siku moja ukifanya mahesabu ya mwaka utakuta wana uwezo wa kukusanya mapato ya tsh 102 billion katika eneo la jiji la Arusha pekee yake.
Chukulia maeneo mengine kama Jiji la DarMwanza,Tanga na barabara kuu zinazouganisha mikoa na wilaya mbali mbali............,.. utagundua makosa ya barabarani kama yatasimamiwa vyema ni chanzo kikuu cha mapato ya serekali.Ukienda Dubai utakuta makosa mbali mbali ya barabarani yanaingiza mapato makubwa serekali kuliko hata kodi.
Kwanini nasema serekali imeacha kuangali makosa ya barabarani kama chanzo kikuu cha mapato yake.Muda nilioakaa wakati nasubiri kuletewa fedha nilishangaa trafic polisi wakitumia magari binafsi (magari yao) kuyakimbiza magari yaliyokaidi amri ya kusimama !Nikajiuliza maswali mawili makuu.
a, Fedha za mafuta wanatoa wapi ?.Je lipo fungu maalum kwaajili ya kazi hiyo au wanajitolea tangu lini trafic wameanza kuonyesha uzalendo kiasi hicho.
b,Ni kwanini hawataki kupokea cheque ambayo fedha ya uhakika zaidi kufika kwa mlengwa (hazina) RPC Arusha.
c, Ni kwanini hakuna utaratibu wa kutangaza mapato yatokanayo na makosa barabarani ki wilaya,mkoa na kitaifa.
d, Vitabu (ERV) vinapokea malipo ya cash na cheque ni kwanini trafic polisi wanasisitiza cash.Je hivi vitabu vina control nzuri ya kueleweka.Mbona tunafanya malipo ya aina nyingi tunatumia cheque na sasa hata mpesa mfano malipo ya Road licence tunalipia kupitia mpesa.
Hili suala la kulipia malipo hasa kodi mbali mbali tunalipa direct bank eg TRA tunalipa VAT,Corporate tax,PAYE,SDL,Withholding tax & Stamp duty online payment ni kwanini IGP kwakushirikiana na Commissioner general wa TRA wasianzishe mfumo wa kulipia makosa ya barabarani kwa mpesa or online payment ili kuondoa matundu makubwa na uwezekano wa mapato kupotea kama walivyofanya TRA.
e, Ni kwanini TRA na jeshi la Polisi mpaka leo hawajaanzisha utaratibu wa kutumia mashine za EFD au polisi wamegoma kama wafanyabiashara wa Kariakoo ?.Hii ni serekali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dr Magufuli ambaye ameonyesha nia ya kutukwamua watanzania wote bila kujali itikadi au dhamana tunatakiwa kumsaidia.Kamishna mkuu na IGP wahkikishe mashine za EFD zinakuwa introduce January 2016 bila kikwazo chochote.
Askari wa usalama barabarani kazi yao iwe kubaini makosa tu na si kukusanya mapato ya serekali.Sisi watumiaji wa barabara tuko tayari kulipa faini mbali mbali tena kwa furaha kuwa iwapo tutajua fedha tunazolipa zinakwenda mahali stahili na si kwa wajanja wachache ambao sasa wanatumia magari yao binafsi kukimbizana na magari ya wakosaji huu ni uhuni uliovuka kiwango cha kuvumilika tufike mahali tusema nchi hii yetu wote lazima tuheshimiane.
f. Tumesoma kupitia vyombo vya habari juu ya askari wa usalama barabarani feki aliyekuwa akikusanya fedha kwa makosa ya barabarani.Kwa maana hiyo hata vitabu vilikuwa feki,askari feki na fedha zilikuwa zikiishia mifukono mwake si hazina ya taif Kama askari alikuwa feki na vitabu feki je haupo uwezekano wa kuwa na askari wa kweli lakini mwenye kumiliki vitabu (ERV) feki !!!!!!!.
Mimi naona uwezekano ni mkubwa sana hivi vitabu vinatumika katika idara nyingi za serekali Afya,Polisi,Mahakama,Elimu ..... vyote vina pigwa chapa na mpiga chapa mkuu wa serekali vingine vinakuwa na makosa mbali mbali ni rahisi sana mfanyakazi wa serekali wa idara ya mahakama kumpatia mfanyakazi wa idara ya magereza au polisi kama idara mojawapo itakuwa na upungufu au mtumishi mbadhirifu kutoa kitabu hicho kwa manufaa yake.Vitabu ERV vianweza kutumika idara yoyote ya serekali kama nilivyo ainisha hapo juu internal control system ni mbovu kweli kweli ndio maana nasema dawa ya kuondokana na hili tatizo ni kuhamia tknologia ya kisasa.
Nawasilisha