Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Rufiji. Watu watatu wamefariki dunia kwa kuzama majini na mmoja kunusurika kifo baada ya mtumbwi waliokuwa wakivukia kuzama bwawani wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo, Ofisa Tarafa ya Ikwiriri, Suleimani Mpangile aliwataja marehemu hao kuwa ni Sijali Abdallah (14), Zuberi Penya (11) wakazi wa Umwe Ikwiriri na Salehe Saidi (31) mkazi wa Dar es Salaam.
Mpangile pia alimtaja aliyenusulika kifo kuwa ni Musa Mkamba ambaye alikuwa akiwavusha marehemu hao.
Alisema chanzo cha vifo hivyo ni mtumbwi waliokuwa wakivukia kujaa maji na kuzama jana Jumamosi saa 3 asubuhi katika bwawa hilo la Umwe.