Kama unakumbuka Rostam aliwahi kukiri kupitia kwenye vyombo vya habari kwamba utajiri wake una asili tangu enzi za miaka ya 1890. Baadhi yetu tukaibua hoja kwamba wakati wa miaka hiyo ni serikali gani iliyokuwa inatambuliwa na Watanganyika (Tanzania Bara)? Je hizo mali za miaka 1890 ambazo ni mwendelezo wa hadi za leo ni halali kwa Rostam? Na kuna Makala iliwahi kuchapishwa MwanaHalisi ikiwa na kichwa kisemacho 'Rostam ni Nani?' mwandishi akiwa ni Mbasha Asenga ikifafanua hili kwa kirefu.