Ronaldinho aonekana akichezea Mexico World Cup jana!

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Gang Chomba upo? Hatimaye ule utabiri kuwa Dogo Geovanni Dos Santos ndiye atakayemrithi Ronaldinho Gaucho umetimia. Dogo huyo ambaya kwa muda mrefu amekuwa akifananishwa na kujifananisha na Ronaldinho jana aliudhihirishia Ulimwengu kuwa yeye ndio Gaucho mpya alipowazungusha Wafaransa huku akiwa amefunga nywele zake kama Dinho. Cha kuvutia zaidi ni kuwa huyu dogo anakaba na kukimbiza kuliko Dinho. Anachotakiwa sasa ni kuongeza tabasamu na kicheko kama Dinho. Naamini mtangazaji wa mechi ya jana, Arsene Wenger, atakuwa ameshaanza taratibu za kumsajili dogo huyu kutoka Galatasaray!
 
he is still tottenham hotspurs player

Mkuu heshima mbele...
Unapomzungumzia Dinho ukae unajuwa kuwa unamzungumzia Balozi wa soka la Mbinguni.

Dos Santos anajifananisha na Gaucho, lakini watu tunaomjuwa Gaucho tunapinga.

Dogo anajitahidi, ila ana safari ndeefu ya kufikia kiwango Cha the saint. Na safari yake ni ya Bajaj wakati Dinho yuko ndani ya Ndege. Je atamkamata?

ALIPATA KUNENA HAYA...
Ni heri uende porini kisha upambane na simba Dume kuliko kupewa jukumu la kumkaba Ronaldinho Gaucho uwanjani....
Maneno haya aliyasema Sergio Ramos.

So Dinho ni kiumbe hai hatari katika medani ya soka.
Huyo Dos santos hata akikenua na kucheka dakika zoooote but still hatoweza kuwa kama The Saint coz kuna vitu hajavifikia...

Forza Gaucho
Siempre Gaucho
No Gaucho
No Football
 
Gaucho..................!!!!!!?????
Huyu bwana noma anachezea mpira anavyotaka.........kukjosekana kwake kombe la dunia kumepunguza radha ambayo sisi wapenda na tunaojua mpira.......tungekuwa tunaoiona
 
du!afadhali mkuu maana nilidhani macho yangu yamepata matege coz kila nikimcheki dogo nahisi kama namuona Gaucho vile hadi nikaanza kutafuta miwani yangu niliyokua natumia nikiwa A- Level.yaani wanafanana kila kitu kasoro minjino tu.
 
Dogo kweli anatisha,i wish wenger asingekuwa mchumi atuletee haya madini pale emirates!!
 
du!afadhali mkuu maana nilidhani macho yangu yamepata matege coz kila nikimcheki dogo nahisi kama namuona Gaucho vile hadi nikaanza kutafuta miwani yangu niliyokua natumia nikiwa A- Level.yaani wanafanana kila kitu kasoro minjino tu.

Wewe humjui Saint Gaucho, na ndo maana ukatafuta miwani yako uliyokuwa unaitumia ulipokuwa east africa comunity.

Ila kwa sisi tunaomjuwa The Saint tunamfahamu hata kwa utulizaji wake mpira tu.

Huyo Dosantos mfananisheni na wapuuzi wenzie lakini si mtakatifu Gaucho ambaye kama mpira ungekuwa na Mdomo basi ungekuwa unaagiza upelekwe kwa Gaucho kwa Dakika zooote 90 ili mpira wenyewe ufurahi na nyie watazamaji mfurahi.
 
Back
Top Bottom