RIWAYA: YATIMA
MTUNZI :RAJU NUHADAMU
Simu : 0679296836
**SEHEMU YA KWANZA**
Mamu alikuwa ni msichana mzuri wa sura,mzuri wa umbo,na pia alikuwa ni mzuri wa tabia.
********************
Alizaliwa katika familia ya kimaskini,alikuwa ni mtoto pekee katika familia hiyo,kwa bahati mbaya wazazi wake walifariki akiwa na umri mdogo sana,baba yake alifariki akiwa na umri wa mwaka mmoja na mama yake Mamu akafariki,Mamu akiwa na umri wa miaka minne.
Mamu hakuwa na mtu mwengine wa kumlea zaidi ya bibi yake aliyekuwa akiishi kijijini,aliishi katika kijiji cha Nyamurunge mkoani tabora,kijiji kilichokuwa na hali ngumu ya kiuchumi.
Baada ya kumalizika harakati za mazishi ya mama yake Mamu,Mamu alichukuliwa na bibi yake kwa ajili ya kumlea,Mamu akaanza maisha mapya nyumbani kwa bibi yake.
Bibi yake Mamu alimpenda sana mjukuu wake,maana hakuwa na mjukuu mwengine zaidi ya Mamu,na pia alivutiwa na uzuri wa tabia ya Mamu,si hilo tu bali uwerevu wa Mamu pia ulimvutia,kwani Mamu alikuwa ni binti mwerevu. Kila alipofundishwa alifundishika na kila alichoelekezwa alielekezeka.
Maisha ya bibi yake Mamu yalikuwa ni magumu sana,alitegemea kilimo cha mkono,na mvua ya muumba,ukubwa wa umri wake ulichangia ugumu wa maisha yake kwa kiasi kikubwa. Rasili mali pekee aliyoona ampe mjukuu wake ni kumfunza kilimo,akiamini kuwa kilimo ndio kitakacho muwezesha kupambana na ugumu wa maisha.
Hakuwahi kufikiria suala la kumpeleka mjukuu wake shule,hata pale Mamu alipofikia umri wa kwenda shule. Na hata Mamu mwenyewe hakuwahi kufikiria suala la yeye kwenda shule.
Hata ile siku alipomuuliza bibi yake baada ya kuwaona watoto wenzake wakienda shule, bibi yake alimjibu hivi,
"Mjukuu wangu kipenzi,kwa sasa hivi mimi sina uwezo wa kukupeleka shule,hata hivo hakuna kitu cha maana utakachokipata huko shule,zaidi ya kupoteza muda,"
"Mbona nawasikiaga wakisema kuwa,ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA?"
"Mmh,mjukuu wangu,labda huo ufunguo huwa unatumikaga kufungia maisha,na si kufungua maisha,maana hao wanaoenda shule hatuoni cha maana wanachokipata",
Mamu alimsikiliza bibi yake kwa makini,
bibi akaendelea,
"wakati wenzako wakienda shule, wewe unalima mbogamboga na vitu vengine,baada ya muda unavuna na kuuza na kupata pesa,ambazo zinakusaidia kwa mahitaji mbalimbali",
"Kwani bibi, wao wakiendaga huko shule huwa hawapati pesa?"
"Subutu!!,labda wao ndio hutoa pesa",
"Bibi,huwa nawasikiaga wanasema,mtu akimaliza shule anapata kazi na analipwa mshahara kila mwezi",
"Hakuna kitu kama hicho mjukuu wangu,nani umemuona kamaliza shule akapata kazi?,wanahangaika hangaika tu huko mitaani,mtoto wa mama Angela,si kamaliza shule mwaka jana,kazi gani anafanya? zaidi ya kuwa hata kazi za shambani haziwezi?"
"Ni kweli bibi,tukiendaga nae shamba hata kulima hawezi, analima vibayavibaya."
"Sasa na wewe unataka kuwa kama yeye"
"Hapana bibi"
"Sasa hao wanaoenda shule,waache waende shule,wewe endelea kujifunza kulima,ukifika umri wa kumaliza shule,utakuwa mkulima hodari,utapata maendeleo mazuri."
Maongezi ya Mamu na bibi yake yalikomea hapo,Mamu aliamini sana mawazo ya bibi yake,aliendelea kujifunza kulima kwa juhudi zote,hakujua kusoma wala kuandika,wala hakuona madhara ya hilo,kikubwa alichokiweza ni kurudisha chenji halisi katika biashara zake za mbogamboga,kwa hilo alikuwa mahiri. Haikuwahi kutokea akaongeza au kupunguza chenji.
********************
Mamu aliendelea kuishi na bibi yake katika maisha hayo ya tabu kwa muda wa takriban miaka kumi,yalikuwa ni maisha ya tabu,lakini yalimkomaza Mamu kiasi cha kuwa na uwezo wa kutatua mambo kama mtu mzima.
Baada ya miaka kumi, bibi yake Mamu alianza kuumwa na hatimae akafariki,
"KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA"
yalikuwa ni maneno ya kumfariji Mamu yaliyosemwa na baadhi ya majirani. Ulikuwa ni msiba wa kuhuzunisha sana kwa Mamu,si tu kwa sababu ya kufiwa na bibi yake,bali bibi yake kwake alikuwa zaidi ya bibi,ni kama baba na mama yake. Hatimae Mamu akamzika bibi yake.
***SEHEMU YA PILI***
Mamu alijitahidi kuondoa mawazo juu ya bibi yake baada ya msiba ule lakini alishindwa,alijikuta akilia kila wakati,kila kitu cha pale nyumbani kilimkumbusha kipindi cha uhai wa marehemu bibi yake.
Alishindwa kuendelea na kilimo akiwa peke yake kutokana na udogo wake,na alishindwa kushinda nyumbani kwa sababu palikuwa panamuongezea huzuni.
Kila alipokiona chumba na kitanda cha bibi yake vilikuwa vinaurudisha msiba upya moyoni mwa Mamu.
Mamu akalazimika kuwa anatoka nyumbani nyakati za asubuhi,na kuzunguka zunguka bila ya mpangilio maalumu,au wakati mwengine alienda nyumba ya jirani yao aliyeitwa mama Angela,na kumsaidia kazi ndogondogo, na Jioni kurudi nyumbani.
Alifanya hivo ili kupunguza mawazo,lakini ilikuwa ni kama anatwanga maji kwenye kinu,kila aliporudi nyumbani nyakati za usiku alijikuta akilia mpaka akipitiwa na usingizi bila ya kujitambua.
Ikawa ndio ada yake,mchana kuzunguka na usiku kulia,kitu kilichopelekea mwili wake kuanza kupungua. Hakiba ndogo ya pesa na chakula alichoachiwa na marehemu bibi yake vilikuwa vinakaribia kuisha.
*******************
"Nitaishi hivi mpaka lini?"
Siku moja Mamu aliwaza baada ya kuamka kutoka usingizini. Aliinuka na kwenda kuangalia hakiba yake ya chakula akaiyona ni ndogo sana,kama angeibana sana isingezidi siku tano.
"Kila kukicha hapa nyumbani pananiongezea simanzi,chakula ndio kinaishia na pesa ndio inaishia,"Mamu aliwaza.
"Nikiendelea kukaa hapa sitaweza kufanya chochote cha maana,sitaweza kuendelea kulima maana msiba wa bibi unajirudiarudia kichwani kila kukicha,"
Mamu aliendelea kuwaza lakini alikuwa na kipindi kigumu cha kuamua nini cha kufanya. Pamoja na umri wa miaka kumi na nne aliokuwa nao, alikuwa na uwezo wa kufikiri kama mtu mzima tena aliyekomaa kimaisha,hii ni kutokana na kukomazwa na bibi yake kimaisha akiwa bado ni binti mdogo.
"Ni lazima nifanye jambo,itanibidi nihame hapa,siwezi kuendelea kukaa tena hapa",
Mamu aliwaza,kwa kupata wazo hilo alijikuta kana kwamba amepata suluhisho la tatizo lake. Lakini swali la msingi likazuka,"nikihama hapa nitahamia wapi?".
Lilikuwa ni swali gumu mno kwa Mamu,kwani hakukuwa na ndugu yake mwengine anemjua aliyebakia katika dunia hii. Aliendelea kutafakari kwa muda,mara akakumbuka kitu.
Akakumbuka kuwa, siku moja bibi yake aliwahi kumwambia kuwa alizaa watoto wawili,mmoja wa kiume na mwengine ni wa kike. Mtoto wa kiume ndie baba yake Mamu,na mtoto wa kike ni mdogo wake ambae ni shangazi yake Mamu.
Mamu alijikuta akichangamka ghafla baada ya kukumbuka kuwa alikuwa na ndugu aliyekuwa hai katika hii dunia ambae ni shangazi yake. Mamu alipata nguvu ya kupika na kufua nguo zake kwa kipande kidogo cha sabuni kilichobakia. Baada ya kumaliza kufua akala,kisha akaamua kupumzika huku akiendelea kutafakari kuhusu shangazi yake.
Swali la kwanza alilojiuliza ni kuwa atawezaje kumpata shangazi yake,maana hakujua ni wapi anapoishi,na hata angejua anapoishi, angempataje maana hajawahi kumuona hata kwa mara moja na wala hamjui hata jina lake.
Alijikuta akipata kibarua kipya cha kufikiria namna ya kumpata shangazi yake huyo asiemjua kwa sura wala kwa jina. Alitafakari kwa muda mrefu akitarajia labda anaweza kupata angalau mwanga wa ufumbuzi lakini hakufanikiwa,alijikuta akipitiwa na usingizi bila ya kutarajia.
Aliposhtuka ilikuwa ni nyakati za usiku sana,akaamka, akaenda chooni kujisaidia na kisha kurudi kitandani ambapo alikaa kitandani kwa muda mrefu akitafakari mpaka mwanga wa jua la asubuhi ukaanza kuonekana.
Alihisi njaa sana wakati ule wa asubuhi,aliinuka na kupiga mswaki kisha akakiendea kiporo chake cha ugali na kachumbri ya jana ya nyanya tupu na akaanza kukishambulia. Alipomaliza alimshukuru Muumba kwa riziki ile, kama alivofundishwa na marehemu bibi yake.
Ulikuwa ni mlo aliouzoea katika maisha yake, tangu kipindi cha uhai wa marehemu bibi yake,baada ya kushiba alijikuta kichwa chake kikichangamka kidogo. Baada ya kutafakari kwa muda kidogo akakumbuka kitu. Kuna siku bibi yake alimwambia ,
"Shangazi yako anakusalimia",Mamu akamuuliza bibi yake,
"Umeonana nae wapi?"
Bibi akamjibu
"Hapana mjukuu wangu sijakutana nae,nimewasiliana nae,huwa nawasiliana na shangazi yako japo mara mojamoja sana".
Mamu alipoyakumbuka maongezi hayo yaliyojiri baina yake na bibi yake alijikuta anaanza kupata wepesi wa jambo lake.
Pamoja na kuyakumbuka maongezi hayo,alibakiwa na kitendawili kigumu alichoshindwa kukitegua ambacho ni,"njia gani bibi aliitumia kuwasiliana na shangazi?",alijaribu kurudisha kumbukumbu zake kwenye maongezi aliyoyakumbuka muda mchache uliopita pengine bibi yake aliwahi kumuambia njia ya mawasiliano aliyokuwa akitumia,lakini hakuambulia kitu. Alijaribu kuifikiria njia ya simu,lakini akaona haiwezekani. Hiyo ni kwa sababu kijiji kizima simu iliyokuwapo ilikuwa ni moja tu,na mtu aliyekuwa nayo alikuwa ni mwalim mkuu wa shule ya msingi.
Mwalimu huyo alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya sana,na ikitokea akakupa simu yake, jiandae kudhalilishwa vilivyo.Mamu alikumbuka vizuri kuwa bibi yake hakuwa tayari kudhalilishwa na mtu yoyote kutokana na umaskini wake.
" hata siku moja sitoenda kuomba simu,sipo tayari kudhalilishwa na kijana mdogo kama yule,hata hivo sina mtu wa kumpigia simu"
Mamu aliyakumbuka vizuri maneno hayo ya bibi yake,akajikuta anazidi kupata mkanganyiko,
"kama bibi hakuwa akitumia simu kuwasiliana na shangazi,ni njia gani nyengine aliyokuwa akitumia?au alinidanganya".
Mamu alijiona mjinga sana kwa kutomuuliza bibi yake njia aliyokuwa akitumia kuwasiliana na shangazi yake,lakini angewezaje kumuuliza kipindi kile wakati bado alikuwa mdogo,hata hayo mawasiliano hakuyajua vizuri kipindi hicho kuwa ni kitu gani?.
Mamu alijikuta yupo kipindi kigumu mno,kila anapopata mwanga kinafuatia kiza kizito mno kuliko hata kiza kilichotangulia.
Alijikuta akianza kujuta kumkumbuka shangazi yake,hakuona faraja aliyoitarajia zaidi ya msongo wa mawazo kuongezeka.
Ghafla aliona machozi yakimtoka, hakujua ni machozi ya hasira au ya huzuni au mchanganyiko wa hasira na huzuni. Machozi yalifuatiwa na kilio cha kwikwi,alilia kwa muda mrefu mpaka akahisi kichwa kinamuuma. Aliendelea kulia kwa muda mrefu mpaka alipitiwa na usingizi.
Alipoamka ilikuwa ni Jioni,akainuka kutoka kitandani na kuamua kutoka nje ya nyumba ili angalau apate jua la Jioni. Akaamua kukaa nje kwenye kigogo cha mti ambacho alikitumia kukaa wakati akiosha vyombo tangu enzi za uhai wa marehemu bibi yake.
Alipokaa pale kwenye kigogo mara akakumbuka kitu,akakumbuka tukio lililotokea miaka kadhaa iliyopita,lilikuwa ni tukio muhimu sana kwake kwa kipindi kile,tukio lenyewe lilikuwa hivi,
Siku moja Mamu alikuwa nje anawasha moto nyakati za Jioni kwa ajili ya chakula cha usiku baada ya kutoka shamba. Mara akatokea kijana wa makamo,
"Bibi yako yupo?",yule kijana aliuliza,
"ndio yupo",Mamu alijibu,"mwambie anaitwa na mwenyekiti nyumbani kwake",yule kijana akaagiza.
Mamu akaingia ndani haraka na kumpa bibi yake ujumbe wa wito aliopewa na yule kijana. Bibi yake akamuuliza,"huyo kijana yuko wapi?",
"Nimemuacha hapo nje",Mamu akajibu. Bibi akatoka haraka kumuwahi yule kijana,alipofika nje akamuona yule kijana akimsubiri,
"Wewe mtoto,ni kweli umetumwa na mwenyekiti uje uniite?",bibi alimuuliza yule kijana,
"Ndio",yule kijana alijibu kwa mkato.
Bibi akamgeukia Mamu akamwambia,
"nawa mikono yako haraka tuondoke",
"Kwani bibi kuna nini?"
"Itakuwa ni shangazi yako tu"
"Shangazi amekuja?"
"Fanya haraka twende,utaona huko huko". Mamu na bibi yake wakaondoka haraka wakaelekea nyumbani kwa mwenyekiti.
Walipofika wakakaribishwa vizuri na mke wa mwenyekiti. Mara akaingia mwanaume mmoja ambae ni mtu mzima wa makamo asiyekuwa mzee.
Yule bwana akamsalimia bibi yake Mamu,"Shikamoo mama","Marahaba mwanangu,nimesikia unaniita, nimekuja kuitikia wito".
Mwenyekiti na bibi yake Mamu wakaanza mazungumzo. Kipindi chote cha mazungumzo Mamu alikuwa akipepesa macho huku na huko,hakuwa makini na chochote kilichokuwa kikiendelea pale.
Kikubwa alichotarajia ni kuwa baada maongezi yale atatokea shangazi yake ili wamchukuwe waondoke nae nyumbani kwao. Alikuwa na hamu sana ya kuonana na shangazi yake,hasa pale alipokumbuka kuwa bibi yake aliwahi kumwambia kuwa shangazi yake amefanana sana na kaka yake yaani baba yake Mamu,na pia aliwahi kuambiwa kuwa yeye Mamu amefanana na baba yake. Kwa hiyo alijua fika kuwa yeye amefanana na shangazi yake.
"Twende Mamu",bibi yake Mamu alimwambia mjukuu wake baada ya kumaliza maongezi yake na mwenyekiti.
" Bibi,shangazi yuko wapi? mbona hatujamchukua?" Mamu alimuuliza bibi yake,
bibi akamjibu
"Mamu,shangazi yako hajaja",
Mamu akauliza,
"kwani bibi tulienda kule kufanya nini?"
" shangazi yako alikuwa ametuma barua"
"Barua ndio nini bibi?"
"Barua ni maadishi, yanaandikwa kwenye karatasi kisha yanatumwa kwa yule anaetumiwa barua"
"Inatumwaje?"
"Kama sehemu kuna sanduku la barua,wanatuma kupitia sanduku la barua. Kama hapa kwetu hakuna sanduku la barua kwa hiyo huwa zinatumwa kwa njia ya treni, mwenyekiti anapoenda stesheni iliyopo hapo kijiji cha jirani huzichukua na kuja kumpa kila mtu barua yake. Lakini kwa wale wasioweza kusoma kama mimi huwa wanaitwa nyumbani kwa mwenyekiti,na mwenyekiti huwasomea barua zao. Kama mtu hahitaji kuijibu barua yake anamshukuru mwenyekiti na kuondoka. Lakini kama mtu anahitaji kuijibu barua yake kama mimi leo anasema maneno anayotaka kutuma na mwenyekiti anamuandikia kwenye karatasi na kuituma kama barua"
Tukio hilo liliishia hapo.
Kumbukumbu ya tukio hilo iliamsha uchanagamfu mpya kwenye kichwa cha Mamu.
ITAENDELEA......
Riwaya hii itakuwa itakujia hapa jukwaani mara mbili kwa wiki,itakujia jumamosi saa 5:00 asubuhi(11:00 am) ,na jumapili saa 10:00 Jioni (04:00 pm).