Deadbody
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 4,274
- 6,592
SITAISAHAU TANGA: SEHEMU YA 1
Nikiwa kwenye mishe zangu za research kwenye mji wa Tanga, ilikuwa ni research ya siku kumi na nne. Jioni ya siku ya pili nikakatisha sehemu flani hivi mjini hapo kuangalia na kutembea tembea, lahaula nikakutana na binti mmoja wa kuvutia sana kwakweli nikajikuta nikivutiwa naye alikuwa mweupe sana na nywele ndefu na umbo kama la mamiss hivi dah nikaona hapa ndio penyewe yani kwani alikuwa na ugonjwa wangu mkubwa unaonivutia kwa wadada nao ni rangi nyeupe. Sikutaka kupoteza wakati mtoto wa kiume ikanibidi nimsogelee ili niweze kumsabahi, tukasalimiana pale na kujuana majina na tukabadilishana namba. Basi ikawa kila jioni nakutana na yule binti, pesa yote namalizia kwake. Kwakweli nikampenda kwani alikuwa ni binti mzuri sana kama malaika aliyeshushwa hata demu wangu niliyemwacha Dar nikamsahau kabisa kwani hakuwa na mvuto kama huyu dada wa kitanga.
Baada Ya kumaliza ile research ya siku kumi na nne sikutamani kurudi Dar ila ilinibidi nirudi ili nikakabidhi kazi ya watu na nikasake mavumba ya ziada ya kunifaa kumchumbia yule binti wa kitanga.
Niliporudi Dar sasa ndio nilielewa ule wimbo wa "Tanga kunani pale".
Siku hiyo nikiwa kwenye chumba changu nimetoka kuoga mara simu ikaita kuichek ni yule binti wa kitanga.
MIMI: Hallow mpenzi
BINTI: Ndio mpenzi, mbona hujajisugua vizuri umeacha povu sikioni?
MIMI: (Nikachukua kidole na kugusa sikioni kukitoa kikatoka na povu), haa umejuaje mpenzi?
BINTI: Nimekuona hapo mpenzi wangu.
MIMI: (Nikiangalia kushoto na kulia), umenionaje?
BINTI: Usijari mpenzi, chukulia kawaida tu.
Baada ya simu kukatika, Dah nilikaa nikawaza na kuwazua nikaamua kupotezea tu. Nikavaa fastafasta, halafu nikaenda kununua msosi nikachukua na kilimanjaro moja nikashushia ili nilale vizuri. Mara simu ikaita,
BINTI: Mpenzi si nilikukataza wewe kunywa pombe?
MIMI: (Nikiwaza kichwani, majanga haya) mbona mi sijanywa pombe!
BINTI: Nimekuona mpenzi umekunywa bia moja.
MIMI: (Nikashtuka na kuangalia kushoto na kulia), aaah sijui eeeh kwani umejuaje?
BINTI: Fanya yote ila tambua hakuna utalofanya nisijue.
Halafu akakata simu, nikaanza kuwaza tena amejuaje kama nimekunywa? Au kasikia harufu ya pombe kwenye simu. Mara sms ikaingia kwenye simu yangu, kuangalia ni yule binti, sms iliandikwa "usiwaze sana mpenzi"
Itaendelea muda mfupi ujao..........