Riwaya.. Ningejua

May 2, 2017
6
2
Hadithi NINGEJUA 1

Mtunzi Christopher Adamu Kibona

Mahali Iringa, Tanzania

WhatsApp 0752773513/0683376813

Sehemu ya kwanza

"We mtoto embu amka, kulala gani huko mpaka saizi ?". Ilikua ni asubuhi ya jumamosi mama mmoja alikuwa anamuasha mtoto wake kwani alikuwa amelala kwa kupitiliza. Unajua wanafunzi wengi siku za wikiend huwa wanalala sana kiss hawaendi shule.

"Mama bhana na wewe me mwenzako leo ndo nataka kulala na we unakuja kuniamusha unanionea hivyo mama ungeniacha leo nilale". Mtoto alilalamika kwani hakupenda kuamka kwa muda huo japo muda ulikuwa umeenda sana ila yeye aliona ni halali kuendelea kulala.

"We embu amka huko, hata kama huendi shule unapaswa kuamka mapema ufanye kazi ndogo za hapa nyumbani, unakuwa kama siyo msichana". Mama mtu naye alilalamika kwa nafasi yake kitu kilichomfanya yule binti kuamka kwa kujilazimisha sana.

"Mama bhana yaani hakupi hata nafasi ya kupumuzika, yaani bora Dada angekuwepo ningekuwa nalala embu subiri aje". Aliongea akimaanisha kwani alikuwa mvivu sana kuamka ila akiamuka na kunywa chai huwa anapotea kama shilingi kwenye mchanga.

Alipoamuka alinawa uso na kusafisha meno yake " yaani mama kila nikitaka kupata raha ananiingilia nikija kutoka hapa nyumbani sijui kurudi nitarudi kwa manati" alendelea kuwaza kwani suala la yeye kuamushwa lilimkera kuliko kawaida. Baada ya kunawa alienda mezani akanywa chai na kwenda kumsaidia mama yake kusuuza vyombo.

"Hivi we litoto kwanini unakuwa mvivu hivi yaani unakua tu ila akili hata hazipanuki ndo zinazidi kupotea, hii kazi ya kuosha vyombo ilikuwa yako ila kwa kuwa hujielewi ndo maana naifanya ". Alipofika tu alipokelewa kwa kusemwa na mama yake, kwakuwa alikuwa na hasira aliamua kukaa kimya ili kuepusha Shari kwani alimjua mama yake kuwa huwa hachelewi kugawa kipigo.

Baada ya kumaliza kazi aliaga kama kawaida yake na kwenda kwa rafiki zake ili waweze kucheza japo kidogo. Walicheza kila mchezo na hatimaye walichoka na kupumzika.

"Jamani mnaonaje tukienda kuogelea, kwani kipindi hichi hakuna mvua nyingi tuende tufanye haraka ili kufika mchana tuwe tumesharudi". Yule mtoto alitoa wazo lililoungwa mkono na wenzake kadhaa, hao kama kumbikumbi waliongozana kuelekea kwenye dimbwi kuogelea. Walitumia muda mwingi kuogelea bila kujali kula walikuwa kama hawahisi njaa.

Walipokuwa wanaendelea kuogelea walishituliwa na sauti ya mmama ambaye daima huwa anapinga watoto kuogelea kwenye madimbwi.

"Nyie watoto mnafanya nini huku ikiwa kila siku nawakataza msije huku, hamjui hatari iliyopo kwenye hata madimbwi eeh. Mtapata magonjwa bure humu, si mnasoma ninyi hamujuwi maji yaliyotuama ni hatari kwa afya ya binadamu ?". Yule mama aliongea akikusanya nguo za wale watoto, alijua kwa namna yoyote lazima watakimbia hivyo alipochukua nguo walikosa namna ya kukimbia ilibidi wawe wapole.

"Samahani mama tusamehe bure hatuweze rudia tena kuja huku kuogelea". Waliongea hivyo tu ili awape nguo zao ila yeye alichukua fimbo na kuwachapa kama funzo kwa siku nyingine. Alipoona ameridhika kuchapa ndipo aliwapa nguo zao. Mama wa watu alikuwa anatoka jasho kama ametoka kukimbia kumbe kazi ilikuwa kuchapa watoto wa wenzake ila alifanya la maana kwani alikuwa anawakinga dhidi ya magonjwa pia dhidi ya kusombwa na maji.

"Yaani huyu mama ana roho mbaya sana, kuna siku ni kumpiga na mawe tu kwani me ananikera sana". Moja kati ya watoto aliongea kwa hasira.

"Unajua kisa cha kutuchapa ni nini, me najua kwasababu watoto wake hawajui kuogelea siku wakijua hata atakuwa hatupigi tena". Mtoto mwingine alichangia hoja ambayo wenzake walionekana kuikubali sana.

"Cha kufanya ni kuwachukua watoto wake na kuwafundisha jinsi ya kuogelea ili tuwe huru au mnaonaje jamani tukifanya hivi?". Walikubaliana kuwachukua watoto wa mama mkali ili nao wajue kuogelea wakidhani ndo itakuwa ponapona yao. Watoto walidhani hapo ndo wameamua vizuri walipanga jumamosi ya Juma lijalo ndo waifanye hiyo kazi.

"We Maria umetoka wapi, toka ulipoondoka asubuhi mpaka saizi ulikuwa wapi". Yule mtoto kwa jina la Maria aliulizwa na mama yake aliyekuwa hana mzaha wowote.

"Samahani mama nimekosa naomba msamaha sirudii tena". Alijua akiongea vitu vingine lazima angekula fimbo za kutosha toka kwa Mama yake.
********** *********
Maria ni msichana aliyezaliwa katika familia ya watoto wanne akiwa na Dada yake mmoja na kaka zake wawili yeye na wazazi wake wanakaa Dodoma mjini mtaa wa Area A. Dada yake ameajiriwa mbeya kama nesi na kaka yake mmoja anasoma chuo kikuu cha Dar es salaamu na mwingine anasoma shule ya sekondari Tosamaganga. Wamelelewa katika maadili mazuri na maisha yao ni maisha ya kawaida. Maria ni mtoto wa mwisho hivyo malezi yake yamekuwa tofauti na wengine wote. Kwani amefika darasa la sita akiwa hajui hata kuosha vyombo kitu kilichokuwa kinawashangaza ndugu zake.

Shuleni pia ni mzembe tofauti na ndugu zake ambao hawajawahi kufanya vibaya katika masomo yao, kitu hichi kimefanya Maria awe anaonekana tofauti na wenzake. Akiwa darasa la nne amewahishika nafasi ya mwisho darasani hali hii ilizidi kuwasikitisha wazazi wake .

Je nini kinafanya Maria awe tofauti na wenzake ????

Kujua yote usikose kuungana nami kesho jioni.

Kusoma riwaya zangu nyingine tembelea page yangu Facebook story za chriss
 
Mkuu samahani hebu fanya uzito flani hivi wa uelezeaji wa matukio(lugha iwe na uzito flani hivi wakuvutia) nafikiri itamakinisha zaidi watu kusoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom