mzaramo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2006
- 6,371
- 5,183
IMEANDIKWA NA:GEORGE IRON MOSENYA
SEHEMU YA 1
IMEANDIKWA NAYE: George Iron Mosenya
SEHEMU YA KWANZA
Maisha wakati mwingine si jitihada pekee zinazoweza
kukutoa sehemu moja kwenda nyingine, kuna wakati
bahati inahusika katika maisha.
Si kwa wote lakini mimi nilibahatika kuwa mtoto
kutoka familia ya kimasikini ambaye baadaye nilienda
kusoma na kisha kupata kazi nzuri ambayo ilinitoa
katika umasikini na kunitupa katika daraja la kati na
baadaye nikawa tajiri.
Nikayabadili maisha ya kizazi changu na kuwaweka
katika mirija ya kujiendesha wenyewe.
Hadi ninafikisha miaka thelathini tayari nilikuwa
nimeyaweka maisha yangu sawa, nikiwa nimesaidia
ndugu zangu kwa kiwango cha uwezo wangu pamoja na
marafiki pia.
Baada ya kutimiza ndoto hizi ndipo kwa mara ya
kwanza nikafikiria juu ya utulivu wa hali ya juu
niliokuwa nauhitaji na niliwahi kuuota tangu nikiwa
nasoma, nilijiahidi kuwa nitakapomaliza kuinyanyua
familia yangu sasa nitaangalia vyema maisha yangu.
Niliwahi kuwa na marafiki wa kike lakini sikuwahi
kunyanyua kinywa changu na kuwatamkia kuwa nina
nia ya kuingia nao katika ndoa.
Nilikuwa nina deni, sikutaka nijiongezee majukumu
mengi yatakayosababisha nishindwe kutimiza vile
nilivyopanga kutimiza.
Katika mkesha wa mwaka mpya nilimpigia mama yangu
simu na kumweleza bayana kuwa ndoto mojawapo
katika mwaka unaoanza ni kuyabadili maisha yangu
kwa kujihifadhi katika mji tulivu.
Akaniuliza iwapo nataka kuhama Tanzania, nikacheka
na kumweleza kuwa sina wazo la kuhama Tanzania bali
nahitaji kuingia katika mji tulivu.
“Unataka kuoa?” mama aliniuliza.
Nikacheka bila kumjibu chochote, naye akacheka kisha
akanitakia kila la heri. Nikampongeza kwa kuelewa
maana yangu upesi sana!
_____
Mwaka ulianza vyema na shughuli zikiendelea kama
kawaida huku lile wazo likiwa kapuni kusubiri
utekelezaji wake.
Naomba niweke wazi kuwa nilikuwa aina fulani ya
mwanadamu ambaye napenda sana kufanya jambo
kadri ya wakati, maana niliwahi kufanya mambo mengi
kwa wakati mmoja na kujikuta nikiharibu ama
kutoyafanya kwa ufanisi mambo mengine.
Hivyo sikuwahi kupanga siku ya kuusaka mji ule
tulivu!!
Siku hii ikiwa ni miezi miwili baada ya mwaka kuanza
pale ofisini kwetu palikuwa na nafasi za kazi zilikuwa
zimetangazwa na watu wengi sana walikuwa
wameomba nafasi. Katika ile hatua ya awali ya usahili
walifika wasahiliwa mia moja na hamsini.
Nafasi zilikuwa tano tu zilizokuwa wazi. Katika ngazi
ya mwisho kabisa nd’o ambayo mimi na wakurugenzi
wenzangu tulikuwa tunahusishwa lakini hatua za awali
walisimamia wenzetu waliokuwa na vyeo vya chini.
Baada ya hatua za awali hii siku ndiyo ilikuwa ile ya
kupata mbivu na mbichi.
Wasahiliwa ishirini wa mwisho.
Katika usahili nilikuwa natazamwa sana, hakika
sikuwa mtu wa mchezo, ukifanya vibaya usitarajie
kuwa nitakubeba kisa tu u msichana ama umeonyesha
huruma ya aina yoyote.
Sikuwa mtu wa aina hiyo kabisa, na kilichokuwa
kinanifanya niwe hivi ni njia ambazo nilikuwa
nimepitia, hakuna njia ya panya yoyote niliyopitia
katika safari yangu ya kimasomo hadi kutafuta kazi.
Na pia nilikuwa nina hofu na Mungu!
Kitendo cha kumpitisha mtu asiyekuwa na vigezo na
kumwacha mwenye vigezo kungeisononesha nafsi
yangu sana.
Katika usahili nilikuwa naogopwa sana.
Hata siku hiyo nilikuwa yuleyule, maswali yangu
yalikuwa si magumu lakini yenye mitego. Maswali
yangu yakiwa na nia moja tu, kuupima uelewa halisi
wa msailiwa.
Walipita wasahiliwa wote katika hatua ya kwanza,
niliwanukuu majina yao.
Baada ya hatua zote za usahili kumalizika hatimaye
tuliwaeleza kuwa baada ya majuma mawili tutawapigia
simu katika nambari walizotuachia.
Tukawaaga wakaondoka!!
Masuala ya usahili yakaishia hapo…..
Nikaendelea na shughuli nyingine hadi majira ya saa
tatu usiku ndipo niliifunga ofisi yangu na kutoka nje
kuelekea katika gari langu.
Nilifungua mlango na kuiwasha gari nikaiacha
ikiunguruma kwa muda huku nikiwa nimewasha
kiyoyozi ili kuleta hewa safi, mara nikasikia hatua
zikijongea nilipokuwa. Nikatambua huyo atakuwa
aidha mlinzi ama kijana mwingine tu amekuja
kuniomba shilingi mia tano.
Nikaandaa hiyo pesa ili tusizungumze sana.
Sikuwa napendelea sana kusikiliza maelezo yao kwa
sababu huwa wanadanganya wana njaa kisha ukiwape
pesa wanaenda kujidunga madawa ya kulevya.
“Samahani kaka…” nikaisikia sauti ya kike.
Nikageuka upesi kumkabili anayeniita, sikuitarajia
kabisa sauti ya kike muda ule. Sikuwa na mazoea na
watoto wa kike kabisa. Mazoea ya kikazi yalitosha
kabisa!
“Nikusaidie nini?” nilimuuliza bila kuijibu salamu yake.
“Naitwa Nyambura…. Naitwa Nyambura Kone…”
alijitambulisha jina lake.
“Samahani sidhani kama nakufahamu..” nilimjibu huku
nikijiandaa kuingia garini ili niondoke.
Akajieleza kuwa siku hiyo alishiriki usahili katika
kampuni ninayofanyia kazi.
Aliposema vile jina likanikaa sawa kichwani.
Anataka kutoa rushwa!! Nilijiwazia huku nikimsikiliza
aendelee kuzungumza na hapo nikamwomba ajieleze
kwa haraka kidogo, kichwani tayari nikiwa nimepanga
shambulizi kubwa na kumpa ili nimuaibishe ikiwa
atanishawishi kunipa rushwa ya aina yoyote, tena
bora angezungumzia pesa ila akithubutu kunieleza
rushwa ya ngono hata vibao nitamchapa hadharani.
Akajikohoza kisha akazungumza.
“Naitwa Nyambura..” nikamzuia kwa mkono na kumsihi
aendelee kwani jina lake tayari alilitaja awali. Na
huku niliona ni kupoteza muda anakoelekea.
Yule binti aliyejitambulisha kwa jina la Nyambura Kone
akajieleza.
“Mimi ni mtoto wa tatu katika familia yangu…
nimetoka Musoma vijijini kuja jijini Dar es salaam kwa
ajili ya usahili huu, usahili ambao naamini kuwa kwa
leo hakika sijafanya vizuri, lakini hiyo sio tafsiri ya
jinsi nilivyo, ninauguliwa mama yangu na sijui hata
kama nitamkuta akiwa hai, sijala tangu nilipokula
jana mchana, zaidi ya yale maji mliyotupatia sijala
chochote….. nimekuja kwa miguu katika usahili na
nitarejea kwa miguu kama unavyoniona…. Nakusihi
sana na sijui kwanini nimekusudia kuonana na wewe
lakini nakuomba utakapofanya maamuzi basi nipe
nafasi ya upendeleo. Sipo kama nilivyojaribu kujieleza
katika usahili…. Nina matatizo makubwa sana
yananikabili… ni matatizo yangu na si ya kampuni
yenu lakini nakuomba kwa maelezo yangu haya mafupi
unisaidie uwezavyo. Mama yangu anakufa, lakini
wadogo zangu wanahitaji kula, achana na kusoma
maana imeshindikana tayari… mimi ni kila kitu kwao.”
Aliweka kituo yule binti. Akabaki kunitazama
Maneno yake hayakunishawishi sana, kwa sababu
ninaamini katika ushawishi wa katikati ya chumba cha
usahili na si vinginevyo.
Nikaitoa pochi yangu na kutoa noti tatu za shilingi
elfu tano nikampatia kama nauli na nikamweleza kuwa
nimesikia ombi lake.
Nilimweleza ilimradi tu kuyamaliza yale mazungumzo,
aondoke na mimi niondoke.
“Namba ya simu si yangu ni ya huyo aliyenipokea, ikiwa
nitapata nafasi ya kupigiwa simu utamwambia
anifikishie ujumbe.”
Akamaliza kunisihi huku akishindwa walau kutoa
shukrani kwa kiasi cha pesa nilichompatia.
Hakika jambo lile liliniudhi sana, nikahisi huyu ni
changudoa aliyebobea na kwangu mimi alitaka pesa
nyingi ili niununue mwili wake, sasa sijaununua na
nimempatia kiasi kidogo cha pesa.
Pesa zangu ziliniuma sana!
Niliondoka pale lakini sikwenda nyumbani moja kwa
moja, sikuwa nimeoa niliishi peke yangu. Hivyo
ilinilazimu kupita hotelini kupata chakula.
Kitendo cha kuondoka eneo lile nikamsahau na
kumpuuzia yule dada aliyejitambulisha kwangu kwa
jina la Nyambura!
Nilipomaliza kupata chakula, wakati nalipia bili ndo
nikamkumbuka tena Nyambura na kujisemea kuwa laiti
kama nisingempatia ile pesa basi ndo ningeitumia
kulipa ile bili ya chakula.
Niliondoka pale, sasa nilikuwa naelekea nyumbani.
Tofauti na siku zote, nilishangazwa na ile foleni
katika barabara ya Morogoro kutokea Kariakoo
nilipopitia, nilitazama saa yangu na ilikuwa saa nne
usiku. Foleni ilikuwa kubwa kiasi kwamba gari zilikuwa
hazitembei kabisa.
Taratibu taratibu hadi gari ikafikia kile chanzo cha
foleni, kuna ajali ilikuwa imetokea.
Nilipotambua kuwa ni ajali nikapandisha vioo vya gari
langu, kwani mazingira kama hayo kwa jiji la Dar es
salaam huwa vibaka nao wanaingia kazini.
Lakini nilibaki kutazama nione hiyo ajali kupitia kioo
kwenye kioo.
Hapo sasa gari zilikuwa hazitembei kabisa, nikashusha
vioo na kujaribu kuwauliza madereva waliokuwa
wameshuka.
Wakanieleza kuwa njia imefungwa kwa mbele, raia
wamegomea gari zisiondoke kwa sababu katika hii
foleni ipo gari iliyogonga!
Niliishiawa nguvu nikaamua kushuka na mimi garini.
Nilidadisi na kuelekezwa majeruhi alipokuwa.
Nilifika na kujikuta natazamana na mwanamke
aliyejivika mavazi mafupi sana yaliyouacha mwili wake
wazi, vijana wa pembeni wakawa wanamteta
wakisema kuwa ni changudoa alikuwa kazini. Mwil
wake ulikuwa umetokwa na fahamu na hakuonekana
kujeruhiwa sana…..
Maneno yale yakapenya na kunifikia, nami nikakiri
kuwa huenda kweli ni changudoa.
“Unasema changudoa… unamaanisha changudoa ana
haki ya kugongwa na gari akiwa upande wake sahihi….
Sharia ya wapi uliyoisoma wewe inayoruhusu mtu
kugongwa na gari kwa sababu tu ya shughuli zake….
Sikiliza kaka usipokuwa na uhakika na kitu ni heri
ukakaa kimya! Angekuwa dada yako ungesema sawa
afe kwa sababu ni changudoa!!!” ilisikika sauti kali ya
kike ikijibu mapigo kwa jazba.
Nikaguswa na maneno yake, kwa sababu nami na elimu
yangu nilikuwa nimekiri kuuwa ni sawa tu agongwe
kwa sababu ni changudoa.
Nikageuka kutazama ni nani anayetokwa na maneno
yale makali.
Nyambura!! Mungu wangu, nilishtuka sana.
Sijui ni kwanini nilishtuka vile, lakini kuna kitu kama
hofu kiliniingia.
Nikachelewa kubandua macho yangu kwake, mwishowe
nikajikuta natazamana naye.
NAKUSIHI!!
Usimuhukumu mtu yeyote kwa sababu ya muonekano
wake, kwa sababu ya kipato chake, kwa sababu ya
kabila ama imani yake kidini.