winston20
JF-Expert Member
- Jun 21, 2020
- 1,116
- 2,319
RIWAYA; DOA
-----1-----
Ulikuwa ni muda sahihi kwa kila mmoja
kurejea nyumbani, muda ambao jua lilikuwa
limeanza kuiacha Mashariki yake na kwenda
kwa mchepuko wake bi. Magharibi. Harakati
za hapa na pale zilianza kufungwa, watu
walianza kujipa uchovu ili mradi tu, warejee
majumbani mwao kupambana na masimango
ya nyumba zao. Wale wenye gubu, ilikuwa ni
wakati wa majuto kwa panya na mbu ambao
huishia kuona na kusikia vibweka usiku kucha,
kiasi cha kuwanyima uhuru wa kubarizi
kwenye vyandarua na kuta za baridi.
Muda huu ni muda ambao huko mwituni,
wanyama wakali nao walikuwa wanafunga
hesabu za mawindo, huku wanyonge wa pori
wakipumua na kulishukuru jua kuzamia kwa
mchepuko wake, huku wakilaani ukali wa mke
halali mashariki; licha ya kuwapa kula,mwanga
na virutubisho, ila aliwachosha kwa kuwapa
adhabu ya hekaheka za kunusuru uhai wao.
Lakini licha ya kushukuru huko, wapo
wanyama ambao muda huo kwao, ndio muda
sahihi wa kuingia mawindoni, kuvizia na
kujipatia shibe.
Hali hii ilikuwa ni furaha kwa bwana jua,
ambae alifurahi kuona kwake na, mchepuko
wake kunafaidisha viumbe wa Mungu kwa
namna tofauti, hivyo kufanya iwe ni ratiba
yake ya kila siku na wakati wote.
Wakati jua anazidi kujichimbia nyumba
ndogo, Duniani kulikuwa na mambo mengi
yanatokea, usiku huu wa rasharasha, usiku
ambao haujaenda eda, kulikuwa na
mwanamichezo mmoja, akijaribu kumalizia
muda wake wa mazoezi ndani kwake.
Hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo,
alipiga balizi, kisha akapiga miinuko kadhaa,
alojinyoosha na kujipinda kwa utalaamu, huku
akiacha viungo vyake vikubali kwa kutoa sauti
ya mvunjiko.
Mwanamichezo huyu, alikuwa ni kocha wa
timu ya vijana ya Azan, timu ambayo ilikuwa
inafanya vyema chini ya mkufunzi huyo raia
wa Burundi. Makazi yake yalikuwa Sinza.
Alikuwa akiishi kwenye nyumba ya waajiri
wake ambao walikuwa ni kampuni ya Azan.
Ilikuwa nyumba nzuri yenye hadhi yake,
nyumba iliozungushiwa ukuta mrefu na juu
yake kukapita nyaya za umeme.
Kocha huyu licha ya kuishi nyumba nzuri na
kubwa, lakini hakuwahi kuwa na mke wala
mtoto na, hakuna aliewahi kujua kuhusu
familia yake.
Aliishi peke yake.
Aliendelea na mazoezi yake, lakini kwenye
ukuta wake wenye nyaya za umeme, kulikuwa
na kiumbe mwenye moyo wa nyama na miguu
miwili yenye vidole vitano. Mtu yule alikuwa
anamalizia kuhifadhi mkasi mdogo aliotumia
kukata nyaya zile na sasa alikuwa amesimama
wima akitizama upande wa mlango wa
nyumba ile.
Mtu yule alikuwa amevaa mavazi meusi,
kuanzia juu hadi chini kwenye raba zake.
Alipokwisha kuhakikisha hakuna anaemuona
pale ukutani, aliruka sarakasi moja kavu na
kutua chini bila kutoa ukelele, kisha alipiga
hatua fupi fupi kama vile alitarajia kuona
jambo uani pale. Mtu yule hakunyoosha
upande wa mlango uliokuwa wazi, bali alipita
upande wa nyuma wa nyumba ile, kisha
alitumia mlango wa jikoni kuingia ndani ya
nyumba ile.
Muda wote huo, kocha hakujua yanayojiri,
wala kuhisi kuna mtu wa ajabu atakuwa
kamtembelea ndani kwake. Aliendelea kupiga
zoezi jepesi, aliporidhika alielekea chumbani
kwake na alipotoka, alikuwa amevaa taulo tu
akielekea bafuni.
Wakati yeye akielekea bafuni,mgeni wake
yeye alielekea sebuleni,ambapo alichukua
simu iliokuwa mezani na kuipachika kwenye
chaji na kuwasha,kisha alikaa nyuma ya jokofu
kubwa na kutulia kimya.
Kwa nini alifanya vile, hakuna aliejua.
Kocha wa timu ya Azan alipotoka kuoga,
alipitiliza chumbani kwake, huko hakukaa sana
alirejea sebuleni, ambapo alianza kutafuta
kitu, mara akasita na kushangaa.
Hakuwa ameweka simu yake kwenye chaji,
alishangaa imejiweka vipi pale na yeye anajua
aliiacha mezani.
Ajabu hii!.
Aliifuata simu ile, nayo ikaanza kuita. Kocha
aliruka nyuma na kutoa macho kama teja
aliefumaniwa.
Aliiogopa simu yake mwenyewe.
Simu ile iliita na kukata.
Kocha bado alikuwa anajaribu kuweka
kumbukumbu zake sawa, hakuwa yeye
alieweka pale ile simu. Taratibu alianza
kuisogelea tena, mara ikaita tena.
Wakati huu aliamua kuipokea, ilikuwa simu ya
mmoja wa waajiri wake.
Kocha alikuwa katikati ya maongezi, hata
wakati mgeni wake alipotoka mafichoni, yeye
hakuwa na habari kabisa, aliendelea kupanga
mikakati ya timu yake kusafiri mkoani kwa ajili
ya mchezo wa kujipima nguvu na timu moja
maarufu.
Kocha alistuka akishikwa nyuma ya shingo na
mkono ambao ulikuwa umevaa glavu.
Alipojaribu kujitikisa, alipigwa teke la mgongo
na kumfanya abinukie mbele, na hilo likawa
kosa, mana mgeni alimbinua shingo na kukaa
kama mtoto analazimishiwa uji wa chumvi.
Kila alipojaribu kujitikisa, hakupata sehemu ya
kushika ili ajinasue na kabali ile matata.
Kocha alianza kuvuta pumzi kwa nguvu, hilo
ndilo lilitegemewa na mgeni, kwani alizidi
kumbinua kocha kwa kumwekea goti katikati
ya uti wa mgongo.
Kocha alishindwa kuhimili kabali ile ya aina
yake, aliaza kuishiwa pumzi huku macho yake
yakianza kuona kiza kizito, huku masikio yake
yakianza kusikia kelele za kuzomea za
mashabiki wa timu alizozifunga.
Dakika mbili badae, mgeni alikuwa anamlaza
chini taratibu, kisha alichukua simu na
kuirejesha tena kwenye chaji, kisha alimvuta
kocha hadi karibu na simu, kisha alimuinua na
kumshikisha simu ile na kuipachika sikioni.
Alipohakikisha maiti ya kocha imeshika vyema
simu ile, aliingia mfukoni mwake na kutoa kitu
kidogo mithili ya punje ya mtama na
kuipachika kwenye spika ya simu. Alipomaliza
alisogea pembeni kidogo na kubonyeza saa
yake, punde ukatokea mlipuko wa kiasi
kidogo, lakini ulikuwa ni mlipuko uliobomoa
kichwa cha kocha kuanzia upande wa kushoto
kwenda juu na kufanya awe kama papai
lilokatwa kipande.
Damu ilianza kutoka, na kusambaa hovyo pale
ndani. Mgeni muuaji alianza kuondoka ndani
ya nyumba ile, huku akiwa ameua bila kuacha
alama ya ushahidi na hiyo ilikuwa ni sheria
namba moja. Na kwa kifo cha kocha, maofisa
wangeishia kujua alilipukiwa na simu wakati
anaongea na simu ikiwa chaji. Muaji akiwa
mbali na hisia feki za maaskari.
Wakati muuaji anaondoka ndani ya nyumba
ya kocha, kulikuwa na mtu mwingine anaingia
pale, akiwa amevaa sawa na yule alietoka,
mtu huyu yeye alikuwa ni mfupi tofauti na
yule wa mwanzo. Aliingia ndani ya nyumba ile
kupitia dirishani,alipofika aliishia kukutana na
maiti ya kocha ikiwa na simu iliolipuka
pembeni yake.
Mtu yule alitoa simu janja yake na kupiga
picha moja, kisha alitoa kibahasha kidogo sana
na kukirusha chini ya uvungu.
Kibahasha kile kilikuwa kimeandikwa herufi
moja iliochanganywa na namba. Ilisomeka hivi
“F3”,Kisha aliondoka mle ndani kwa kupita
njia tofauti na alioingilia.
Nyumba ya kocha ilikuwa imetembelewa na
watu wawili, huku mmoja akiua na mwingine
akiacha ujumbe wenye maana aliojua yeye, na
dhahiri alieua hakujua kama ameonwa na mtu
alieacha ujumbe.
Lakini kwa nini huyu aue na huyu aache
ujumbe, kwanini?
Hakuna aliejua sababu zaidi ya wao wahusika
wenyewe.
Mtu wa pili kuingia nyumbani kwa kocha,
ambae ndie mtu wa mwisho kutoka nyumbani
kwa kocha, yeye aliamua kuendelea na ziara
yake jirani na maeneo yale. Kulikuwa na
nyumba moja ambayo alihitaji kuitembelea
usiku ule. Mtu huyu ni kama hakujali kabisa
kile alichokiona nyumbani kwa kocha.
Mtu huyu alipofika usawa wa nyumba
alioikusudia, aligeuka kushoto na kulia
kutazama kama kuna mtu yeyote aliekuwa
anamfuatilia. Alipohakikisha hakuna mtu,
alijongea taratibu na kuufikia ukuta,
aliutazama kwa sekunde kadhaa, kisha akatoa
glavu na kuzivaa. Alipomaliza alizijaribu kwa
kuushika ukuta, alipohakikisha zinafaa kwa
kazi alioikusudia, alianza kuukwea ukuta ule
huku akisaidiwa glavu zile maalumu kwa
kupandia kuta na miamba mirefu.
Tofauti ya ukuta huu na ule wa kocha, ukuta
huu ulikuwa unavipande vingi vya chupa kwa
juu, hivyo alipofika juu, alitulia kidogo na
kujivuta kwa kasi hadi alipotua chini na
kuachia ukelele mdogo usiostua. Alifanya vile
kukwepa kudhurika na chupa zile.
Alijinyanyua na kutembea bila wasiwasi,
macho yake yalikuwa sambamba na dirisha
moja alilokuwa amelikusudia kabla na baada
ya kuingia pale. Ni dhahiri aliijua nyumba ile.
Hakuhangaika na kukwepa taa zilizokuwa
zinawaka sebuleni, wala hakutaka kuhadaika
na kelele za watoto waliokuwa wakitizama
filamu za Tom na Jerry.
Yeye alikusudia kuingia bila kuwastua wale
watoto ama mtu yeyote aliekuwa pale
sebuleni.
Alipolifikia dirisha lile, alijaribu kusukuma kioo
lakini kilikuwa kimefungwa kwa ndani, haraka
alingiza mkono mfukoni mwake na kutoa
chuma kidogo chenye muundo wa bikari, kisha
alikapachika kwenye kioo na kuzungusha kwa
duara, aliporidhika alikirudisha mfukoni
mwake na kukivuta upande wake kipande cha
kioo alichokata. Alipokwishakitoa, aliingiza
mkono na kufyatua kabali ya kioo na
kukisukuma pembeni, kisha alipita na kuingia
ndani, ambapo alijikuta akitokea jikoni na ndio
ilikuwa kusudio lake.
Kutokea pale jikoni, kushoto kwake kulikuwa
na korido ambapo ukiifuata utatokea kwenye
chumba kikubwa cha mmiliki wa nyumba ile.
Mtu yule alitembea kwa hatua za kunyata na
kisha aliishia mlangoni mwa chumba
alichokikusudia.
Alitulia kidogo na kusikiliza, aligundua kuna
mtu ndani ya chumba kile, ni kama ambavyo
alikuwa anajua kuhusu ratiba ya pale ndani ya
mtu aliemfuata.
Aligonga kidogo na kutulia. Kukawa kimya.
Aligonga tena na mara hii kwa nguvu kidogo.
Mara ikasikika sauti ya mwanamke pale ndani,
ikimruhusu aingie.
Ni dhahiri mwenyeji wa chumba kile alijua ni
watoto au mfanyakazi ndie anaehitaji kuingia.
Mgongaji alitabasamu kiupande, kisha
aliusukuma mlango taratibu na kuingia ndani,
ambapo alikutana na mwanamke mwenye
umri wa kukadiria miaka sitini kasoro moja
hivi. Mwanamke yule alionekana mrembo
licha ya ngozi yake kuanza kupukutisha nyama
za urijali.
Mwanamama yule alitoa macho ya kuhoji,
huku akiwa ameshika taulo lake akishindwa
kumalizia kuusitiri utu wake.
“Wewe ni nani na umeingiaje hapa!” Mama
alihoji kwa kigugumizi cha woga.
Badala yake hakupata jibu, bali mtu yule
alikisogelea kitenza mbali na kuwasha radio na
kuweka sauti ya juu kidogo.
Mama yule dhahiri alijua mambo si mambo,
haraka aliachia taulo lake hadi chini na kubaki
mtupu, lakini hakujali,mikono yake yenye kasi
ilikuwa inaiwahi bastola yake kitandani, lakini
kasi ya mgeni ilikuwa kubwa na kumsukuma
kidogo kumpotezea mwelekeo,mama
hakutaka kukubali kirahisi, alitaka
kujipambania, lakini aliwahiwa kwa kofi zito
usoni,kofi lilomtoa kwenye ufahamu wake
kwa sekunde kadhaa na hata aliporudi kwenye
utimamu alikutana na kitu ambacho
hakukitarajia. Mgeni wake alikuwa ameshika
chupa ya marashi anayojipulizia mwili mwake.
Mtu yule alikuwa anayapuliza marashi yale
usoni pake na kwa kuwa halikuwa tukio la
kutegemea, alijikuta akivuta pumzi nyingi ili
kukwepa kile alichohisi mgeni wake
alikikusudia, lakini alikuwa amechelewa sana,
kwani alipovuta pumzi, alivuta harufu kali ya
marashi. Alianza kukohoa hovyo huku
akijaribu kuzuia asivute harufu kali ya marashi,
lakini haikusaidia, alikuwa amevuta harufu
nyingi kiasi koo lilikauka na hata majimaji
yanayokaa puani kulainisha
vinyweleo,yalikuwa yamekimbia kwa adha ile.
Mgeni alikuwa na hakika na kazi yake, hivyo
hakutaka kuendelea kuhangaika na
mwanamke yule aliekuwa mtupu na utu uzima
wake mbele ya kijana yule mdogo aliekuwa
amefunika uso wake kwa kitambaa maalumu.
Mwanamke yule alizidi kupambania uhai
wake, huku dhahiri akionekana kuhitaji
kunywa maji ili kupooza koo lililokuwa
limekauka na pua zikiwa kavu na zilizoenea
harufu ya manukato ya bei kubwa.
Mtu yule alitoa kibahasha kidogo kilichokuwa
na sawa na bahasha aliokuwa ameiacha
nyumbani kwa kocha. Bahasha hii pia ilikuwa
na herufi moja na namba “F3”. Bahasha ile
aliitupa uvunguni mwa kitanda na alianza
kuondoka, lakini ni kama alikumbuka kitu,
haraka alirudi na kuinama uvunguni, ambapo
aliitoa ile bahasha, kisha aliandika namba
mbili tu na kuitupa tena kule uvunguni.
Alipomaliza aligeuka upande ule ambao
alikuwa mwanamke akijitahidi kukohoa ili
aweke sawa koo lake.
Jamaa aliona picha kubwa ikiwa ukutani, picha
ilikuwa ya mwanamama yule akiwa kwenye
mavazi ya kipolisi yaliojaa nyota begani.
Ni kama hakuijali picha ile, badala yake
aliondoka na kupitia njia ile ile aliokuwa
amekujia.
Lakini mtu yule alikuwa anajua kabisa, si rahisi
kujua yule mwanamke ambae alikuwa ni
mstaafu wa jeshi la polisi, atakuwa ameuawa.
Kitu kimoja alichohakikisha ni kuwa mauaji
ya kocha alioyashuhudia, yanaendana sawa na
mauaji alioyafanya yeye kwa msataafu yule na
afisa habari wa timu ya Azan.
Muuaji alitokomea huku nyuma akiacha msiba
mzito na wenye utata mwingi, lakini ulikuja
kuumiza vichwa vya watu kwa namna tofauti
tofauti. Kuna wale ambao hawakukitegemea,
lakini wapo waliokitegemea. Lakini ilikuwa ni
kizungumkuti zaidi kwa idara ya usalama,
ambayo ilishindwa kujua kama yale mauaji
yalikuwa yanahusiana ama ni tofauti, lakini pia
haikuonekana kuwa ni mauaji, ni kama kocha
alilipukiwa na simu huku mstaafu akivuta
hewa nyingi ya manukato kiasi alishindwa
kupumua vyema.