RITA Dodoma kuna mambo hayako vizuri

RITA Dodoma kuna mambo hayako vizuri

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
716
Reaction score
1,144
Leo nomefika ofisi za RITA DODOMA kuanzia saa tatu na robo mpaka naondoka saa Saba mchana sikupata huduma. Nimefika pale kwenye ofisi zao zilizopo Makole kwenye jengo la PSSSF gorofa ya tano nilichoshuhudia ni maajabu.

Kwanza hakuna dawati la maulizo wala huduma kwa wateja.

Kulikuwa na nyomi ya kufa mtu na mlango wa kutolea huduma uliokuwa unafanya kazi ni mmoja tu Kati ya milango mingi.

Nilikuwa nahitaji kujua hatua za kichukua cheti cha mtoto baada ya tangazo lakini hata maelezo sikupata.
Baada ya muda kidogo akaja kijana mmoja nafikiri alikuwa mmoja wa staff pale ofisini.

Nikamuuliza utaratibu upo je aksema kama unataka huduma kale pale, nikamwambia hata huduma ya kuuchukua fomu nayo nikae,majibu yake sasa kidogo nizimie, akasema kachukue kwingine unakojua wewe.
Majibu hayo yalinifanya nimuulize kama kweli yeye ni mtumishi pale na mfanyakazi wa Umma maana CODE and CONDUCT hakuonyesha kabisa kama ni mtumishi wa Umma.

Ubishi ikaanza hapo kwa shingo upande akapomba radhi yakaisha.

Nikakumbuka ni juzi tu Rais Samia katumbua watu pale tena mabosi wa Ile taasisi kumbe uozo upo kuanzia chini kabisa.

Nidhamu naona kama imeshuka sana kwenye ofisi za umma kwa wateja wao, huduma tunazostahili kabisa mpaka ubembeleze kama unaomba kazi. Kwa Ile nyomi na mhudumu mmoja kutoa service itaisha baada ya muda mrefu sana.

Nimeamua kuacha kufuatilia hicho cheti mpaka siku nitakopokuwa na mood ya kufanya hivyo. Watumishi kwenye ofisi za umma wanatuona kama wateja wao hatuna lolote kwao sijui hii kasumba itaisha lini.
 
Back
Top Bottom