Risasi zarindima muda huu Kitunda, mmoja atiwa nguvuni

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
Nikiwa katika pitapita nimesimama hapa Kitunda panaitwa Magole kwa mpemba zinakuja gari ndogo mbili zinakimbizana. Ile gari ya nyuma ambayo naamini ni walinda usalama anatokea mmoja na kupiga risasi hewani lile gari dogo la mbele linasimama na wanatoka wanaume wa tatu mbio mmoja wao kavaa kanzu (sina lengo la kuchfu imani). Ile kanzu ilimfanya asiwe na mbio hivyo kupigwa ngwara na kuanguka kisha kutiwa nguvuni wale wawili walikimbia na polisi waliwakimbiza huku gri lililotumika likitelekezwa.

Binafsi huwa sipendi sana ushabiki mandazi hivyo niliondoka eneo husika. Shikamoo IGP mpya
 
Nikiwa katika pitapita nimesimama hapa kitunda panaitwa magole kwa mpemba zinakuja gari ndogo mbili zinakimbizana ile gari ya nyuma ambayo naamini ni walinda usalama anatokea mmoja na kupiga risasi hewani lile gari dogo la mbele linasimama na wanatoka wanaume wa tatu mbio mmoja wao kavaa kanzu (sina lengo la kuchfu imani) ilekanzu ilimfanya asiwe na mbio hivyo kupigwa ngwara na kuanguka kisha kutiwa nguvuni wale wawili walikimbia na polisi waliwakimbiza huku gri lililotumika likiteketezwa binafsi huwa sipendi sana ushabiki mandazi hivyo niliondoka eneo husika....shikamoo IGP mpya
Hakuna uhusiano hapo
 
Wiki 3 zilizopita kuna vijana walinyanganywa bodaboda zao na kuuwawa, humo kitunda kwa mbele huko, pia kuna jamaa yangu alikodi bodaboda pale banana Aviation house, kufika mbele ikajitokeza bodaboda nyingine na kumpora jamaa wakishirikiana na ile bodaboda aliyokodi..
 
Ni bora tuone chanzo halisi cha kurupushani hizo ni nini badala ya kutoa lawama tu za upande fulani..
 
Baadaye utawaskia...
''Watu waliokuwa wamevaa KANZU na wakiwa wamefuga ndevu wamerushiana risasi na jeshi la polisi na katika majibizano hayo "Gaidi" mmoja amepigwa risasi na akasikika akisema "ALLAHU AKBAR" na amefariki akikimbizwa hospitalini...."
Shubaaamit!


Sasa haya, umeyatoa wapi mbona kwenye huu uzi hayapo!

Acheni , kukuza mambo na hizi dini za kigeni aiseee.

Wakati mwingine kujitoa ufahamu kwa makusudi siyo jambo nzuri.
 
Mletauzi hivi unajua kwamba habari isiyojitosheleza pia ni branch ya umbeya?
Tutaamini vp kuwa wewe c mmbeya wakati habari yako ina vionjo vya umbeya?
 
Back
Top Bottom