Risala ya mwaka (summary of the year)

Risala ya mwaka (summary of the year)

Haber Faraday

Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
97
Reaction score
182
LESSON; RISALA YA MWAKA (SUMMARY OF THE YEAR).

Hatimae leo mwalimu ameamua kurudi tena darasani baada ya likizo ndefu, pole kwako wewe mwanadarasa ambae hali yako kiafya si nzuri lakini pia hongera kwako wewe ambae uko buheri wa afya, mwalimu ataenda kutufundisha somo mujarabu kabisa, somo mahususi kwa muda huu ulionao sasa na muhimu kabisa kwako wewe kuweza kujifunza, pamoja na somo hili kuenda kutufunza bali pia linaenda kutukumbusha vitu ambavyo hatupaswi kuvisahau. Twende tukaanze kuliangalia somo hili.

Kabla ya kuanza kulisoma somo hili, ni vyema ukatenga muda wako wa kutosha na itafaa zaidi kama utapata sehemu tulivu kabisa ya peke yako, nafikiri yule mfwatiliaji wa masomo ya mwalimu anakumbuka somo lililoongelea umuhimu/faida na ulazima wa kutenga muda wa kuwa peke yako katika eneo tulivu linalokupa uwanja mpana wa wewe peke yako, basi fanya hivyo kwa somo hili pia, kwa kufanya hivyo utakuwa umejiongezea kitu kikubwa katika ufahamu wako.

Note; {nitapenda zaidi kutumia neno summary badala ya neno Risala}, sote tunafahamu kuwa mwaka una siku zisizopungua 365, ni siku nyingi sana na ni muda mwingi sana endapo utaweza kuzibadilisha hizo siku na kuwa masaa, na kama hutojali nenda mbali zaidi ubadili ziwe dakika, lakini pia si vibaya kumalizia kuwa sekunde, hapa kwenye sekunde kumbuka kitu kimoja ambacho ni kwamba idadi ya sekunde utakazozipata hapo basi kumbuka kwamba moyo wako umeweza kudunda kwa idadi ya sekunde hizo pasi na kupumzika na hata hapa unapoendelea kusoma makala hii moyo bado uko kazini, sote tusimame tunyamaze kwa dakika moja tumshukuru huyu aliyeuumba mwili huu wa nyama wenye mfumo tata (a complex system), Na kumshukuru kwa dhati na moyo uliopondeka na unyenyekevu kwa kukufanya uendelee kuishuhudia hiyo complex system.

Baada ya kukumbushana hapo kuhusu muda wa uwepo wetu chini ya jua na nyota zingine ndogo twende tusonge mbele zaidi, kwa kuwa umeweza kufika siku hii ya leo basi ni dhahiri kwamba ulikuwa unafanya vitu fulani ndani ya huu mwaka ambavyo vimekuwezesha kuendelea kuishi, vitu hivyo vimekufanya ule, unywe, uvae na mambo kadha wa kadha.

Tusimame tena dakika mbili tuweze kuvikumbuka vitu vyote tulivyoweza kuvifanya ndani ya huu mwaka, (mwalimu akazie hapa) hapa inajumuisha vitu vyote haijalishi vilikusababisha hasara au mafanikio, hahaha, mwalimu anacheka kuona mwanadarasa mwingine hana haja ya kukumbuka kwa sababu toka mwaka uanze anafanya kitu cha aina moja;

Nini namaanisha ni hivi kama huyo mtu ni mwalimu kama Faraday hapa basi yeye kacheza na chaki tu mwaka mzima mpaka sasa unaisha, kama ni muuza nyanya basi kauza kila aina ya nyanya mpaka siku 365 zinakatika, ngoja Bruce Lee atuchekeshe kidogo hapa alipoongelea juu ya hofu yake alisema “I fear not the man who has practiced 10000 times and kicks once, but I fear the man who practiced one kick 10000 times”. Naam! Naamini hapo pameeleweka nini namaanisha, baada ya kuyakumbuka hayo tuliyoweza kuyafanya ngoja tujaribu kuyahusianisha (to link), je na nini?;

Hiki hapa, ni kuhusianisha na yale tuliyokuwa tumeyapanga kuyafanya ndani ya mwaka huu kabla haujaanza, Tusimame tena dakika moja tukumbuke yale tuliyokuwa tumeyapanga kuyafanya ndani ya huu mwaka hapohapo bila kuweka kituo jaribu kuyahusianisha na yale uliyoyafanya kama je ni yale uliyoyapanga? Au laah umefanya mengine ambayo hukuyapanga, ama umefanya uliyoyapanga lakini je umeyatimiza kwa kiwango gani? Na kama je yamekufikisha ulipokuwa unataka kufika au yamekufikisha nusu ya sehemu uliyokuwa umepanga kufika au vile vile yameenda kinyume na pale ulipopanga kufika,

Hii dakika moja ya kuyakumbuka yote hayo na kuyahusianisha ngoja mwalimu acheke kidogo hahaha! Kwasababu mwanadarasa mwingine hakupanga kabisa kabla ya mwaka kuanza yote aliyoyafanya yalikuja kama ajali.

Baada ya hatua hiyo si vibaya tukazidi kusonga mbele na somo hili, mwanadarasa mwingine ameenda mbali zaidi katika kukumbuka kwake kisha anatikisa kichwa ishara ya masikitiko, masikitiko haya yanatokana na kukumbuka nini, mwalimu Faraday anakutajia sababu kuu ambayo ni, mwanadarasa huyu hajafikia pale alipokuwa amepakusudia lakini hiki sicho kinachomfanya asikitike bali ni vitu/mambo kadhaa ambavyo vimekuwa visababishi vya kufanya asifikie alipopakusudia, vitu hivyo si vingine bali ni hivi mwalimu anaenda kukutajia tuanze na cha kwanza, Binadamu, pazuri hapa na wanadarasa walio wengi wanaingia hapa ngoja mwalimu akufafanulie uelewe.

Katika kuishi kwetu hapa duniani, tunaishi katika jamii na jamii ni watu hivyo hakuna anaeweza kuishi nje na watu, na kwa kuwa mtu hawezi kuishi pasi na kufanya jambo fulani basi vivyo hivyo hakuna jambo ambalo linaweza kufanyika pasipo uhusika wa watu, sasa huu uhusika wa watu ndio huu unaomfanya huyu mwanadarasa atikise kichwa akiomaanisha masikitiko kwasababu anakumbuka kwamba asingekuwa fulani basi huu mwaka ningekuwa nimefikia sehemu fulani, ama wasingekuwa watu fulani ningekuwa nimefikia pale nilipokuwa nimepakusudia;

hahaha! Kwanini mwalimu anacheka hapa ni kwasababu anajua wanadarasa walio wengi wakiwa wanapanga mambo yao huwa wanaiacha nguzo moja kubwa ambayo ni madhara ya jamii katika kila unalopanga kulifanya wanaothubutu kuwaza hili wanajisahau kwa kuiweka jamii mbali huku wakisahau jamii huanza na Familia, Rafiki au mtu wako wa karibu anaweza kuwa mke au mpenzi wako hehehe kazi kwelikweli.

Tuje cha pili mabadiliko ya mifumo mbali mbali katika utawala ambao kwa huo tuko chini yake na tunautii, hapa wanadarasa vijana wengi wamejawa na manung’uniko pakoje hapa, ngoja mwalimu aende kwenye mfano moja kwa moja ili mwanadarasa asipate tabu kupaelewa hapa,

kwa mfano kuna kijana anaitwa Kizito na mwingine anaitwa Jamila, hawa ni wahitimu katika wa vyuo vikuu, huyu kizito ni mtoto wa mwisho wa mzee mwambatata ambae ni mkulima katika kijiji cha mporoto mkoani mbeya ambae kula kwake kumeshikiliwa na uwepo wa mvua lakini huku kibanda chake kikiwa hakiihitaji mvua, mzee huyu ana watoto watano na wanne waliomtangulia kizito wakiwa wamekumbwa na wimbi la utumiaji wa pombe za kienyeji, macho yote ya mzee yamebaki kwa kizito;

Huyu kizito alisoma shule ya msingi pale kijijini mporoto huku akikosa hata kitu cha kusitiri miguu yake, lakini alifaulu na kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya kata pale mporoto, kutokana na kukosekana kwa walimu wa masomo ya sayansi mtihani wake wa mwisho alikosa cha kuandika katika mitihani ya masomo ya sayansi lakini uwepo wa walimu wawili wa masomo ya sanaa, kizito aliweza kufaulu masomo haya ya sanaa na kujiunga kidato cha tano aliendelea na kufanya vizuri katika mtihani wake wa kidato cha sita akipata daraja la kwanza kabisa, alikuwa na uwanja mpana wa kusomea chochote lakini kutokana na hali ya nyumbani kwao chini ya baba yake mwambatata;

Aliona si vibaya akasomea ualimu aliamini atakapomaliza basi ataweza kuajiriwa ili kile kimshahara kidogo aweze kumnunulia hata shati jipya baba yake Mwambatata huku baadae akijikusanya ajiajiri katika kilimo kutokana na yeye kukijua na pia ardhi ya kijijini kwao ikiwa haikatai zao lolote, huyu kizito amehitimu Elimu ya juu mwaka 2015 lakini mpaka leo yupo mtaani kwasababu mfumo wa utawala umebadilika kidogo na kuamua kutoajiri watu wa aina ya kizito na hatimae Kizito amekuwa mwepesi, manung’uniko yamemjaa moyoni mpaka akilini mwake Cheti chake hakina thamani tena yupo kijijini mporoto analima kilimo cha mkono ambacho kinakosa hata mbolea kwa kuwa mfukoni hana kitu.

Huyu Jamila kidogo mwalimu Faraday anajawa na simanzi kabla ya kuelezea manung’uniko yake juu ya mabadiliko ya mfumo wa utawala anaamua kuyaacha ya Jamila, tuingie kisababishi cha tatu na cha mwisho kama kisababishi cha masikitiko ya mwanadarasa huyu ambacho ni yeye mwenyewe binafsi, hapa huyu mwanadarasa anajilaumu sana kwa baadhi ya yale aliyokwisha kuyafanya, kwa yale ambayo hakuyapanga kuyafanya bali yalikuja tu njiani (accidentally) anajilaumu kuwa kwanini amefanya na yale ambayo alikuwa ameyapanga anajilaumu kwa njia alizozitumia kuyatekeleza huku akijua njia sahihi baada ya matokeo,

hahaha! Mwalimu anacheka kidogo hapa kwamba wengi wao waliyapanga yale watakayoenda kuyafanya juu ya msingi kawaida na hata yale yaliyokuja njiani kama ajali yalitengewa asilimia mbili za kuyatafiti na kujigunza juu ya hayo.

Kuyaelewa hayo zaidi kajikumbushe tena masomo ya mwalimu Faraday somo linaloitwa jinsi ya kuuweka mpaka wako mbali (How to keep far your limits) bila pamoja na somo linaloitwa Akili yako kufanya vitu isivyopaswa kuvifanya, na kutokufanya vitu ipaswavyo kuvifanya.

Pamoja na hayo yote lakini hupaswi kunung’unika kwasababu kuna siku mbili kuu katika maisha yako ambapo ya kwanza ni ya kuzaliwa na ya pili ni pale utakapokuja kujua kuwa kwanini (The two most important days in your life are the day you are born and the day you find out why). Hivyo pengine kuanzia hivi sasa ndio utaenda kuifanyia kazi hiyo siku ya pili;
Kama sababu ni mabadiliko ya kimfumo kutokana na utawala ambao kwa huo tunaouheshimu na kuutii basi pitia somo linaloitwa Ajira utatoka na kitu kipya na kama sababu ya manung’uniko ni binadamu masomo ya mwalimu faraday yanayohusu Jamii yatakufunza hapa, na kama sababu ni wewe mwenyewe basi somo la Mapinduzi ya kimfumo na misingi utaweza kuondoka na kitu.

Baada ya hayo tuvute pumzi kwa dakika mbili kisha tuendelee, hahaha, binadamu tunatofautiana sana mimi mwalimu Faraday pale ninapoanza kusikia vinyimbo redioni vikiimba “Merry’s born child jesus Christ...........” sijui kama ni hivyo inavyoimbwa lakini nyimbo hizi huwa zinanijaza simanzi badala ya kuruka na kutokwa jasho kwa kuserebuka kiroho kinalia kwatu kwanini mimi hali inanitokea hivyo pengine tofauti na wengine;

Kwasababu kwangu mimi inakuwa kama kengele (alarm) inayonikumbusha kuwa zile siku 365 zinaenda kuisha basi akili inanirudisha kipindi nilipovisikia vinyimbo hivi mwaka 2016, 2015, 2014.......

Nafikiri mpaka hapo utakuwa umegundua kitu kwa wale ambao hatukuukimbia umande basi kile tulichokiita sequence and series kwenye hesabu utajua namba inayofuata na utagundua kuwa zinapungua au kuongezeka kwa ngapi, Kumbe lile shimo ambalo juu linawekwa tuta na mwili huu unaoandika haya ukiwa umefukiwa ndani na haujiwezi tena basi linakuwa linanikaribia lakini swali je nimefikaje hapa je?....

Ngoja John anisaidie kufupisha maneno anaposema “A man who views the world the same as fifty as he did as twenty, has wasted thirty years of life”.

Basi kufikia hapo mwalimu akutakie usomaji mwema, bila kusahau sio kila neno lipo kwa ajili ya wote wewe utakaelielewa basi ujumbe ulikuwa umekusudiwa kwako, uwe na jioni njema, kutakuwa na somo la kuuga mwaka na pia kutakuwa na somo la kuupangilia na kuufungulia mwaka ujao. Usikose!!


H.Faraday (0625934471).
 
Chonde chonde wana Jf usiquote huu uz ni mrefu tutatiana njaa tu wengne simu zetu zina ram ya mb 4, we comment tu. Haya ngoja nianze kusoma nilitaka ni mipe tahadhari.
 
Back
Top Bottom