Ripoti ya tume ya Sitta vipi?

Ripoti ya tume ya Sitta vipi?

SERGIO

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
348
Reaction score
145
Samwel Sitta, Waziri wa Uchukuzi, mara baada ya kuteuliwa kwenye wadhifa huo aliutangazia umma kuwa ameunda tume ya kuchunguza utendaji wa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Mhandisi Madeni Mapande, baada ya kumsimamisha kazi kwa tuhuma mbalimbali. Baadaye alitangaza kuwa tume imekamilisha kazi yake, lakini hajawahi kutangaza matokeo/mapendekezo ya tume hiyo. Alichofanya ni kumuondoa Mapande na kumpeleka Utumishi ili apangiwe kazi nyingine. Kwa maoni yangu umma una haki ya kujua tume iligundua nini katika uchunguzi wake. Au shida ya Sitta ilikuwa ni kumng'oa tu Kipande? Kwa nini amekuwa kimya kuhusu kilichogunduliwa na tume kwa manufaa ya TPA?
 
Hivi unamjua vizuri Sitta? Yule ni mzee wa madili. Kwa vyovyote asingeweza kufanya kazi na mtu kama Kipande ambaye inasemekana amezuia madili yote ya wakubwa bandarini. Ndio maana alipopewa tu hiyo wizara, alianza kushughulikia bandari kabla hata hajapewa briefing ya kutosha na bodi kuhusu kinachoendelea. Masuala ya bandari na zaidi ya unavyoyajua.
 
Mleta mada lazima utakuwa mnufaika wa uhalifu na uchafu wa Vipande vya Madeni...
 
Huyo Kipande si alipelekwa TPA na swahiba wa Sitta, Dk Mwakyembe? Tena nakumbuka Mwakyembe alimwagia sifa nyingi sana huyo jamaa ambaye naambiwa ana ubabe fulani. Ikawaje tena?
 
Mleta mada lazima utakuwa mnufaika wa uhalifu na uchafu wa Vipande vya Madeni...

Wallahi simjui Kipande wala mtu yeyote TPA. Najaribu kuwa mdadisi tu kwa vile nimesikia mengi kuhusu hili suala. Mimi ni mlalahoi tu ndugu yangu DuppyConqueror.
 
si amerudishwa utumishi? ili apangiwe kazi nyingine kuna tatizo gani
 
Hivi yule jamaa si alikuwa Wizara ya Ujenzi na pale alikuwa anakaimu tu, kwa nini nhakurudishwa wizarani akapelekwa Utumishi kupangiwa kazi nyingine?
 
Back
Top Bottom