Riport ya utafiti-positive thinkers

Riport ya utafiti-positive thinkers

gwahe

Senior Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
147
Reaction score
84
WANAJUKWAA,
Nnimeamuwa kuweka maneno machache ambayo yalisomwa kwa mwandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ripoti, pia kiambatanisho cha matokeo ya jumla. Kuelezwa kuwa Positive Thinkers imedhaminiwa na Loawasa kwa 100% mimi kama raisi wa PTT, hizo ni changamoto kama changamoto hasi zingine.

Wakati wa utafiti, watafiti walipata changamoto kama hizo na zingine kuhusisha serikali kama ina mikono yake. Lakini atayesoma UTANGULIZI HAPO CHINI NA KUSOMA RIPOTI nzima ambayo inapatika Positive Thinkers | Implementing Success Strategies & Enhancement of Possibility Thinking atakuwa amepata ufahamu maana kamili ya utafiti wetu. HIZI TAARIFA ZOTE ZINAPATIKANA KWENYE WEBSITE.

UTANGULIZI.
Positive Thinkers Tanzania(PTT) inapenda kuchukua nafasi ya pekee kuwashukuru wadau wote wa maendeleo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kitechnologia ambao wamekuja kuhudhuria uzinduzi wa utafiti huu. PTT inatoa shukurani za dhati na chanya kwa wanahabari wote waliojitokeza na kushiriki na kwenye uzindizu wa utafiti wenye malengo chanya kwenye jamii.Utafiti huu umefanywa na taasisi isiyo ya kiserikali inayojukana kwa jina, "Positive Thinkers Tanzania". Kwa niaba ya Positive Thinkers Tanzania. Utafiti huu hauna mlengo wa ki-itikadi ya chama cha siasa ,wala hauna madhumuni ya kufanya kampeni kwa mwanasiasa yeyote yule nchini.

Lengo kuu la ufatifi huu ni "Kutambua vigezo na matarajio ya wananchi katika kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania". Wanafikra Chanya Tanzania, wanayo imani kuwa, matokeo ya utafiti huu ni mwongozo muafaka kwa ajili ya wadau wote nchini katika maswala ya siasa na maendeleo. Utafiti umebaini mambo mengi ya msingi ambayo wanasiasa na wanaharakati wa maendeleo wanahitaji kuyatazama kwa mtazamo mpya na makini.

POSITIVE THINKERS TANZANIA.
Positive Thinkers Tanzania(PTT), ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyosajiriwa nchini Tanzania tarehe 1 Februari 2011. Positive Thinkers Tanzania ilisajiliwa kwa nambari 00004344. Makao makuu ya PTT yako Dar es Salaam, Tanzania.Taasisi imeundwa na watanzania wenye mtazamo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii, Wenye kuamini kuwa mtu akijengewa hali ya kuwa na mtazamo chanya ataweza kufanya mabadiliko kutoka hali duni na kuwa na maisha bora. Pia mtu akiwa na mtazamo chanya anaweza kuwajibika na kuleta mabadiliko yanayohusu hatima yake ya sasa na ya baadaye. PTT inaamini kuwa jamii ya watanzania inaweza kufanya maamuzi chanya juu ya hatima ya mtu binafsi, mtaa, mkoa na hata taifa kwa ujumla.

Dira ya PTT:
Kuwa taasisi inayoongoza kuelimisha, kujenga uwezo na ubunifu kwa jamii ya watanzania, kujenga mtazamo chanya katika harakati za kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya kitanzania.

Dhamira ya PTT.

Positive Thinkers Tanzania inaamini katika kujenga uwezo na fikra chanya kwa wadau na raia, kujenga uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, kutafiti na kutathimini matarajio na mahitaji ya wananchi juu ya mustakabali na hatima zao, pamoja na kushiriki katika kutatua changamoto za maendeleo ya uchumi, jamii na siasa nchini.

MELEZO YA UTAFITI.
Kwanini Utafiti huu umefanyika? Utafiti huu umetokana na hamasa ya wadau wa maendeleo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na teknolojia kutaka kujua hali halisi ya mtazamo, vigezo na matarajio ya wananchi katika kumchagua kiongozi wao. Kutokana na tafiti mbali mbali zilizofanyika nchini Tanzania katika maswala ya ushiriki wa wananchi kufanya maamuzi ya kisiasa; swala la vigezo na matarajio ya wananchi katika kufanya maamuzi ya kumchagua kiongozi limekuwa halipewi nafasi kubwa. Kutokana na changamoto nyingi zinazojitokeza, hasa kipindi hiki ambacho Tanzania inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu kitaifa, shirika lisililo la kiserikali la Positive Thinkers Tanzania (PTT) liliamua kufanya utafiti juu ya vigezo, sifa na matarajio ya wananchi katika kufanya maamuzi ya kumchagua kiongozi.

Wanafikira Chanya Tanzania wamekuwa wajiuliza maswali mengi kuhusiana na hatima ya Tanzania na Watoto wa kesho wa TANZANIA. Wamekuwa wakijiuliza mawaswali mengi?? Je, nchi yetu itakuwa katika mikono ya viongozi waadilifu na wawajibikaji? Je, misingi gani ya uongozi itakayolifikisha taifa la Tanzania katika hatima wanayoitaka wananchi?.

Mawasli haya na mengineyo yamepelekea kuwepo na haja ya kufanya utafiti juu ya vigezo wanavyovitarajia wananchi katika kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania ifikapo Oktoba 2015.

Malengo Mahsusi ya Utafiti.
Malengo mahususi ya utafiti yalikuwa ni kama ifuatavyo:
a) Kutambua vigezo wanavyotumia wananchi kufanya maamuzi na wapiga kura kuchagua kiongozi.
b) Kutathimi matarajio ya wananchi kwa kiongozi watakaye mchagua, kuwa Diwani, Mbunge au Raisi.
c) Kutathimi chama cha siasa chenye mvuto wa kuongoza nchi.
d) Kutathimini kiongozi anayefaa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
e) Kutambua vipaumbele vya wananchi wanavyotarajia raisi mtarajiwa avitimize km kiongozi anayefaa.
f) Kubaini kiwango gani cha elimu ya wapiga kura waliotoa maoni na vigezo vya kuchagua viongozi.

CHANGAMOTO.
Zipo changamoto nyingi ambazo zimejionesha kutoka kwa wananchi wakati wa kufanya utafiti huu.
Kwa mfano:
a)Wananchi wengi hasa vijana kwenye vijiwe (magenge) vya 'Boda Boda' na kahawa walikuwa wakidai wapatiwe chochote ili waweze kutoa ushirikiano. Jambo hili ni changamoto inayotokana na mazoea ya watu kudai chochote hata kwa jambo lenye manufaa ya kueta hatima nzuri kwa nchi yao. Pia walielekeza kusikiliza Zaidi au kusikiliza amri kutoka kwa kiongozi wao, jambo ambalo ni hatari kwa mtazamo chanya katika maamuzi ya kuchagua kiongozi wenye sifa.

b)Kutokana na umuhimu wa vigezo na vipaumbele vya kumchagua kiongozi, wananchi (washiriki wa utafiti) walio wengi walitaka kuchagua vigezo vyote vilivyopo badala ya kimoja tu kama ilivyoainishwa kwenye maelezo ya dodoso la utafiti. Hii ilitokana na kero nyingi za wananchi hazijafanyiwa kazi.

c)Baadhi ya wananchi, hasa mkoani Mtwara walikuwa na hofu ya kushiriki wakidhani utafiti huu umehusisha serikali na hivyo, ni moja ya upelelezi kutambua watu wasiounga mkono chama tawala. Hili lilitokana na vurugu za maswala ya gesi miaka iliyopita.

d)Baadhi ya washiriki waliamini (kwa fikra zao) kuwa mpangilio wa maswali uliegemea chama tawala kwa vile chama tawala (CCM) kimeonekana kuwa cha kwanza kwenye orodha ya maswali kwenye dodoso.

e) Wananchi wengi walikuwa wakisita kutoa maoni/ kushiriki kutokana na kuhisi kuwa utafiti huu unahusiana na kampeni za vyama fulani au jina mojawapo la mgombea au kuhusisha serikali katika kuona na kutathimini mapungufu ya kiutendaji.

Kutokana na changamoto hizo, Positive Thinkers bado inamini, elimu inahitaji kwa wananchi ili waweze kuwa na ufahamu wa kutosha na kushiriki kikamilifu wakati wa kupiga kura na kufanya maamuzi sahihi na kwa malengo chanya na kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

UCHAMBUZI WA DATA.
Uchambuzi wa Sampuli kwa Mfumo wa Elektroniki ulitumika Ili kurahisisha utaratibu wa kuchuja sampuli na kuainisha majibu yaliyotolewa na washiriki, PTT ilibuni mfumo wa elektroniki wa sayansi ya komputa (fast web applications system) unaojulikana kwa jina la "PTT Research Data application" .Mfumo huu ulitumiwa na watafiti na walipewa mafunzo kabla ya kuanza utafiti namna ya kuingiza taarifa za utafiti kwa mfumo wa kielektroniki.

Mfumo huu wa kitaalumu kwa teknologia ya (Web based application system) ulioruhusu kuona bayana hali halisi ya matokeo ya utafiti mahala popote kila mtafiti anapoingiza majibu. Na huu ni mtizamo chanya na siyo hasi kwa vyama vyetu vinavyokuwa madarakani ili kuanza kufikiria aina hizi za teknologia. Na mfumo huu unatuma ujumbe moja kwa moja kwa Tume ya Uchaguzi(NEC). Kuanza kufikiria kwenda kwenye teknologia ambayo hairuhusu udanganyifu wa uhesabiwaji wa kura. Na pia mfumo huu unatuma ujumbe kwa vyama vya siasa kutotegemea kuiba kura na kuchelewesha kuhesabu kura. Ufumo huu haukwepeki maana dunia ipo kwenye mifumo hii ya sayansi na teknolojia. Kwa matumizi ya aina hii ya mifumo ya kielektroniki, wananchi wategemee viongozi au chama kinachochukua dola kutekeleza ahadi kwa vitendo kwa sababu hakutakuwa na nafasi ya kufikiria kwamba kuna njia nyingine yeyote itayolazimisha wizi wowote na ucheleweshaji wa kuhesabiwa kura.

Positive Thinkers Tanzania ina amini hakuna, chama chochote cha siasa kinachotawala milele kwa mifumo inayoruhusu teknologia ya kisasa. Mifumo ya aina hii, mbali na kurahisisha utendaji wa kazi. Pia kuna mifumo mingine ya kisasa inayoruhusu elimu ya umma kwa pamoja na kwa majadiliano na aina hii ya mifumo ya mawasiliano ndiyo hatari Zaidi kwa nchi zinazohitaji maendeleo kutoka kwenye mifumo mibaya. Mfano ( mitandao ya kijamii, whatapps na n.k).

Mfumo wa PTT Research Data application, nitakao ueleza na kuuangalia ulivyotumika. Utakuwa umejibu maswali mengi sana kwa wandishi wa habari na wadau wote katika sintofahamu ya kuhesabiwa kwa kura katika chaguzi zetu zilizopita na pia katika uchaguzi mkuu octoba 2015..

HITIMISHO.
Pamoja na changamoto nyingi zilizoonekana kwa pande zote; watafiti na washiriki, matokeo ya utafiti huu yameleta mwanga katika maswala ya maamuzi hasa yanayohusu hatima ya nchi katika kuchagua viongozi watakao faa kuongoza nchi, na wananchi kwa ujumla. Wananchi wameanza kupata mwanga na weledi katika kufanya mamuzi chanya katika kuchagua viongozi wanao wahitaji bila kufuata itikadi zao na wakizingatia kwa makini kiongozi anayefanya kwa vitendo.

Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, ijapokuwa wananchi na wanasiasa waliowengi wanadhani kuwa viongozi wa kisiasa watategemea na idadi ya wanachama wenye itikadi zao, yapo makundi ndani ya vyama ambayo yanatambua kuwa itikadi ya chama siyo kigezo bali sifa na vigezo vya kiongozi (mgombea) ndiyo msingi wa kumchagua kiongozi anayefaa kuongoza. Wananchi wamechoshwa na rushwa na ufisadi uliokithiri unaotendwa na watumishi wa umma na wanasiasa na haya yote hujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kutokana na kura zilizopigwa kuhusu sifa na vigezo vya Raisi atakayefaa. Sifa na kigezo cha utendaji kwa vitendo kimechukua nafasi kubwa na kupata kura 1619 (49%) ya kura zote zilizopigwa. Hii inadhirisha kuwa, raisi anayetarajiwa lazime awe na sifa au historia ya utendaji kwa vitendo vinavyodhirika.

Kutokana na utafitifu huu, Positive Thinkers Tanzania imebaini kuwa wananchi wenyewe ndiyo waamuzi wa mwisho katika kufanya maamuzi chanya ili hatimaye Tanzania iwe nchi itayopiga hatua kiuchumi, kisiasa na n.k . Mwandishi wa vitabu Napoleon Hill's katika kitabu chake cha OUTWITTING THE DEVIL. Alizungumzia na kutoa elimu katika undani wa siri na uhuru katika mafanikio ( The secret to freedom and Success) alisema ~Most real failures are due to limitations which men set up in their own minds. " na akaendelea kueleza "The greatest barrier to their recovery, is their own fear and self-doubt instilled by their recent experience. Nafikiri Watanzania tunafahamu changamoto tunazozipitia. Positive Thinkers inaamini watazania wenyewe ndiyo waamuzi katika kufanya maamuzi sahihi (chanya au hasi.). Na utafiti huu umeonya kuwa watanzania wanaweza kufanya maamuzi.

Ahsanteni na pamoja Zaidi.
Tibatizibwa Gulayi Yabutinga.
Raisi wa Wanafikra Chanya Tanzania (PTT)
Jumapili 29/03/2015
 

Attachments

  • Matokeo ya jumla.jpg
    Matokeo ya jumla.jpg
    126.7 KB · Views: 197
Chama Chenye Mvuto ni Chadema right?....so Why not Dr Slaa
 
Chama Chenye Mvuto ni Chadema right?....so Why not Dr Slaa

SWALI LA CHAMA CHENYE MVUTO, Lililenga washiriki kila mtu na ikitikadi yake awaeleze watafiti ktk eneo analoishi au kufanya kazi chama gani chenye mvuto na kupendwa na wananchi.

Kulingana na kura zilizopigwa, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa chama cha siasa nchini kilichochukua nafasi ya kwanza kuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA; ambacho kilipata kura 1471 (44.6%). Kikifuatiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichochukua nafasi ya pili kwa kura 1136 (34.4%). Nafasi ya tatu kwa mvuto ilichukuliwa na Civic United Front (CUF) kwa kura 348(10.6%); na nafasi ya nne ilichukuliwa na NCCR-Mageuzi kwa kura 61 (1.8%). Hata hivyo, utafiti ulibaini kuwa wapo wananchi wengi wasio na uchabiki,ufuasi wala mvuto wa chama chochote cha siasa. Kundi hili la wananchi lilijibu "Sina Chama", ambapo jumla ya kura 251 (7.6%) zilipigwa na washiriki wa utafiti wasio na chama cha siasa.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti kama ilivyooneshwa kwenye jedwali Na. 13, inaonesha kuwa siyo washiriki wote wa chama fulani cha siasa walipendelea vyama vyao. Kwa mfano: washiriki 171 wa CHADEMA walisema kuwa CCM ndiyo chama chenye mvuto zaidi nchini, wakati huo washiriki 66 wa CCM walipigia kura CHADEMA.
 
kwa mujibu wa anwani ilipo ofisi ya Positive Thinkers ndipo zilipo ofisi za kampuni mojawapo anayomili Lowassa Uongo kweli????
 

Attachments

  • IMG-20150329-WA0004.jpg
    IMG-20150329-WA0004.jpg
    66.1 KB · Views: 100
Nyie mmeshakula pesa ya Edward kaeni kimya, fanyeni tafiti nyingine mvute pesa this time vuteni pesa ya uhakika mwambieni ataongoza kwa asilimia 96 na atakayefuata Dr. Slaa kwa 56% ila chama kinachopenwa zaidi kiwe Chadema kwa asilimia 80 CCM 67% halafu asilimia 96 wanachukia ufisadi na rushwa. hiyo ndio tafiti ya kisayansi zaidi ya hii mliofanya
 
Back
Top Bottom