Vikao vya Harusi
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 532
- 165
Kwa ufupi
Unyanyasaji wa watoto ndani ya ndoa
ni suala binafsi. Kwa mfano, mtoto
akitumia vibaya shilingi mia mbili au
hata elfu tano za baba au mama na
kuchomewa mikono yake kama adhabu,
ni dhahiri kabisa kwamba hili ni suala
binafsi na litashughulikiwa kibinafsi
pia.
Haya, waheshimiwa na waishiwa
wasomaji wangu, kwa mara nyingine
tena, magazeti yanatoa habari ambazo
iwapo ni kweli, yanazidi hata uwezo wa
ubunifu wangu. Ndiyo maana nilipata
barua kibao.
Makengeza,
Ni matumaini yangu kwamba
maprofesa wetu wa sheria wanasikiliza
kwa makini maneno yanayotolewa na
watu wengine wanaojidai kuwa na
wataalamu wa sheria. Kwa mfano wiki
iliyopita tumeambiwa kwamba suala la
ubakaji, hata kama limefikishwa hadi
vituo vya polisi au kutangazwa
hadharani, ni suala binafsi. Nadhani
tafsiri hii itatusaidia sana (sisi
wanaume hasa) pamoja na kusaidia
serikali isilazimike kujaza jela kutokana
na mihemko ya watu wanaoshindwa
kuihimiliki. Kwa hiyo, katika vitabu vya
sheria, pawe na sehemu kabisa na
makosa binafsi. Na ili kuwasaidia kaka
(na dada) zangu wasomi, naomba nitoe
yafuatayo kama masuala binafsi,
yanafanyika na watu binafsi na
ubinafsi wao.
Masuala yote ya jinsia ni masuala
binafsi, yaani kupigwa kwa mke,
kupewa ulemavu na hata kuuliwa ndani
ya ndoa ni suala binafsi. Aidha,
unyanyasaji kijinsia wa aina yoyote
kuanzia kushikwashikwa hadi kubakwa
na kunajisiwa uhesabiwe kuwa na suala
binafsi pia. Ila iwapo mwanamume
anapigwa na mwanamke, hili ni kosa la
jinai maana hii inaenda kinyume cha
maumbile.
Unyanyasaji wa watoto ndani ya ndoa
ni suala binafsi. Kwa mfano, mtoto
akitumia vibaya shilingi mia mbili au
hata elfu tano za baba au mama na
kuchomewa mikono yake kama adhabu,
ni dhahiri kabisa kwamba hili ni suala
binafsi na litashughulikiwa kibinafsi
pia.
Wizi pia ni suala binafsi. Mtu
anapokupimia oili ndani ya daladala,
au hata kukutisha na panga na
kukunyanganya pesa ni suala binafsi.
Hata ufisadi ni suala binafsi. Kwa nini
mtu anaamua kufisadi. Ni kwa sababu,
kwa maoni yake binafsi, anaona mfuko
wake binafsi haujajaa kulingana na
matakwa binafsi ya nafsi yake.
Ila tu, inabidi kutoa hadhari. Kulingana
na misingi ya sheria asilia, inabidi
kutofautisha kati ya walio nacho na
wasio nacho. Ndiyo maana, mke
akimpiga mume, lazima ashtakiwe kwa
kufanya tendo kinyume cha maumbile.
Naam. Simba akimrarua swala,
atashtakiwa, lakini swala wakiungana
kumwadhibu simba, lazima
wachukuliwe hatua kwa pamoja maana
wanatishia amani na utulivu wa mbuga.
Na kwa binadamu vivyohivyo.
Itakuwaje swala aamke na kulalamika
kwamba simba amemrarua?
Simba mtarajiwa.
Haya na mwingine,
Makengeza,
Mimi nawashangaa Wabongo
wenzangu. Mkubwa katembea na
mdogo. Hata kwa kutumia nguvu. Kisha
tunaambiwa ni suala binafsi. Kipya ni
nini hapa. Tangu zamani, walinzi wetu
wa usalama (hasa usalama wa madume
na vigogo) wamesema siku nyingi.
We si ulikunywa bia zake ana haki ya
kudai malipo.
Yaani sista, kweli unataka kumuumbua
mumeo. Hebu rudini nyumbani
mpatane.
Ha ha ha ha. Na nguo kama hii
unategemea nini?
Ubinadamu huo jamani. Angalia
anavyopendeza (huku udenda
ukidondoka)
Ndiyo maana wanawake wengi
wamekuwa na utu na busara wa
kunyamazia mambo hayo. Nyeti za
dume ni suala nyeti na zinapaswa
kubaki nyeti. Potelea mbali kama
wananyamaza kwa sababu wanajua
wanapoteza muda na heshima
wakilalamika kwa sababu wanageuziwa
kibao kila wakati. Potelea mbali kama
wadogo hawana imani na mfumo ili
mradi umegusa mkubwa. Suala ni
kwamba wananyamaza hivyo ni suala
binafsi na hakuna cha zaidi.
Ndiyo maana naona dunia imeharibika
kabisa. Sisi wazee tunakumbuka enzi za
blanketi mtu. Wakubwa wakienda
mikoani watalalaje peke yao bila kutiwa
joto kidogo. Hivyo blanketi chapa mtu
ilikuwa sehemu muhimu ya huduma
kwa kigogo. Na Redio Manzese
iliwaongelea wakubwa wengi wenye
----- wa ngono maana walikuwa
wanawashwa kila wakati na msichana
mzuri ndiye pekee mwenye uwezo wa
kumkuna. Waziri fulani alipachikiwa
jina la Mgonjwa kutokana na tabia hii.
Kwa hiyo iwapo tabia hii inaendelea
kuna shida gani. Tujali haki ya nani?
Haki ya kadogo eti asinyanyaswe au
haki ya kigogo kutowashwa? Ni wazi
kabisa kwamba haki ya kigogo
kutowashwa ni muhimu zaidi. Hata
kama msichana ni mdogo namna gani si
hoja. Haki ya kigogo inabaki palepale
na tukishapukutisha haki hii, sijui
tutafikia wapi.
Kigogo mstaafu.
Lakini mwingine hakukubaliana nao
kabisa.
Mwishiwa mwenzangu,
Nategemea utaelewa kwa sababu wewe
ni mwishiwa si mheshimiwa kama hawa
wengine wenye ubinafsi wa nafsi katika
kudai masuala ya jinai ni masuala
binafsi. Hebu tuangalie stori yenyewe:
Kufanya ngono na msichana mdogo ni
kosa la jinai. Hata kama alitaka
mwenyewe bado ni kosa la jinai.
Kuandika vitisho kwenye SMS kwa mtu
yeyote ni kosa la jinai, hata kama
umekasirika namna gani
Mimi na wewe tukifanya makosa hayo
tutakamatwa mara moja. Hebu ona
wale waliofungwa juzi kwenye masuala
ya pembe za ndovu. Sasa hawa
wakubwa wao wataguswa. Sisi punda ni
wakupondwa. Lakini inaonekana
kwamba kuna dawa fulani wanayopewa
vigogo inayowafanya wasiguswe. Daima
ukitaka kuwashika, mikono inateleza,
hata ulimi unateleza hadi wanadai ni
mambo binafsi.
Ndiyo maana najiuliza kwa nini sisi
waishiwa hatuwezi kufanya kitu. Kwa
nini asasi zilizoshikia bango jambo hili
kwa kudai mtuhumiwa ajiuzulu tu
wasitangulie mahakamani na kufungua
kesi ya madai kwanza? Kama ni suala
binafsi, kwa nini tusifanye mashtaka
binafsi hadi wale wenye nafasi waache
ubinafsi wa nafsi zao na kukubali
kwamba hili ni suala la jinai. Ni suala
la kuhakikisha si tu kwamba haki
itatendeka bali itaonekana wazi
kwamba imetendeka.
Naam. Maana iwapo mashtaka haya si
kweli, hata yule aliyetoa naye amefanya
kosa la jinai, kumkashifu mtu tena
kigogo kabisa. Wananchi tuna haki ya
kujua ukweli. Tuna haki ya kudai
ukweli ili tuweze kupima tufanye nini.
Lakini mwisho wa yote, wakati umefika
kuona kwamba unyanyasaji kijinsia si
suala binafsi hata kidogo. Hebu tujiulize
hata kwenye jamii zetu, kwa nini mwizi
anakamatwa mara moja lakini mbakaji,
fataki, mtongozaji wa mabinti wadogo
hawakamatwi kabisa, eti wana dawa
fulani inayofanya wasionekane. Si
kweli. Ni kwamba tunafumbia macho
makosa hayo, eti hatukubali kwamba
kumwumiza msichana au mwanamke
kimwili na kiakili ni uhalifu, kuharibu
nafasi yake katika jamii ni uhalifu,
kumpatia magonjwa ya mwili na akili
ni uhalifu. Kumpiga mwenzio ndani ya
nyumba na kusababisha majeraha na
hata ulemavu ni uhalifu. Kwa nini
hatukubali?
Hivyo ubinafsi wa wenye nafasi
wasituvuruge. Wakati umefika kuona
kwamba masuala haya ni masuala ya
uhalifu. Lazima haki itendeke.
Unyanyasaji wa watoto ndani ya ndoa
ni suala binafsi. Kwa mfano, mtoto
akitumia vibaya shilingi mia mbili au
hata elfu tano za baba au mama na
kuchomewa mikono yake kama adhabu,
ni dhahiri kabisa kwamba hili ni suala
binafsi na litashughulikiwa kibinafsi
pia.
Haya, waheshimiwa na waishiwa
wasomaji wangu, kwa mara nyingine
tena, magazeti yanatoa habari ambazo
iwapo ni kweli, yanazidi hata uwezo wa
ubunifu wangu. Ndiyo maana nilipata
barua kibao.
Makengeza,
Ni matumaini yangu kwamba
maprofesa wetu wa sheria wanasikiliza
kwa makini maneno yanayotolewa na
watu wengine wanaojidai kuwa na
wataalamu wa sheria. Kwa mfano wiki
iliyopita tumeambiwa kwamba suala la
ubakaji, hata kama limefikishwa hadi
vituo vya polisi au kutangazwa
hadharani, ni suala binafsi. Nadhani
tafsiri hii itatusaidia sana (sisi
wanaume hasa) pamoja na kusaidia
serikali isilazimike kujaza jela kutokana
na mihemko ya watu wanaoshindwa
kuihimiliki. Kwa hiyo, katika vitabu vya
sheria, pawe na sehemu kabisa na
makosa binafsi. Na ili kuwasaidia kaka
(na dada) zangu wasomi, naomba nitoe
yafuatayo kama masuala binafsi,
yanafanyika na watu binafsi na
ubinafsi wao.
Masuala yote ya jinsia ni masuala
binafsi, yaani kupigwa kwa mke,
kupewa ulemavu na hata kuuliwa ndani
ya ndoa ni suala binafsi. Aidha,
unyanyasaji kijinsia wa aina yoyote
kuanzia kushikwashikwa hadi kubakwa
na kunajisiwa uhesabiwe kuwa na suala
binafsi pia. Ila iwapo mwanamume
anapigwa na mwanamke, hili ni kosa la
jinai maana hii inaenda kinyume cha
maumbile.
Unyanyasaji wa watoto ndani ya ndoa
ni suala binafsi. Kwa mfano, mtoto
akitumia vibaya shilingi mia mbili au
hata elfu tano za baba au mama na
kuchomewa mikono yake kama adhabu,
ni dhahiri kabisa kwamba hili ni suala
binafsi na litashughulikiwa kibinafsi
pia.
Wizi pia ni suala binafsi. Mtu
anapokupimia oili ndani ya daladala,
au hata kukutisha na panga na
kukunyanganya pesa ni suala binafsi.
Hata ufisadi ni suala binafsi. Kwa nini
mtu anaamua kufisadi. Ni kwa sababu,
kwa maoni yake binafsi, anaona mfuko
wake binafsi haujajaa kulingana na
matakwa binafsi ya nafsi yake.
Ila tu, inabidi kutoa hadhari. Kulingana
na misingi ya sheria asilia, inabidi
kutofautisha kati ya walio nacho na
wasio nacho. Ndiyo maana, mke
akimpiga mume, lazima ashtakiwe kwa
kufanya tendo kinyume cha maumbile.
Naam. Simba akimrarua swala,
atashtakiwa, lakini swala wakiungana
kumwadhibu simba, lazima
wachukuliwe hatua kwa pamoja maana
wanatishia amani na utulivu wa mbuga.
Na kwa binadamu vivyohivyo.
Itakuwaje swala aamke na kulalamika
kwamba simba amemrarua?
Simba mtarajiwa.
Haya na mwingine,
Makengeza,
Mimi nawashangaa Wabongo
wenzangu. Mkubwa katembea na
mdogo. Hata kwa kutumia nguvu. Kisha
tunaambiwa ni suala binafsi. Kipya ni
nini hapa. Tangu zamani, walinzi wetu
wa usalama (hasa usalama wa madume
na vigogo) wamesema siku nyingi.
We si ulikunywa bia zake ana haki ya
kudai malipo.
Yaani sista, kweli unataka kumuumbua
mumeo. Hebu rudini nyumbani
mpatane.
Ha ha ha ha. Na nguo kama hii
unategemea nini?
Ubinadamu huo jamani. Angalia
anavyopendeza (huku udenda
ukidondoka)
Ndiyo maana wanawake wengi
wamekuwa na utu na busara wa
kunyamazia mambo hayo. Nyeti za
dume ni suala nyeti na zinapaswa
kubaki nyeti. Potelea mbali kama
wananyamaza kwa sababu wanajua
wanapoteza muda na heshima
wakilalamika kwa sababu wanageuziwa
kibao kila wakati. Potelea mbali kama
wadogo hawana imani na mfumo ili
mradi umegusa mkubwa. Suala ni
kwamba wananyamaza hivyo ni suala
binafsi na hakuna cha zaidi.
Ndiyo maana naona dunia imeharibika
kabisa. Sisi wazee tunakumbuka enzi za
blanketi mtu. Wakubwa wakienda
mikoani watalalaje peke yao bila kutiwa
joto kidogo. Hivyo blanketi chapa mtu
ilikuwa sehemu muhimu ya huduma
kwa kigogo. Na Redio Manzese
iliwaongelea wakubwa wengi wenye
----- wa ngono maana walikuwa
wanawashwa kila wakati na msichana
mzuri ndiye pekee mwenye uwezo wa
kumkuna. Waziri fulani alipachikiwa
jina la Mgonjwa kutokana na tabia hii.
Kwa hiyo iwapo tabia hii inaendelea
kuna shida gani. Tujali haki ya nani?
Haki ya kadogo eti asinyanyaswe au
haki ya kigogo kutowashwa? Ni wazi
kabisa kwamba haki ya kigogo
kutowashwa ni muhimu zaidi. Hata
kama msichana ni mdogo namna gani si
hoja. Haki ya kigogo inabaki palepale
na tukishapukutisha haki hii, sijui
tutafikia wapi.
Kigogo mstaafu.
Lakini mwingine hakukubaliana nao
kabisa.
Mwishiwa mwenzangu,
Nategemea utaelewa kwa sababu wewe
ni mwishiwa si mheshimiwa kama hawa
wengine wenye ubinafsi wa nafsi katika
kudai masuala ya jinai ni masuala
binafsi. Hebu tuangalie stori yenyewe:
Kufanya ngono na msichana mdogo ni
kosa la jinai. Hata kama alitaka
mwenyewe bado ni kosa la jinai.
Kuandika vitisho kwenye SMS kwa mtu
yeyote ni kosa la jinai, hata kama
umekasirika namna gani
Mimi na wewe tukifanya makosa hayo
tutakamatwa mara moja. Hebu ona
wale waliofungwa juzi kwenye masuala
ya pembe za ndovu. Sasa hawa
wakubwa wao wataguswa. Sisi punda ni
wakupondwa. Lakini inaonekana
kwamba kuna dawa fulani wanayopewa
vigogo inayowafanya wasiguswe. Daima
ukitaka kuwashika, mikono inateleza,
hata ulimi unateleza hadi wanadai ni
mambo binafsi.
Ndiyo maana najiuliza kwa nini sisi
waishiwa hatuwezi kufanya kitu. Kwa
nini asasi zilizoshikia bango jambo hili
kwa kudai mtuhumiwa ajiuzulu tu
wasitangulie mahakamani na kufungua
kesi ya madai kwanza? Kama ni suala
binafsi, kwa nini tusifanye mashtaka
binafsi hadi wale wenye nafasi waache
ubinafsi wa nafsi zao na kukubali
kwamba hili ni suala la jinai. Ni suala
la kuhakikisha si tu kwamba haki
itatendeka bali itaonekana wazi
kwamba imetendeka.
Naam. Maana iwapo mashtaka haya si
kweli, hata yule aliyetoa naye amefanya
kosa la jinai, kumkashifu mtu tena
kigogo kabisa. Wananchi tuna haki ya
kujua ukweli. Tuna haki ya kudai
ukweli ili tuweze kupima tufanye nini.
Lakini mwisho wa yote, wakati umefika
kuona kwamba unyanyasaji kijinsia si
suala binafsi hata kidogo. Hebu tujiulize
hata kwenye jamii zetu, kwa nini mwizi
anakamatwa mara moja lakini mbakaji,
fataki, mtongozaji wa mabinti wadogo
hawakamatwi kabisa, eti wana dawa
fulani inayofanya wasionekane. Si
kweli. Ni kwamba tunafumbia macho
makosa hayo, eti hatukubali kwamba
kumwumiza msichana au mwanamke
kimwili na kiakili ni uhalifu, kuharibu
nafasi yake katika jamii ni uhalifu,
kumpatia magonjwa ya mwili na akili
ni uhalifu. Kumpiga mwenzio ndani ya
nyumba na kusababisha majeraha na
hata ulemavu ni uhalifu. Kwa nini
hatukubali?
Hivyo ubinafsi wa wenye nafasi
wasituvuruge. Wakati umefika kuona
kwamba masuala haya ni masuala ya
uhalifu. Lazima haki itendeke.