Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,756
- 239,421
Huyu Dc kwa muda mfupi sana alijipatia umaarufu wa pekee hasa baada ya wananchi wa Iringa kukumbwa na mafuriko.
Alishinda na wahanga kwa 24/7 na kuhakikisha wanapata misaada ya hali na mali, wengi tulimpongeza kwa jambo hilo na tukaona sasa kweli Iringa imepata DC hasa, ilifika wakati jamaa alijitosa ndani ya tope tena bila viatu na wala hakuogopa hata hookworms, lengo likiwa lile lile la kuokoa maisha ya wahanga.
Kibao kilikuja kugeuka pale alipoanza kujitafutia umaarufu kupitia mafuriko hayo, sasa badala kuwa mwokozi tu akaanza na kutafuta promo, mara kabeba mwandishi ili apigwe picha ionekane kabeba mhanga wa mafuriko!
Wadau wakastuka, mbiu zikapigwa nchi nzima kwamba "eti mkuu anautafuta u-RC kufa na kupona". Cha ajabu sasa baada ya wakuu wa mikoa kupatikana mjomba katoweka hewani!
Swali ni je ni kweli Kasesera mbilinge zote zile ulilenga U-RC?