Rev. Msigwa amfagilia rais Kikwete

Rev. Msigwa amfagilia rais Kikwete

hasason

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
1,648
Reaction score
1,542
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mh.Peter Msigwa.


Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mh.Peter Msigwa amefanya mkutano hapo jana katika viwanja vya Mwembetogwa, mkoani humo. Mkutano huo ambao ulikuwa wa kufungia mwaka 2013, Msigwa pia aliutumia mkutano huo kwa kuwapongeza baadhi ya mawaziri ambao utendaji kazi wao unaonekana kuwa mzuri, akiwemo Waziri wa Wizara ya Maji na Naibu Wake ,Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Mazingira ambao wameonesha msimamo wa kweli katika kuwatumikia wananchi.

Katika hatua nyingine mbunge Msigwa amemshukia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na kusema kuwa anatafuta umaarufu binafsi kuliko kukijenga chama chake na kuwa hana nia njema na CHADEMA,hivyo amewataka Wanachadema wa jimbo la Iringa mjini kutomsikiliza huku akibainisha kuwa Mwanachama na Kiongozi mzuri ni yule ambae anafanya kazi ya kukijenga chama chake na si kujijenga yeye binafsi.

Amesema kuwa iwapo Zitto hatotaka kumsikiliza mwasisi wa Chama hicho, Mzee Mtei wala kuwasikiliza viongozi wa juu wa chama hicho akiwemo mwenyekiti wa katibu mkuu, ni wazi hakitakii mema CHADEMA na wana Chadema hawana budi kumpuuza kiongozi na mwanachama yeyote mwenye lengo la kuua chama.

Kuhusu rasimu ya Katiba, Mbunge Msigwa amempongeza Rais Kikwete kuwa ameonyesha ushujaa wa hali ya juu katika kupigania upatikanaji wa katiba mpya, na kuwa iwapo wabunge wa CCM watapinga wao kama Chadema watarudi kwa wananchi kuhamasisha kupiga kura ya kuikataa katiba itakayopendekezwa na wabunge wa CCM.

Aidha Msigwa ameongeza kusema kuwa atakuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali kama itaonekana kuwa na viongozi dhaifu huku akiwataka watanzania kutathimini yale yote waliyofanya mwaka 2013 na kuwatakia kheri ya mwaka mpya,
 
Msigwa ameongea points sana ila mleta mada umeona tu "amemfagilia Kikwete" hujaona vingine alivyoongea. Tuache kupotosha mambo jamani
 
Sasa hivi tutamshangaa asiemfagilia JK sio anaemfagilia.

Lipumba, Mbowe, Slaa, Seif Sharif, Mnyika, Lissu,Mbatia,Zitto,Mrema,Cheyo N.K wote kwa Nyakati tofauti wamekuwa wakimsifia jk hadharani baada ya kushindwa kuvumilia kukaa kimya.
 
Msigwa ameongea points sana ila mleta mada umeona tu "amemfagilia Kikwete" hujaona vingine alivyoongea. Tuache kupotosha mambo jamani

Are you certainly , its only that i have observed??
 
Hawa sio vigeugeu elewa hata mateka anapopewa maji ya kunywa husahau umateka na kushukuru kwa maji.vivyo hivyo pamoja na mikataba mibovu aliyo ridhia Raisi inabidi tumsifu kukubali kuundwa kwa katiba mpya kwani kila mwenye kuitakia mema JMT anaamini itasaidi mustakabali wa nchi zetu Tanganyika na Zanzibari
Ni vigeugeu hawaaa pipo
 
Weee msigwa amemkana rais wake slaa!!! Aangalie asiambiwe msaliti,ameanza kuwa rafiki na maccm! Ooh aangalie aise wachaga wako kama mmarekani hawana rafiki wa kudum.
 
Weee msigwa amemkana rais wake slaa!!! Aangalie asiambiwe msaliti,ameanza kuwa rafiki na maccm! Ooh aangalie aise wachaga wako kama mmarekani hawana rafiki wa kudum.

Are you sure?
 
Weee msigwa amemkana rais wake slaa!!! Aangalie asiambiwe msaliti,ameanza kuwa rafiki na maccm! Ooh aangalie aise wachaga wako kama mmarekani hawana rafiki wa kudum.

Pamoja na kuwa ni wapinzani lakini ishu ya katiba rais kikwete lazima asifiwe coz sio ilani ya CCM lakini amekubali matakwa ya wananchi ya kupata katiba mpya. "Give devil his due" hujui msemo huu
 
vyama vingi vya siasa hapa Tanzania vipo kwa ajili ya ruzuku lakini si kwa malengo ya kuingia ikulu na ndio maana hadi leo hii viongozi ama wanachama wa vyama hivyo wanatakiwa kuwasikiliza waasisi wa vyama,hii inamaanisha kuwa hakuna mambo mapya yanayotakiwa kuwepo labda tu yawe yamepata baraka na wenye vyama.
Bado kuna safari ndefu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom