Reserved ID zinamilikiwa na nani?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,084
Siasa ni propaganda na propaganda ili ziwe na nguvu inabidi zisokomezwe kwenye masikio ya wengi, na ili hili liwezekane unahitaji team ya watu vijana mahiri wanaojua kuendesha makundi ya propaganda
Tuko kwenye kizazi cha utandawazi, ulimwengu wa upashanaji habari kwa njia mbalimbali, mitandao ya kijamii ikiwa ndio mahiri sana kwa sasa...!!!
Jamii Forum ni mmojawapo wa mitandao ya kijamii Tanzania maarufu unaopendwa na kuheshimika zaidi kama chanzo muhimu cha habari za uhakika na za kuaminika...
Ni kwa sababu hiyo mtandao huu umewavutia wengi mpaka viongozi wakubwa wa kisiasa nk.. Hivyo basi wamekuwa wakiutumia kufikisha jumbe zao, fikra na maono....
Ili uweze kuitumia JF ni lazima ujiunge na kuwa mwanachama... Kwa kufuata taratibu zilizopo hasa kutumia utambulisho bandia
Kigezo hiki kimewapa mwanya mkubwa vikundi vya propaganda kutengeneza wanachama wengi kwa matumizi binafsi na matakwa ya watu fulani
Ni kawaida kila linapotokea jambo kubwa la kisiasa nchini ID ngeni hujitokeza na makala ndefu kulipigia chapuo jambo husika, au kulipinga kwa nguvu zote, kumfagilia fulani ama kumponda fulani kwa kumzushia tuhuma mbalimbali....
Joto la kisiasa limepanda kidogo kipindi hiki cha lala salama ya mwaka 2018 kuna makala nyingi za ID ngeni na zote ziko jukwaa la kisiasa?
Mmiliki ni nani? Kwa vyovyote ni ile kamati ya rohombaya [emoji23][emoji23][emoji23] sio Rohombaya
 
Ha ha ha haaaaa... Nimekumbuka kipindi cha uchaguzi, huwa zinaibuka ID hizo mpaka unashangaa.

Kuna watu waliambiwa na wao watumie mitandao kuwajibu wanaowaponda so nadhani ndo ID za hao.

Lakini pia kuna wale 7k per post.
 
Ha ha ha haaaaa... Nimekumbuka kipindi cha uchaguzi, huwa zinaibuka ID hizo mpaka unashangaa.

Kuna watu waliambiwa na wao watumie mitandao kuwajibu wanaowaponda so nadhani ndo ID za hao.

Lakini pia kuna wale 7k per post.
Halafu mode of posting inafanana... Ni kama vile ni mtu mmoja anaandika na kupost kupitia ID mbalimbali, ID zombies, maruhani
 
Halafu mode of posting inafanana... Ni kama vile ni mtu mmoja anaandika na kupost kupitia ID mbalimbali, ID zombies, maruhani
Ha ha ha haaaa... Multiple ID. Kuna uzi mmoja nimeuona leo una propaganda chafu sana nikatazama ile ID ni JF senior tu ila ule muandiko upo kwenye makabrasha kabisa.

Ni sawa leo wewe ukafungue ID nyingine hata ujifiche vipi sisi Tunaoishi na wewe zaidi ya miaka mitano humu tutakujua tu.
 
Siasa ina mambo ya ajabu sana, dakika za kuhesabu unashangaa linaibuliwa zengwe fulani si raia, ili mradi tu kumwondolea sifa.

Hii ni sawa umeoa mke umezaa nae watoto kadhaa, unajua kabisa ni wanao na watoto wanajua wewe ni baba yao ghafla mkeo ama watu wa nje wanakuambia fulani na fulani sio wanao.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] lazima tu nitajulikana
 
That's why I hate politik
 
Siku hizi hichi ki msemo maarufu kinaitwa UMETUMWA.Yaan ukijaribu kutoa maoni yako jinsi unavoona mambo yanayoenda.Utaambiwa umetumwa,mi huwa nachoka naamuwa niende mtaa wa Arusha nkale ZANZIBAR PIZZA
 
Siku hizi hichi ki msemo maarufu kinaitwa UMETUMWA.Yaan ukijaribu kutoa maoni yako jinsi unavoona mambo yanayoenda.Utaambiwa umetumwa,mi huwa nachoka naamuwa niende mtaa wa Arusha nkale ZANZIBAR PIZZA
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji44][emoji23][emoji23]hata hii umetumwa[emoji23][emoji23]
 
Wiki hii zimepungua tena zinasubiria tukio lingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…