Redio za FM zinaajiri watangazaji wasio na taaluma

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Mar 31, 2016
6,679
8,421
Kiukweli kumekuwa na kuongezeka kwa redio za FM sasa kila mtu anaajiriwa humo bila utaratibu kiasi kwamba kila MC, msanii wa movie, mwanamuziki (kasoro chura) wengi ni weupe vichwani hata kusoma ni tatizo achilia mbali kuchambua mada au kutema yai.

Mhe. Waziri peleka ule muswada bungeni wa kila mtangazaji angalau awe na digrii ya kwanza/ Bachelor toka chuo kinachotambulika.

Cc. MC Pilipiliiii
 
Wasomi wamekuwa ni wasomi wa kulalamika lalamika tuu bila hata kuwa na solutions za matatizo yao, sasa kweli mtangazaji uliye bukua adi una PHD au master's degree, lakini kiutangazaji umeachwa mbali na mbwiiga, huna ubunifu, huna mvuto wa utangazaji, yaani ni majanga matupu, leo unalalama ohooo.

Akina mbwiiga wanatuzibia riski!!
 
Kwanza hongera kwako ulietoa huu uzi kwa kuliona hilo,big up sana

Kule kahama, Shinyanga kuna kituo cha redio kinaitwa Kahama FM, duuh ni balaa

Watangazaji ni weupe kichwani. Kuna binti ninaemfahamu kabsa(jinalimehifadhiwa) alimaliza tu kidato cha nne akachukuliwa kuwa mtangazaji wakampangia kipindi cha kutangaza usiku kuanzia saa nne mpaka saa saba usiku ili awe anajifunza kidogokidogo kuongea on air, yani shida tupu.
 
Wasomi wamekuwa ni wasomi wa kulalamika lalamika tuu bila hata kuwa na solutions za matatizo yao, sasa kweli mtangazaji uliye bukua adi una PHD au master's degree, lakini kiutangazaji umeachwa mbali na mbwiiga, huna ubunifu, huna mvuto wa utangazaji, yaani ni majanga matupu, leo unalalama ohooo
akina mbwiiga wanatuzibia riski!!
Toa mfano?
 
Hao wamiliki wa hizo radio station wanaangalia cheap labour jamani . Wewe ukiajiriwa pale na PHD yako utakubali ulipwe laki 4 kwa mwezi au ndio utaleta sheria zako za kisomi.Hao wasiosoma hawana hata muda wa kujua haki zao kama wafanyakazi so ilimaradi wanapata salary end of the month kwao wameridhika.
h
Hata huku kwenye kazi zetu wapo sana watu wanaoajiriwa bila kufit qualifications za ajira husika ili mradi tu wamlipe mshahara mdogo ili wao wapate faida zaidi kuliko kuajiri professionals katika fani husika.
 
Back
Top Bottom