Red Cross Tanzania kwafutuka tena

Red Cross Tanzania kwafutuka tena

Status
Not open for further replies.

Dadiz

Member
Joined
Jun 30, 2018
Posts
20
Reaction score
8
Taarifa zilizotukia hivi punde ni kuhusu kundi la vijana wapatao 11 wameanza mchakato wa kimya kimya kuomba serikali iingilie kati kuwalazimaisha viongozi Redcross kuruhusu uchaguzi ufanyike ama la uongozi uliopo uvunjwe na kiundwe chombo huru cha mpito kuongoza chama hicho.

Inaelezwa kuwa Katiba ya Redcross inataka uchaguzi ufanyke kila baada ya miaka 5 na uchaguzi wa mwisho ulifanyika 2012 yaani miaka 7 iliyopita lakini bodi na viongozi wa Mikoa wakiendelea kung’ang’ania kubaki maradakani kinyume na katiba zote mbili yani ile ya zaman na hii mpya.

Katika kikao cha kupitisha Katiba mpya mwaka 2018 lilitolewa azimio uchaguzi uanze mwezi march 2019 lakin hadi tarehe 1 Julai bado uchaguzi haujaanza kutokana na hofu kubwa iliyotanda miongoni mwa baadhi ya viongozi kwa baadhi kuogopa kuangushwa ktk nafas zao hivyo namna pekee waliyochagua ni kusogeza mbele uchaguzi kila muda unapowadia.

Inaelezwa kuwa katika kuna taarifa za ndani kuwa kikao cha Bodi ya Taifa ya Chama hicho itakaa tar 10 julai lakini lengo kuu likiwa ni kusogeza tena mbele hadi mwaka 2021 kwa hoja dhaifu kuwa mwaka huu mwamko ni mdogo kwa wanachama na mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu. Aidha kundi dogo hususani kutoka mikoa ya Kagera, Dar esa slaaam na Arusha linasimamia msimamo wa kufanya uchaguzi mwaka huu kwani endapo hautafanyika Chama kitalazimishwa kufanya uchaguzi na serikali jambo ambalo linaleta taswira mbaya kwa jamii.

Katibu Mkuu wa Redcros alipotafutwa muda wote simu yake ilikuwa imezimwa na hata ujumbe alioutumiwa bado haujapokelewa. Na mwandishi hakumpata Rais wa chama hicho Ndg Mwadin Jecha ambaye tetesi zinasema anashinikiza uchaguzi usogoezwe mbele kwa sababu ambazo hazijfahamika. Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Deus Masawe akiwa na vinana wenzake wameeleza kuwa watajitokeza mbele ya waandishi wa habari siku moja kabla ya siku ambayo ilipangwa kuanza kuchukua fomu za uchaguzi mgazi za Mikoa endapo ratiba itabadlishwa km wanavyoshinikiza wakubwa wachache

“ Wapo wanaosingizia kuwa matawi ni machache na wengine wanasema hatuna pesa za uchaguzi huku wengine wakisema elimu haijatolewa kwa wananchi lakini hadi leo hii hata taarifa ya mamilion zilizofujwa kule kigoma kwenye REDCROSS DAY haijawekwa wazi, hata reporti ya wakuu wa idara na baadhi ya watendaji wanaopishana angani kwa maposho ya ajabu hakuna ambaye nyanyua kauli kwenye bodi maana nao wanagawiwa. Lakini zaidi mbaya kuliko zote ni baddhi ya Mikoa yenye hati chafu kutochukulowa hatua kwa watendaji hao” alimalizia Deus.
------

Taarifa hii imekanushwa, zaidi soma

 
They have a point

Usiwe mechanical
Pale Redcross pana ulaji wa kufuru hasa misaada tunayopata mingi huishia mikononi mwa wajanja, pana mama mmoja hapo ni mke wa mkubwa fulani hivi huyo kwenye pesa ni janga la taifa
 
Pale Redcross pana ulaji wa kufuru hasa misaada tunayopata mingi huishia mikononi mwa wajanja, pana mama mmoja hapo ni mke wa mkubwa fulani hivi huyo kwenye pesa ni janga la taifa
Hata huku mikoani ni taabu tupu! Kuna wakati walipata mradi wa mabilioni kilichofanyika huku mikoani vijana walichota fedha zile na kuanza kushindana kujenga mahekalu na kununua magari. Hivi Redcross ina mwenyewe?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom