Red Brigade na Green Guard ni hatari kuliko silaha za maangamizi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
inasikitisha kuona tanzania mbali na kujiita kisiwa cha amani tunashindwa kuweka misingi ya amani ili amani tuliyo nayo iwe endelevu.

ni jambo la hatari sana kuruhusu vyama vya siasa kuwa na makundi yenye hulka za kijeshi. hili ni jambo hatari sana ambalo wenye buasara waliliona na kutunga sheria ya kuzuia majeshi yetu kuingia katika siasa.

wapuuzi wanaunda makundi yenye hulka za kijeshi ndani ya vyama vya siasa.

wanasema kwenye msafara wa mamba hata kenge wapo, hivyo katika chama chochote cha siasa kuna watu watu wenye utu wanaothamini utu wa watu wengine na kwao hawako tayari kutumia maisha ya wanadamu wengine kupata vitu vidogo kama madaraka, lakini katika vyama hivyo hivyo kuna watu ambao hulka zao ni tofauti na za wanadamu wako tayari kutesa watu, kuua watu au kufanya vituko vya kinyama tena kwa watu wasio na hatia kulazimisha wao kupewa vyeo au madaraka.

hakuna anayemjua mwanadamu mwenzake yukoje maana hata wanafamilia wanaokuwa wakidhani wanafahamiana ipo siku wanageukana na kuchinjana.

hakuna anayeweza kuwajua watu hawa wenye fikra za kijinga popote walipo na kwa kuwa siasa zimejaa makundi yanayopingana yakigombania madaraka si vyema kuruhusu vyama vya siasa kuunda makundi ya kijeshi.

akitokea mhuni yeyote akapata sababu yake mwenyewe iwe ya kweli au ya uongo akiwashawishi makundi haya kwa peremende zilizo wazi kuwa tukitoka msituni tutagawana vyeo, watu wasio na mbele leo wanaahidiwa vyeo vya ajabu nani atawazuia? si nguvu ya uongozi wa vyama vyenyewe au uongozi wa nchi unaweza kuyabiti makundi haya.

tena tunawatafutia mitaji kwa urahisi kwa kufundisha vijana wetu mafunzo ya kijeshi na tunashindwa kuwapatia ajira wanabaki kuwa walinzi katika makampuni ya ulinzi.

makundi haya ni hatari kuliko wanyama wa mwituni wakali katika makazi ya wanadamu kwa maana hao tunaweza kjipanga na kuwadhibiti.

makundi haya ni hatari kuliko silaha za maangamizi maana mkikubaliana nyote mnaacha kuzitumia.

lakini makundi haya ambayo yanaweza kumtumikia yeyote anayekuja mbele yao na kuwaahidi mafanikio yao binafsi hata kama ni kuwapa ahadi zisizotekelezeka, makundi haya ambayo yenyewe yakisha lenga mafanikio fulani yanaweza kumlazimisha hata yule anayeyaongoza kubaki katika malengo yao kama yakiona kinyume kwao hakuna faida.

ni jamii ya wajinga pekee inaweza kutrade amani kwa vitu vidogo tu vya kusema makundi haya yaruhusiwe kulinda interest za makundi ya siasa kwa kuangalia withini legal framework bila kuangalia possibilities na probability za hatari zilizoko nje ya legal arena.

tunaomba serikali yetu ya awamu ya tano ione makundi haya ni jipu kuliko majipu mengine yote na kupitia sheria na vyombo ilivyonavyo ikomeshe hulka za kijeshi ndani ya vyama vya siasa.

tumekuwa tukisikia kauli kama "kama mambo yatakuwa haya nchi hii haitatawalika" kauli hizi zinaonyesha watu wenye nia ya kutumia mitaji hii lakini pengine hajapatikana mjinga wa kutangulia porini na wengine wakafuata.

tunaomba serikali mliangalie hili
 
Jombaa...wasikukoseshe usingizi..trust me...wasiwasi wangu mimi ni hao Red Brigage, in a worst case scenario labda wanaweza kugeuka Panya Rodi....kitu ambacho hakihatarishi usalama wa Taifa.
 
Jombaa...wasikukoseshe usingizi..trust me...wasiwasi wangu mimi ni hao Red Brigage, in a worst case scenario labda wanaweza kugeuka Panya Rodi....kitu ambacho hakihatarishi usalama wa Taifa.

jamani acha kabisa usiwadharau hawa maana wanasiasa ambao wako nyuma ya makundi haya ndio uwatazame kutazama uwezo wa makundi haya.

ni wazi kuwa wanasiasa wenye mawazo ya kizamani ndio wanarudisha mawazo haya katika jamii na hizi ni siasa za miaka ya 60. lakini siasa hizo za miaka ya 60 zimeisumbua sudani ikagawanyika na sio kugawanyika tu uniambie kuna mwananchi gani wa sudani kusini atapata second chance ili kujijenga kufidia mda uliopotea kwenye vurugu?

walijigawa kutoka sudani kwa kisingizio cha kunyanyaswa lakini baada ya kujitenga bado wanapigana wao kwa wao sasa walewale waliokuwa wakidai kunyanyaswa kuna wengine wanadai wanawanyanyasa wao!

yaani ukiwaruhusu wanasiasa kupata nguvu ya kijeshi basi hawa wanatumia shida kidogo zilizopo katika jamii kuficha uroho wao wa madaraka na kujidai wanatetea shida za wananchi kumbe wanatafuta madaraka wao. na kila huyu anapopata madaraka basi mwingine ambaye hajapata anatumia mtaji uleule.

ni vigumu mwanasiasa yeyote kuanza kuunda jeshi kama anaona kutafuta madaraka baada ya kukosa kwenye uchaguzi lakini ukiwaruhusu kuanza mchakato mapema basi huo unakuwa mtaji ambao wale wapuuzi wa siasa za miaka ya 60 huandaa plan B incase plan A ikifeli.

haya makundi unayoyaona kwa sasa ni mtaji wa kushawishia watu wa kumpa sapoti na wananchi wengi wanaangalia posibility. akimwambia mtu tunaenda kuchukua madaraka na wewe hapo ulipo nitakupandisha mara dufu hata sisi tusikuwa nyuma ya makundi hayo wananchi kwa vyombo vyetu tunagwanyika kila mmoja akiangalia uwezekano wa kupata zaidi.

lakini ni vigumu kuwashawishi watu kama huna mtaji na ndio unaenda kuanza kabisa.

lengo langu ni kiviwekea vyama vya siasa vikwazo vya kijeshi ni nguzo muhimu katika kudumisha amani.
 
Back
Top Bottom