Record ya Simba kwa magoli chini ya Sven yaifunika Yanga

Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,282
3,077
SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameweka rekodi ya kuongoza kikosi hicho kufunga mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu 2019/20 akiwa ameongoza kwenye jumla ya mechi 11, alishinda 9, sare moja na kupoteza mchezo mmoja.

Katika mechi hizo 11 Sven ameshuhudia kikosi chake kikifungwa mabao 8 na kufunga jumla ya mabao 26 ambayo ni mengi kuliko yale ya Yanga ambayo imecheza mechi 19 na imefunga mabao 24.

Alianza kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli ambapo mechi ya kwanza alishinda mabao 4-0, KMC 0-2 Simba, Simba 2-0 Ndanda, Simba 2-2 Yanga, Alliance 1-4 Simba, Simba 2-1 Mbao, Simba 3-2 Namungo, Simba 2-0 Coastal Union, Simba 2-1 Polisi Tanzania, Simba 0-1 JKT Tanzania, Mtibwa 0-3 Simba.

Sven alisema kuwa kinachoipa ushindi timu yake ni juhudi za wachezaji kupambana ndani ya uwanja.Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na jumla ya pointi 53 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Lipuli .

CC @ Saleh Jembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nikisema haya masimba mapumbavu nakosea?
Shida nn mkuu?
FB_IMG_15814497531187856.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwanini mashabiki wa Simba walikuwa wanamlilia Uchebe, wakati kumbe Simba ya Sven yupo kwenye mwenendo mzuri tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Walikua sahihi kwa sababu walikua wanaona wachezaji wanacheza kwa kujituma ila wanashinda kwa kutumia ubora walionao kulingana na wachezaji wa timu pinzani,
Na anayestahili kulaumiwa kutojituma wachezaji ni kocha.
Sven toka amekuja Simba haijawahi shinda kwa goli moja, ni mbeli kuendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na bado team malalamiko watalalamika sana tunampango wakufunga goli nyingi tuwagawie vyura kila mchezaji sita
 
Nasikia CHURA wameshindwa ku post wishes za VALENTINE kisa ni rangi nyekundu.
 
Back
Top Bottom