Bale still the same, alikuwa anakimbia na mpira at the end pasi hajui anampa nani. Cristiano mipira ilikuwa inamgonga tu, watu wanachukua ye anashika kiuno. Jesé alikuwa anatimua mbio bila mpira. Kroos na Modric walicheza vipindi tofauti lakini wana akili timamu. Watoto wadogo wengine tuwape japo game mbili ili tuwatathmini vizuri lakini bado sioni sababu ya Illara kuwepo uwanjani. Marcelo alicheza vizuri kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili nyota alikuwa Isco. Ukiondoa Arbeloa, beki nyingine zote zimetulia. Nashindwa kuelezea mchezo, lakini ndio hivyo lazima waletwe watu wenye akili pale. Navas akipewa play time msimu huu, De Gea akae huko huko aliko.