RC Kafulila anafanya kazi Simiyu

RC Kafulila anafanya kazi Simiyu

Vmatongo

Senior Member
Joined
Dec 8, 2021
Posts
158
Reaction score
240
Mkoa wa Simiyu ni moja kati ya mikoa ambayo inajishughulisha zaidi na kilimo pamoja na ufugaji. Hasa kilimo cha Pamba sasa ivi pia wanalima Alizeti.
Kwa miaka mingi kilimo cha pamba mkoani Simiyu badala kuwa mkombozi kiligeuka kuwa kilio hasa pale mkulima anapovuna mazao yake toka shambani ndio mirija ya unyonyaji inapoanza kuchomekwa mwili mzima!

Amcos walikuwa wanapanga kila kitu ikiwa ni pamoja na bei ambayo haikidhi ghalama za uzalishaji. Lakini wao walikuwa wanajilipa mabilioni ya hela huku hawazalishi wala hawawsaidii wakulima si pembejeo wala ushauri hao jamaa utawaona kwenye manunuzi huku wakichezesha bei kama wanavyotaka ili kuwaibia wakulima.
Na kwa sababu ya kuiba ilikuwa wanawakopa wakulima ili wao wauze kwa bei nzuri kwenye Makampuni na wanapata faida baadaye wanamlipa mkulima kidogo sana ulikuwa wizi wa wazi kabisa.
Sasa tunashukuru ujio wa kafulila hii biashara ya utapeli kutoka kwa hao jamaa wanaojiita Amcos imefika mwisho baada ya kuintroduce Simiyu model ambayo sasa mkulima anachagua auze pamba yake wapi tena bila mkopo ni kwa cash. Hawa amcos na wenyewe ni wanunuzi kama wengine na wanagombea kupata pamba na wanlipa hela taslim na hawakopi tena, Kafulila amezuia mambo ya ukopaji.

Baada ya kupita miaka mingi mkulima anauza pamba yake bila mkopo hii peke yake ni mafanikio makubwa sana, ukiachilia mbali suala la bei ambayo ipo juu kwa sasa kuliko kipindi kingine chochote! Kuna mafanikio mengi kwenye kilimo hiki cha Pamba ambayo Kafulila ameyaleta.

Kama ataendelea kubaki katika mkoa huu ingawa najua fitina kwa huyu kijana ni nyingi tutaona mabadiliko makubwa katika mkoa wetu wa Simiyu hasa hasa huu ujinga wa dawa feki ambazo haziuwi wadudu wa pamba. Tunategemea uzalishaji zaidi miaka miwili inayokuja. Tutavunja rekodi.
 
Hongera zake ,usajili wake unazaa matunda .
 
Back
Top Bottom