RASMI: Mashtaka dhidi ya Mitandao ya Simu kutokana na Wizi na athari wanazonisababishia

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,095
2,429
wadau mara nyingi nimekuwa nikitoa malalamiko kuhusiana makampuni ya simu kwao binafsi na pia hata kwenye jamii kwa ujumla.na kushangaa kwa nini TCRA imeshindwa kutulinda sisi wateja na kuacha tunanyanyaswa na kuonewa kama vile tumekosa mtu wa kutusimamia.sijafahamu kama serikali inalitambua hili au imeamua kupuuzia. malalamiko yangu yamekuwa katika maeneo makuu mawili.
1. Makampuni ya simu yamekuwa yakiniibia sana mimi mteja wao kwa kuniunga katika Huduma ambazo mimi sikuwahi kuziomba hata kwa bahati mbaya. nina ushahidi wa meseji zao nyingi wakinitumia ujumbe kuwa wameniunga kwenye huduma flani na kuwa watanikata kiasi flani cha pesa kila siku. HUU NI WIZI. nimekuwa hata nikiuliza wanihakikishie ni lini nimejiunga hiyo huduma na wamekuwa wakikiri kuwa hawana ushahidi sababu ni kweli sijajiunga.

2. Makampuni ya simu yamekuwa yakinisababishia usumbufu na privacy harassment kwa kiasi kikubwa sana. mara kadhaa inaonekana wanagawa namba yangu kwa watu ambao wanaitumia kujitangaza au kutangaza bidhaa zao bila idhini yangu. tunafahamu kuwa matangazo huwa yanalipiwa je mimi nafaidika na nini namba yangu kutumika nao kuwafanyia watu wengine matangazo? HUU NI WIZI na USUMBUFU mkubwa hasa napokuwa nimepumzika au nafanya kazi nyingine na wao wananitumia text kutangaza mambo ambayo mimi siyahitaji.

3. Makampuni ya simu yamekuwa yakinilazimisha nibadili DINI yangu. KATIBA YETU INARUHUSU UHURU WA KUABUDU. wao wananitumia text kuhusiana na dini ambayo si yangu wakinitaka nitumiwe mistari ya vitabu vya dini husika na pia mafundisho. hili ni kinyume na Imani yangu ambayo hawaijui. hapa wameingilia uhuru wangu na kunishinikiza kubadili Dini au kuni hubiria dini ambayo si yangu.

4. USUMBUFU NA KUINGILIA UTULIVU WANGU. mara kadhaa makampuni ya simu yamekuwa yakinipigia simu kutaka kuniambia huduma zao ilhali mimi sipo interested nazo.kama ningetaka kuzijua ningepiga customer care/service kuulizia. wanaponipigia muda ambao nimelala, nimepumzika wananiharibia utulivu hasa kwa mimi ambaye nina tatizo la kupata usingizi.sasa ninapoamshwa na simu ambayo kwangu si muhimu najikuta naanza kupata shida ya kupata tena usingizi na kunisababishia maumivu ya kichwa. lakin pia wanapopiga simu muda wa kazi ambao tunapaswa kuwa busy kulijenga taifa na kazi zangu zinahitaji utulivu mkubwa wa kiakili wanafanya mental disturbance na hivyo hili limeanza kuwa athari kwangu sababu mara kadhaa nasahau ambacho nilipaswa nifanye sababu ya kukatishwa na hizi simu zao na texts zao

WITO:
Wadau tushirikiane katika hili nazidi kukusanya idadi ya watu ambao tutaenda mahakamani pamoja so soon kushtaki na pia naonana na wanasheria kadhaa mpaka sasa nimepata mmoja ambaye yupo tayari nahitaji pia kama kuna mwanasheria mwingine humu ndani tuwasiliane ili hatimaye tuweze kusaidiwa tatizo hili kubwa ambalo inaonekana TCRA wameamua kulifumbia macho.

naomba tuwasiliane zaidi na wanasheria mbali mbali,wadau na wote wenye kupenda kuheshimiwa kwa privacy zao na pia kupeana maoni na ushauri.
 
Pole sana kwa Usumbufu ila upuuzi wa haya makampuni unakuja baada ya usingizi wa TCRA.

Siku ikiguswa itaguswa kweli JPM hajalala.
 
Back
Top Bottom