Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,677
- 22,946

Raisi Erdogan akiwa na mkewe baada ya upigaji kura ya maoni.
Raisi Recep Tayyip Erdogan siku ya jumapili alishinda kura ya maoni ambayo aliiitisha ili kuomba ridhaa ya wananchi wa Uturuki kuongoza nchi hiyo kwa kihula mingine miwili.
Hata hiyo matokeo ya kura hiyo yametiliwa shaka kubwa na vyama vya upinzani vkidai kuwa tume ya uchaguzi ya YSK imevuruga matokeo ili kumpa ushindi raisi Erdogan.
Ushindi wa Erdogan umekuja ukiwa ni mwembamba mno na kuashiria mgawanyiko mkubwa kati ya wananchi wa taifa la Uturuki.
Serikali ya raisi Erdogan imepania kuendelea na marekebisho ya katiba ya nchi hiyo ili kuipa uwezo wa kuendelea na mipango yake na raisi Erdogan atakaribishwa kwenye chama kinachotawala nchi hiyo cha AK.
Ndani ya katiba ilokuwepo kulikuwa na kipangele kilichokuwa kikimtaka raisi aliepo madarakani kuacha kujishirikisha na chama chochote cha siasa na pia ilimtaka raisi kutokuwa na upendeleo.
Mpaka sasa wapinzani wa raisi Erdogan wanapinga matokeo ya kura hiyo ya maoni lakini kuna dalili kwamba itakuwa ni vigumu sana kuweza kubadili matokeo hayo, jambo ambalo litaonyesha mgawanyiko mkubwa wa wananchi wa Uturuki.
Moja ya sababu za kupinga upigaji kura hizo za maoni ni kitedo cha wasimamizi wa vituo vya kupiga kura ambao wanadhaniwa kwamba kwa makusudi waliwahadaa wananchi kutumia karatasi za kupigia kura zisizo na mihuri jambo linaloashiria ukiukwaji mkubwa wa sharia zinazoongoza upigaji kura.
Idadi rasmi ya kadi ngapi za kupigia kura zisizo na mihuri haikujulikana na kwamba je tume ya uchaguzi YSK iliamuru kwamba ni kadi ngapi zitumike katika dakika za mwisho. lakini tume hiyo ikaridhia matumizi ya kadi hizo baada ya ombi la chama cha APK.
Matokeo haya pia yamezua masuali mengi kutoka kwa nchi za jumuiya ya Ulaya ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikiiandaa Uturuki kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya hiyo.
Siku ya Jumapili tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa raisi Erdogan amefanikiwa katika kura ya maoni kwa asilimia 54.1 ya kura zote za ndiyo zilizopigwa.
Kura hii ya maoni imepigwa kabla ya uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2019, na unaifanya Uturuki kuwa nchi inayofanana katika utawala wa aina ya jamhuri baada ya Ufaransa na Marekani.
Raisi wa Marekani Donald Trump ametuma salamu za pongezi kwa raisi Erdogan kinyume na viongozi wa mataifa mengine ya magharibi.
Baadhi ya mabadiliko ya katiba ya Uturuki yataanza kufanyika mwezi Novemba mwaka 2019 ambapo bunge la nchi hiyo halitapata nafasi ya kudhibiti shughuli za serikali na mipango yake na pia ofisi ya waziri mkuu itaondolewa.
Pia raisi atakuwa na sauti Zaidi katika kuteua majaji 12 kati ya 15 wa mahakama kuu, kupanga bajeti kutokana na anavyoona na pia kurejea katika chama chake cha kisiasa.

Wananchi wakionyesha kummunga mkono raisi Erdogan.
Miji mkuu ya Uturuki ya Ankara, Istanbul na Izmir imepiga kura ya Hapana wakati majimbo ya mashariki ambako kuna wafungwa wengi wa kisiasa ambao wanashirikiana na wananchi wa kabila la wakurd ambao ni wachache nao wamepiga kura ya Hapana.
Hii inamaanisha nini kwa Uturuki?
Wale wanaounga mkono kura ya maoni wanaamini kwamba raisi Erdogan amepewa uwezo mkubwa na serikali yake itakuwa na uwezo wa kupambana na tishio la ugaidi, vurugu katika nchi jirani ya Syria na matishio ya ndani kama majaribio ya mapinduzi.
Wapinzani wao wanaamini kwamba kitendo hiki kimeua demokrasia na raisi hawezi kudhibitiwa.
Hata hivyo pande zote mbili zinaamini kwamba Bunge la nchi hiyo limeondolewa uwezo wake wa kumdhibiti raisi hata pale anapokuwa anataka kutekelkeza majukumu ambayo anaona ni kwa maslahi ya nchi.
Je, wapinzani wanaweza kubadilisha matokeo?
Jibu ni kwamba itakuwa ni vigumu.
Tume ya uchaguzi tayari imetangaza matokeo ya kura ya maoni kwamba waloshinda kwa kura ya "Ndiyo" ni wengi asilimia 54.1
Wapinzani wana uwezo wa kuandamana mitaani kupinga ushindi huo lakini wanafikiria upande wa pili wa hatua ya serikali itakayochukua dhidi yao.
Je, Uturuki itaendelea kushirikiana na umoja wa Ulaya?
Jibu ni ndiyo, na hata baada ya raisi Erdogan kuwashutumu viongozi wa jumuiya ya Ulaya kwamba wana tabia kama ya wanazi wa kijerumani , lakini bado milango ya majadiliano ipo wazi na tangu kura ya jumapili ipigwe kumekuwepo na dalili ya kupoa kwa mashutumu toka kila upande.
Vipi kuhusu Uturuki na uanachama wake NATO?
Uhusiano wa Uturuki ndani NATO upo zaidi na Marekani ambayo siku zote inahitaji ushirikiano wa Uturuki dhidi ya vita vya kuwatokomeza magaidi wa ISIS.
Na ndiyo maana raisi Donald Trump amekuwa wa kwanza kumtumia salama za pongezi raisi Erdogan.
Lakini Marekani bado haipendezwi na kampeni ya uturuki dhidi ya wanamgambo wa kikurdi ambao wanashirikiana na Marekani katika vita na ISIS kwa kusafisha njia ya vita.
Chanzo: Vyombo mbalimbali vya kimataifa.