Raisi Donald Trump kuzitembelea idara nyeti aanza na makao makuu ya CIA leo.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
15,502
22,355
ad_232186973-e1484935205158.jpg


Raisi wa 45 wa Marekani Donald Trump leo pamoja na shughuli zingine anatarajiwa kufanya ziara kwenye makao makuu ya shirika la ujasusi la Marekani la CIA yaliyoko mjini Langaley katika jimbo la Virginia.

Tayari CIA inaye mkurugenzi mpya bwana Michael Pompeo ambae anatarajiwa kuapishwa na bunge la Marekani.

Kitendo cha raisi Trump kutembelea idara hiyo ya ujasusi ni katika kuonyesha mshikamano kati ya taasisi ya uraisi na idara hiyo khasa baada ya kashfa ya Russia kutuhumiwa kuingilia mawasiliano na pia baada ya vita ya maneno kati ya timu ya raisi Trump na mkurugenzi alieondoka bwana John Brennan.

Ziara hii ni moja ya mfululizo wa ziara za raisi Trump kutembelea idara na taasisi mbalimbali nyeti za serikali kujitambulisha rasmi kuwa yeye ndiye amiri jeshi mkuu.

cia_getty.jpg


Baada ya uchaguzi wa urasi nchini humo, baadhi ya viongozi wa CIA walitoa taarifa za kuihusisha nchi ya Russia na uingiliaji wa harakati za uchaguzi nchini marekani ambapo kwa kiasi fulani kitendo hicho kilionekana kumsaidia bwana Donald Trump na kumpa ushindi.

Raisi Trump tayari amewaagiza majenerali wa jeshi la nchi hiyo kuandaa mpango wa namna ya kulishughulikia suala la ugaidi unaohusishwa na kundi la ISIS katika nchi za mashariki ya mbali pamoja na ule unaofanywa katika nchi zilizoendelea, Marekani na barani Ulaya.

Raisi Trump amewapa majenerali hao siku 30 kuhakikisha wanakuja na mpango madhubiti ambao utaifuta kabisa taasisi hiyo ya ugaidi duniani.

Kundi la ISIS limekuwa likielekeza sana mashambulizi yake katika nchi mbalimbali duniani huku nchini Syria likishindwa vibaya katika vita yake na majeshi ya serikli ambayo yamekuwa yakisaidiwa na Russia, Iran na Hezbolah.

Katika kuonyesha kwamba analichukulia suala la usalama kwa uzito wake, raisi Trump tayari aliwateua majenerali wastaafu bwana Marine generals James au “Mad Dog” Mattis na John Kelly kuongoza wizara ya ulinzi na ile ya mambo ya ndani.

Bwana Kelly ataongoza wizara ya mambo ya ndani au "Homeland Security" yenye watumishi wapatao 240,000 wakiwemo maofisa wa mipakani, askari kanzu, na maofisa wanashughulika na kuwaondoa raia waso na hati za makazi nchini humo au "undocumented migrants".

Wengine ni majenerali Michael Flynn ambae anakuwa mshauri wa usalama wa taifa na jenerali Keith Kellogg ambae anakuwa mnadhimu mkuu wa baraza la usalama la Marekani.

Katika hatua ingine raisi Donald Trump amesaini tamko la kuifanya tarehe 9 September 2011 kuwa ni siku ya mashujaa wa nchi hiyo yaani National Day of Patriotism.
 
Back
Top Bottom