Diranqw
Senior Member
- Mar 13, 2016
- 160
- 72
Napenda nitumie jukwaa letu kutoa ushauri mdogo kwa Dr.Magu-Rais wangu;ni vizuri kuwa makini na wasaidizi wako hasa wanaokushauri kwenye utekelezaji wa majukumu yako ili wasije wakakufedhehesha mf.kwenye uteuzi wako wa wakuu wa mikoa najua pamoja na hatua ya haraka uliyochukua nakupongeza sana lakini bado nina wasiwasi mkubwa kwa baadhi yao kuhusu dhamiri zao katika kushughulikia changamoto za jamii yetu tazama maeneo ya huduma kama hospitalini,barabara,kilimo,utendaji wa baadhi ya viongozi wa umma naona kama kuna kamchezo fulani wa kukuhadaa wewe na sisi wananchi fuatilia utaona na kuelewa vizuri.
Vivyo hivyo kwa wakuu wa wilaya wengi wao ambao kwa sasa wanajikosha kama vile ni wazuri kwenye usimamizi lakini kabla ya hapo tunawafahamu utendaji wao na dhamiri zao. Kabla ya uteuzi wao ni vizuri vyombo vyako unavyo viamini wafuatilie nyendo zao na kujua usafi wao na umahiri wao, wengi wao sasa hivi wanatumia vyombo vya habari waonekane udanganyike uwarudishe.
Chonde chonde rais wangu najua unaweza, wengine wako hapo kukukwamisha na kukuchafua uwe makini nao.
Kila la kheri kaza buti sisi wananchi tuko nyuma yako!