Rais wangu Magufuli ni lini utalihutubia Taifa?

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
5,457
16,671
Pengine utakuwa umebanwa na namna ya kutengeneza mfumo wako kwa muda wa miezi miwili na ushee sasa, lakini sidhani kama utakuwa umebanwa kias cha kushindwa kulihutubia taifa kujua mwelekeo wa serikali yako, kwani tayari umeshalihutubia bunge, umehutubia wafanyabiashara, bado hujazungumza na sisi wananchi wa kawaida ambao wapo waliokupigia kura na waliompigia mpinzani wako mkuu ndg Lowassa... muhimu ni hotuba yako ya kuliunganisha taifa liliogawanyika vyakutosha kipindi cha uchaguzi ......
Kuna masuala yakiachwa bila kuyatolea maelezo sidhani kama ni unungwana...

Kwamfano;
1. Je ni kweli kuwa maamuzi ya mawaziri wako yanafuata maagizo yako au mwelekeo wa serikali unayoitaka au ni utashi wa mawaziri wenyewe, vitu kama kubomolea wananchi nyumba, Kodi, Elimu, Kazi hadi usiku wa manane nk?
2. Je ni kweli kwamba wewe unapendelea team ushindi ya chama chako katika teuzi mbali mbali na wala hujali kwamba kwenye siasa kuna watakaokuunga mkono na watakao kukataa...? mfano kama baadhi ya teuzi zako ziliangalia uadilifu, iweje waliotajwa kwenye kashfa za Escrow, ununuzi wa mabehewa fake ya train wakawemo?

3. Pamoja na ahadi yako lya elimu bure hadi kidato cha nne, je unafahamu ukweli kwamba tatizo la elimu ya Tanzania haijawahi kuwa ada pekee? na ndio maana wapo wazazi wanaopeleka watoto wao shule hadi za mil 40 kwa mwaka na zipo hapa Tanzania?

4. Vipi muelekeo wa serikali yako kuhusu upatikanaji wa maji salama ya kunywa mijini na vijijini? Kwamba pamoja na ukubwa wa miji kama Dar es salaam hatuna hifadhi(Reserve) ya maji safi? Juzi tumemuona Rais mstaafu akikagua mradi wa maji tukaambiwa anasaidia kutekeleza ilani ya CCM.... yeye ni Mwenyekiti wa CCM mradi wa maji ni wa watanzania wote, CCM ina shule na miradi mingine, anatoka wapi kukagua miradi ya walipakodi kwa kisingizio cha chama.... nini kinaendelea?

5. Wananchi pia tunataka kujua mrejesho wa waliokwepa kodi bandarini, hatua stahiki ulizoahidi zimefikia wapi?

6. Uliahid utatengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wadogo, lakini hadi sasa mawaziri wanaendelea na ziara za kushtukiza maofisini, ni lini wataweka mipango ya kuwainua watu hao?
7. Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, waziri bado anazungunka na ziara za kushtukiza vingu nguti, tungejua muelekeo wako katika kutumia mtaji wa rasilimali watu na hasa vijana kataka kuendeleza kilimo ikiwemo mirad mikubwa ya umwagiliaji na kilimo cha kisasa.....

8. Kwanini viongozi wengi walio chini yako wanataka kutuaminisha kwenye ziara za kushtukiza, je una mikakati yeyote ya kuweka mfumo thabiti wa utumishi na uwajibikaji wa pamoja?

9. Masuala makubwa ya afya bado hayajajibiwa, bado mawaziri wanashtukiza, kwasasa wanajadiliana na waganga wa kienjeji.... angalao hili la msd kuweka maduka hospitali limesaidia kwa kias.. lakin vip bima ya afya kwa kila mwananchi? mkakati wa kupanua kada hii ya afya na kuhakikisha kila chuo kinadahili wanafunzi wengi zaid ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi yao?

10. Elimu ya juu imefanywa siasa kubwa na wengi wa wanasiasa wanaogopa kuizungumzia kiuhalisia, hivi kwanini hatuwekezi kwenye elimu ya ufundi? vyuo vyote vya ufundi nchini kwa sasa vinataka kutoa degree hata kama hakuna phd holder hata mmoja, nini muelekeo wako kwa mambo hayo?

11. Kuna hili la chuki, kulipa visas na kuwabagua waliokunyima kura...... linaanza kudhihirika taratibu, na sasa tayari mlinzi wa mpinzani wako ameshafutwa kazi(Kwa sababu yeyote ile) Huoni kama inawathibitishia wanaokudhania hivyo kuwa ni kweli?

Rais wangu Magufuli ulianza vizuri, wapo watu binafsi, wafanyabiashara, wawekezaji, wanafunzi, wakulima, wafanyakazi,wahamiaji nk. wanapenda kujua mustakabali na rais wao kwa sasa ili nao waendane na spidi ulioanza nayo, hudhani kwamba ni muda pekee wa kulihutubia taifa sasa kuondoa hizo sintofahamu?
 
Mzee wa sitowaangusha alizani ikulu ni boxing room akaanza kupiga ma pushup mikutanoni ngoja ataomba pooo mwenyewe
 
Kuna hadithi ambayo sina uhakika na ukweli wake lakini inafunzo muhimu kuhusiana na maada.

Wachina walimpa Nyerere taarifa ya mradi wa kujenga TAZARA wakati huo. Ilikuwa na kurasa tano tu. Inasemekana Mwl. alistuka kupata taarifa fupi kiasi hicho. Ndipo wachina wakamuuliza, unataka report au reli?

Nasi tujiulize kama tunataka matunda au hotuba kwa Magufuli.
 
#wise and ideological comment
 
Nchi haingozwi kwa hotuba,kama umeshindwa hotuba za bungeni na kwa wafanyabiashara,basihutamuelewa JPM milele
 
Nchi haingozwi kwa hotuba,kama umeshindwa hotuba za bungeni na kwa wafanyabiashara,basihutamuelewa JPM milele
Kabisa. Zile hotuba zina maelezo ya kutosha kuhusu mtazamo na mwelekeo wa Magufuli. Kilichobaki ni utekelezaji tu.
 
Rais aliwaambia hapa kazi tu, wao wakifikiri kazi inajumuisha na hotuba ndefu zilizojaa ngonjera na mipasho. Ngosha sio mwanasiasa ni mwanasayansi. Hana muda wa blah blah. Baada ya makatibu wakuu kuapishwa wakaambiwa wale kiapo cha uaminifu cha pamoja, na wakaambiwa asiyekuwa tayari kuapa basi akae pembeni. Matendo ya Ngosha ni hotuba tosha, hahitaji maongezi mengi yatakayowapa watu kick za kutokea kwa kuita waandishi wa habari na kuanza kuikosoa hotuba ya rais. Huyu sio rafiki wa wanaharakati wanaotafuta sababu za press conference.
 
Kwahiyo mkuu unadhani marais wote duniani wanahutubia mataifa yao kwakuwa wanapenda bla bla? Magu ni mwanasayansi wenye uzoefu wa miaka mingapi kwenye fani yake? Phd yake ya chemia ameifanyia kazi lini?
 
Waulize watanzania PHD imefanyiwa kazi lini waulize waliompa kura milioni 8, wao wanajua lini imefanyiwa kazi. Hotuba nyingi hazina mpango kama utekelezaji ni mbovu. Aliyepita alikuwa anahutubia bunge mpaka wabunge wanaanza kusinzia, lakini makontena mangapi yametoka nje ya bandari bila ya kulipiwa ushuru?. Watu wanataka kazi na sio kupoteza muda kwenye siasa za kulihutubia Taifa. Uadilifu ni muhimu kuliko mbwembwe za hotuba.
 
Kuna hadithi ambayo sina uhakika na ukweli wake lakini inafunzo muhimu kuhusiana na maada.

Wachina walimpa Nyerere taarifa ya mradi wa kujenga TAZARA wakati huo. Ilikuwa na kurasa tano tu. Inasemekana Mwl. alistuka kupata taarifa fupi kiasi hicho. Ndipo wachina wakamuuliza, unataka report au reli?

Nasi tujiulize kama tunataka matunda au hotuba kwa Magufuli.
Mkuu una point lakini kwenye scenario na mazingira tofauti sana.
Hotuba ya rais ni tofauti na taarifa ya mradi........ hotuba za rais hata iwe ya dk kumi, itasaidia sana kuondoa sintofahamu iliyopo........
 
Hotuba ipo ataitoa pindi atakapomalizia kuwateua wakuu wa mikoa na wilaya msihofu
 
Back
Top Bottom