Rais wa Mexico Pena Nieto akataa agizo la Donald Trump

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
[HASHTAG]#KIMATAIFA[/HASHTAG]:Mvutano umeibuka baina ya Mexico na Marekani baada ya Rais Donald Trump kutoa agizo la kujengwa ukuta mpakani mwa nchi hizo mbili ili kuzuia wahamiaji haramu na kuitaka nchi ya Mexico kulipia ukuta huo.
Kufuatia kauli hiyo Rais wa Mexico Pena Nieto amepinga vikali kauli hiyo na kusema kuwa Mexico haitalipia ukuta huo.
ITV
9704dc12222ad014a64ec4188f2b1156.jpg
 
Mwambie Trump aache ujinga,yeye ndiye anayeuhitaji huo ukuta hivyo agharamie.
Tena umweleze kuwa hapa Tz tuna cement za kutosha maana Dangote anazalisha nyingi sana na ana magari kabisa ya kusafirishia/kusambazia.
 
Mexco ni nchi maskini. Idea ya Trump ya kujenga ukuta ni kuilinda America dhidi ya watu kuingia kiholela ndani ya nchi hiyo kupitia ama kutoka Mexco.

Ukiangalia mara nyingi watu wanaoingia kupitia mexico ni kwa ajli ya kutafuta maisha ndani ya Marekani na hivi karibuni jaribio la magaidi kutumia mwanya huo pia kuingia America. Sina uhakika wa namna gani Mexico inaathirika na watu wake kuondoka na kwenda Marekani kwa njia za uchochoro kiasi kwamba iingie gharama ya kujenga ukuta.

Sioni kama kuan significant flow ya watu kutoka America kuingia Mexico kwa njia za panya na madhara yake kwa mexico hayako wazi.

Kwa sababu ukuta huu unaonekana kubeba maslahi mapana ya usalama wa Marekani, ninadhani ni busara nzuri America ikagharimia ujenzi huo, kwa kuw aunaonekana na muhimu zaidi kwa Marekani kwa sasa kulilko Mexico.
 


Huyu ni Rais mstaafu Wa Mexico naona uzalendo umemshinda kaamua kutema nyongo....

Amesema Mexico haiwezi kulipia upumbavu kupoteza pesa za walipa kodi.......

Amesema Marekani wakiweka kodi ya 20% ili kulipia ukuta na Mexico wataongeza kodi kwenye makampuni ya marekani yanayouza hasa magari nchini Mexico ambayo yameajiri Wa marekani milioni 10 ndani tu ya Marekani........

Ameongeza "Trump is the mad President and Mexico will never pay for fucking wall"
 
Yeye ni mtaafu tu, au katiba yao inampa veto rais mstaafu dhidi ya aliye madarakani!? Ingekuwa vema tumsikie rais wa Mexico aliye madarakani kwa sasa.
 
Yeye ni mtaafu tu, au katiba yao inampa veto rais mstaafu dhidi ya aliye madarakani!? Ingekuwa vema tumsikie rais wa Mexico aliye madarakani kwa sasa.
Mbona hata huyo aliyopo ameshasema kuwa hafanyi ujinga huo??"kuwa wewe usiyetaka watoto wa jirani waje kudoea kwako ndio ujenge ukuta sio mimi maskini ndio nifanye kazi ya kuwazuia"
 
Hakika Trump ataongeza maadui wengi sana kwa Marekani na ataiharibu kabisa.............
 
TRUMP kaisha andaa namna ya wao kuchangia automatically, bidhaa zote wanazoinport kutoka mexico zitaongezwa kodi ya asilimia kadhaa. Pesa hiyo itatumika kujengea ukuta mkuu
 
Unanikumbusha ule mgogoro wetu na Malawi,idea km hii ingeweza kutumika km pangekua nchi kavu
 
Ni bora wachimbe mfereji wafuge samaki pumbav zao..alaf trump nae wa zamani....kama anaona vp ....awaombe wachina wamsaidie kutengeneza electronic wall
 
Mwambie Trump aache ujinga,yeye ndiye anayeuhitaji huo ukuta hivyo agharamie.
Tena umweleze kuwa hapa Tz tuna cement za kutosha maana Dangote anazalisha nyingi sana na ana magari kabisa ya kusafirishia/kusambazia.
Ha ha ha dangote anasafirisha kwa magari hadi mpakani mwa USA na Mexico?
 
Back
Top Bottom