Rais wa Korea Kasikazini amwapisha mwanaye wa miaka 9 kuwa luteni wa jeshi

Kaputula La Marx

JF-Expert Member
Mar 28, 2015
562
494
Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini Amemuapisha Mwanae Wa Kiume Kim Lau Jong Un II Mwenye Umri Wa Miaka 9 Kuwa Luteni Wa Jeshi La Nchi Hiyo Yakiwa Ni Maandalizi Ya Kumuandaa Kijeshi Mtoto Huyo Ili Baadae Awe Mkuu Wa Majeshi Wa Nchi Hiyo.

Kabla Ya Kuapishwa Kim Lau Jong Un II amepitia mafunzo ya kijeshi akiwa na umri wa Miaka 7 na kufaulu ngazi ya ofisa wa Jeshi. Mtoto huyo hajasoma Elimu ya shule yeyote zaidi ya Elimu ya kijeshi.

Kim Lau Jong Un II anaweka historia ya kuwa Afisa Mwanajeshi Mwenye Umri Mdogo kuliko maofisa wote wa cheo cha Luteni jeshini Dunia Nzima.
9e6521faeb3562b1d6a1620788e1cd8c.jpg
 
Kwa nini majina ya hawa jamaa huanza na Kim badala ya kuishia na kim ikiwa ni jina la ukoo?
 
Mkiambiwa hili dikteta linatakiwa liondolewe mnaleta utetezi wa kijinga. Sadam, Qadafi, et. al wote walikuwa na ujinga huo; kuwarithisha watoto nafasi muhimu za nchi. Ile sio nchi ya kifalme; just one family imeamua kuwageuza mamilioni mandondocha. Majenerali wanauwa kinyama just kwa hisia tu; leo anampromote mwanae anayenyonya kuwa afisa wa jeshi. Ni zaidi ya matusi kwa wananchi ila ndio hivyo wafanyeje maana wako utumwani.
 
Yaani kwa akili yake ndio anamuandaa actually amemtangaza rasmi huyo mtoto just in case of anything endapo vita itazuka au akiuwawa kwa namna yoyote ameshawachagulia wakorea mtawala. Huyo mtoto atafichwa balaa; huenda akaishi Kremlin kwa siri kubwa. Nchi gani inaendeshwa kwa hisia za mjinga mmoja?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Watu watakuja kuleta unafiki hapa ohhh long live North Korea wakati huku nyumbani kikitokea kitu kidogo tuu ohhh dikteta uchwara
 
Back
Top Bottom