Political Jurist
Senior Member
- Sep 6, 2021
- 143
- 120
RAIS SAMIA TUVUSHE,MATOKEO TUMEYAONA .
Na.Amon Nguma.
Uhai na uendelevu wa viumbe hai na jambo lolote lile Duniani halitegemei uzao tu au mwanzo wake bali ni uwezo mkubwa wa kulinda uhai wa kiumbe au jambo hilo, kulea na kuendeleza katika hatua zote za makuzi/maendeleo mpaka kufikia hatua ya ukuaji inayoweza kujisimamia au kijilinda ,kwa nyakati zote hizi ulinzi na malezi huwa ndio nguzo muhimu na ya kutegemewa ili kufikia malengo .
Waswahili husema kazi sio kuzaa tu lakini kulea pia ni muhimu ,kwamba kuanza jambo ni muhimu sana lakini kuliendeleza ili lilete manufaa au matokeo ndio kazi kubwa zaidi na si wote wawezao na ndio sababu ya matajiri kuwa wachache Duniani kwani sio kila jambo lililoanzishwa au linaloanzishwa hufikia malengo au huleta matokeo tarajiwa .
Jambo la Kihistoria la uzinduzi wa Safari za Treni za Mradi wa Reli ya Kisasa ( SGR) kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma pamoja na utekelezaji wa vipande vingine mpaka Kigoma na nje ya Nchi ni udhihirisho wa uwezo mkubwa wa kuanzisha jambo na kuliendeleza alionao Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan ,pongezi nyingi sana Mhe.Rais .
Zifuatazo ni sababu kwa uchache kwanini Rais Samia anastahili pongezi nyingi katika hatua hii -.
1).Sanjari na Mradi wa SGR Serikali chini ya Mhe.Rais Samia imeendeleza na kukamilisha Mradi mkubwa wa kimkakati wa Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere wa Rufiji(STIGLERS) ambao imetumika Takribani Trilioni Saba ambao pia ulikuwa katika hatua za awali za utekelezaji lakini nao umekamilika na kuanza kutumika,hii ni udhihirisho kuwa Mhe.Rais.Samia sio tu ana uwezo wa kulea na kuendeleza jambo moja bali mambo .
2). Pamoja na kazi kubwa katika SGR lakini ni kipindi hiki ambacho kumekuwa na mapinduzi makubwa katika sekta ya Kilimo ikiwemo miradi ya umwagiliaji ,utafiti ,wataalamu na Uwezeshaji kupitia BBT n.k lakini muhimu ni kupandisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka Bilioni 292 mwaka 2020/2021 mpaka Trilioni 1.2 mwaka 2024/2025 ,uwezo wa kufanya jambo zaidi ya moja kwa ukubwa ni sifa ya viongozi wanamapinduzi ,hongera sana Mhe.Rais.
3). Kutokana na ukubwa usio kifani wa Miradi hii na fedha nyingi ajabu zinazohitajika wakati wa utekelezaji wengi waliamini ni ama miradi ikwame au huduma za jamii ziende likizo ,lakini ukweli ni kwamba katika awamu hii kumekuwa na mapinduzi makubwa katika sekta ya afya ikihusisha ujenzi wa miundombinu ,usimikaji wa mitambo ya kisasa , ajira pamoja na uendelezaji wa wataalamu wa Sekta ya afya.
4). Wakati SGR na STIGLERS zikitekelezwa kwa ukubwa ni kipindi hichohicho ambacho sekta ya Elimu nayo imetendewa haki ,ujenzi wa madarasa zaidi ya 20,000 ,ujenzi wa shule za Mikoa za Wasichana Mikoa yote ,Elimu Bure kidato cha tano na sita ,nyongeza ya Bajeti ya Mikopo Elimu ya Juu na uzinduzi/uanzishaji wa mikopo kwa vyuo vya kati .
5). Aidha pamoja na Mradi wa SGR unaoigharimu Nchi zaidi ya Trilioni 20 ,Mradi wa Umeme zaidi ya Trilioni 7 ,miradi ya Barabara na viwanja vya ndege pamoja na miradi mingine ya ujenzi lakini Rais Samia ameendelea kutoa vibali vya ajira kila mwaka kwa miaka minne mfululizo, kuboresha huduma na kupunguza tatizo la ajira na mlundikano wa wahitimu waliokuwa mtaani kwa miaka mitano mfululizo,hili lisiposemwa basi mawe yatasema .Pongezi Mhe.Rais hakuna kilichobaki nyuma.
Katika kipindi kifupi cha uongozi wake ndio wakati ambao Taifa limefanya Sensa iliyogharimu mamia ya mabilioni ya Shilingi na imefanyika kwa ubora pamoja na miradi mengine mingi ambayo haijatajwa hapo juu .
Pongezi nyingi Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa kiongozi Mwanamikakati na Mwanamapinduzi na zaidi kwa kazi kubwa na nzuri ya mapinduzi ya kimaendeleo ulioifanya na unayoifanya kwa ubora na kila la kheri katika majukumu yako sasa na siku za usoni .
Mama tuvushe ,dhamiri ni njema na matokeo tunayaona . Matumaini yetu kwako ni makubwa zaidi ya jana .Kesho yetu ni njema kwa uweza wake Mwenyezi Mungu .
Kazi Iendelee
Amon Nguma
0620615659