Rais na RC, Jiji la Dar linahitaji taaluma si Siasa!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
17,005
20,423
IMG_20160321_063522.jpg
Leo imetimia kile kiitwacho uchaguzi wa marudio Zanzibar, mimi simshirika wa hicho, ninachoamini leo ilikuwa sensa ya chama cha siasa.

Sipo huko, leo naangazia mada tofauti kidogo, ndio maana siasa na demokrasia vinawambwa msalabani kwa gimbi la Tanganyika Yangu, fungeni na kuomba tufike salama, mfano wetu uwe Mynimar kwa San Su Ki.

Jana nimemsikiliza Paul C. Makonda mkuu wa mkoa wa Dar, nipongeze kwa kuthubutu, nampongeza kama Makonda kwa dhamiri yake, iwe na mafaa au iwe dhariri, nashawishika kumpongeza kwamaana hata shetani hufanya kazi tena kwa nguvu na bidii lakini kazi zake zote ni mbaya mbele za mwanadamu.

Ninukuu maneno ya Mwalimu Nyerere Mwaka 1984 katika hotuba yake ya muago wa kifo cha Edward Sokoine alisema,

"hatutamkumbuka sokoinne kwa kuwa alikuwa na akili sana maana hata shetan anaakili sana, hatutamkumbuka sokonne kwa kuwa alikuwa mchapakazi sana maana hata shetani ni mchapakazi sana ila tutamkumbuka kwa moyo wa upendo maana shetan hana moyo waupendo, tutamkubuka kwa moyo wauzalendo maana shetan siyo mzalendo"


Malengo na mipango ya kijana mwenzangu ama nikazie kwakusema MDOGO WANGU Makonda ni mizuri lakini ni hatari kwa jiji la Dar, ama ametumia wataalamu na wakampotosha ama ametumia utashi wake, na hapa naamini ni utashi wake tena wa kisiasa.

Kwamba polisi atakayepambana na Jambazi atapewa zawadi, hii ni nzuri, lakini nadharia ya kiusalama ni mbaya tena mbaya sana, huenda hajaitumia ofisi ya kitaalamu inayomzunguka kuomba ushauri kabla hajahadhiri. Katika medani inayozungukwa watu kubambikiwa kesi, kuuwa kwa raia kujichukulia sheria mkononi, na kubwa zaidi kauli za " Tumeriua jambazi ririkuwa rinapambana na porisi" zitadi katika jiji. Kijana mwenzangu Makonda, kaa na wataalamu wape nafasi wabuni mbinu na mikakati mipya ya kiusalama ndani ya jiji kuliko siasa ziongoze jiji, ni hatari.

Kwamba mtaa utakaofanya vizuri katika usafi utapewa zawadi yenye thamani ya milioni 20, hii nayo ni nzuri, nalazimika kukupongeza, lakini nasikitika kwamba hukuiangalia Dar, umetangaza mithiri unaiangalia pota tu. Tumia wataalamu wa mazingira waliojaa tele katika ofisi yako wakupe njia mbadala ya kuliweka jiji safi.

Makonda unafahamu vema wenyeviti wa mitaa/vijiji ndio viongozi wa kiserikali wasiolipwa posho hata senti tano nchini? Na zaidi ndio viongozi wa kiserikali wanaosuguana sana na raia huku chini? Ningekuwa ni mimi hata bila kuomba ushauri kwa wataalamu wangu, ningeliomba baraza la jiji chini ya Meya Isaac M. Charles litenga sehemu ya bajeti ili kuwalipa posho wenyeviti wa mitaa ya jiji, huku usafi ukitiliwa mkazo.

Muhimu zaidi jiji la Dar leo lilipofikia halipaswi kuongozwa kwa mfumo wa mkoa, Rais ikimpendeze na ningebahatika kumshauri, ningemshauri Jiji la Dar liundiwe kuwa WIZARA ya JIJI la Dar, liwe na Waziri atakayechaguliwa toka chama chenye madiwani wengi, liwe na katibu mkuu mtendaji, liwe na Mkurugenzi. Na liwe na idara za utendaji.

Majiji mengi barani afrika yamebadilika baada ya kuwa wabunifu kiutawala, na sio siasa, Jiji la Nairobi lilibadilika baada ya kuundiwa wizara, Jiji La Beijing, Jiji la Selous, Jiji la Rio De Janeiro,Jiji la St. Pertersberg, Jiji la Rome nk.

Bila hivi jiji litaendelea kuwa la vibaka na ujanjaujanja huku likiwa na muundo wa Sodoma na Gomora.
 
Kawaida yako kile chote kitokacho CCM nikulaum tu hata angefanya kama ulivyoandika ungekuja na criticize na kushauri afanye kama alivyosema jana.
Siasa hizi bana.....Kuna gazeti lilimtukana mzee mmoja hapa Tanzania kwa zaidi ya miaka saba mpaka mzee wa watu akawa ndo kipimo cha ushetani Tanzania.Haya bana...Siasa njema
 
Umeharibu ulipo kosoa na Kushauri wazi wazi hivi!Sasa kwa kuwa anataka aonekane yeye giniazi,huu Ushauri hauta Pokelewa...Ili wasije waka ambiwa kuwa nondo hizi wamezitoa kwa mwana Ukawa!
 
Kawaida yako kile chote kitokacho CCM nikulaum tu hata angefanya kama ulivyoandika ungekuja na criticize na kushauri afanye kama alivyosema jana.
Siasa hizi bana.....Kuna gazeti lilimtukana mzee mmoja hapa Tanzania kwa zaidi ya miaka saba mpaka mzee wa watu akawa ndo kipimo cha ushetani Tanzania.Haya bana...Siasa njema
Kwahiyo wewe huoni hoja bali mtoa hoja?
 
Alichonishangaza hata mimi ni kushindanisha wenyeviti wa mitaa yote bila kujali utofauti wa kipato,tofauti ya miundombinu baina ya mtaa au kata na kata,maeneo yaliyopimwa na yasiyopimwa pamoja na mazingira ya watu kwa ujumla kwenye mitaa ya jiji hili.

Kwa mfano,unawezeje kumlinganisha mwenyekiti wa mtaa wa Mnyamani ulioko Buguruni na mwenywkiti wa mtaa wa Mchafukoge hapa town Center au yule wa mtaa ulioko Masaki kwa vibosile?

Makonda yatamshinda tu siku si nyingi unleas akubali kushaurika.
 
Alichonishangaza hata mimi ni kushindanisha wenyeviti wa mitaa yote bila kujali utofauti wa kipato,tofauti ya miundombinu baina ya mtaa au kata na kata,maeneo yaliyopimwa na yasiyopimwa pamoja na mazingira ya watu kwa ujumla kwenye mitaa ya jiji hili.

Kwa mfano,unawezeje kumlinganisha mwenyekiti wa mtaa wa Mnyamani ulioko Buguruni na mwenywkiti wa mtaa wa Mchafukoge hapa town Center au yule wa mtaa ulioko Masaki kwa vibosile?

Makonda yatamshinda tu siku si nyingi.
Tunatakiwa kumsaidia na hii ndio njia ya kumsaidia
 
hamu ya ukawa ni kuona ccm inafeli lakini ajabu ni kua ccm inafanikiwa katika kila idara hapa nchini.
 
Dar inahitaji metropolitan independent organ,kama kampala wanayo y dar icwe? Pili kama kuna pexa za kuchezea kwa zawadi ni bora wawekez kwenye garbage collectors points kona zote za jiji na kulipa wazoa taka mitaani badala ya hiyo njia butu..ccm walishakata pumzi ya uwezo wa fikra za maendeleo,buree kabxa
 
Vijana wenzangu mna mawazo mazuri, tatizo ni kufungwa na minyororo ya vyama, tukiweza kulishinda hili tutashirikiana kuijenga nchi yetu
 
Back
Top Bottom