Rais mzuieni Makonda kabla raia wasio na hatia hawajaanza kupigwa risasi

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Nikiri kwamba huyu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameanza kunitia wasi wasi kuhusu baadhi ya maamuzi yake anayochukua.

Kwa mfano, katika hili la kumpa zawadi ya sh milioni moja askari atakayepambana na kulishinda jambazi, ni jambo la hatari sana tena sana. Maana ili ulishinde jambazi mara nyingi lazima ulipige risasi na uliue na ukiliua ushahidi mwingi utakuwa umejificha.

Kama kila kona kumekuwa na shutuma za askari wetu kuwabambikiza raia kesi za mauaji ili kujipatia hongo au kumkomoa mtu, hivi kwa kuahidiwa milioni moja watashindwaje kuwapiga risasi waendesha boda boda au mtu mwingine yeyote na kusingizia kwamba ni jambazi lililokuwa linawakimbia, maiti inaambatanishwa na gobole lililopatikana katika tukio jingine ili mradi tu kuipata hiyo milioni moja. Vinginevyo tukubaliane kwamba sasa Dsm imeruhusiwa yafanywe mauaji ya holela.

Nilidhani, kwa mawazo yangu kwamba kamanda Simon Sirro kwa uzoefu wake badala ya kukubaliana kirahisi rahisi na wazo hili la Makonda ambaye hana uzoefu na mambo haya alitakiwa kuiona hatari hii na kumshauri mapema.

Suala la polisi kupambana na kulishinda jambazi ni moja ya majukumu ya kazi yake na kitendo kinacholiongezea jeshi la polisi na askari husika sifa, si kitendo cha kuahidiwa zawadi.

Ningekubaliana na jambo hili kama zawadi hiyo angetangaziwa raia anayetoa taarifa kwa siri inayosaidia kukamatwa jambazi badala ya askari anayelishinda jambazi, tafsiri ya kushinda hapa ikiwa ni kuua.

Nashauri wasaidizi wa Rais, watu wa Usalama au mheshimiwa Rais mwenyewe walipime jambo hili na wampe maelekezo yaliyo salama zaidi mkuu wa mkoa badala ya kubaki kama lilivyo.
 
Mkuu naungana na ww.....hoja ya msingi kabisa na tunaona Dar ikienda kuwa eneo la hatari kuishi.......Makonda apunguze speed anapoelekea ni kuharibu wala sio kufanikisha.........walio karibu naye wanatakiwa kumpa ushauri zaidi.
 
Dili hili, nikiishiwa ada ya mwangu inglishi midia skuli naingia mtaa naua jambazi moja kisha ada inapatikana.
demu wangu akiniomba samsang galaksi mpya ya lakin 8, naingia mtaa naua jmbazi moja na chenchi inabaki ya kujipumzisha baa wiki endi.
Asante kondakta kwa fursa hii. Hapo ni mkuu wa mji wa dar es salaam tu, ungekuwa waziri wa mambo ya ndani naamini unge ahidi 10m kabisa kwa kichwa cha jambazi mmoja.

WABEJA BABA
 
Hao wanaoua na kuchukua mali za watu kila kukicha hao mbona hamuwalaani? Wezi wanajulikana ila nani ajitoe muhanga kupambana nao? Wee kaibe wakulime risasi kisha wakalipwe milioni yao.

Hata huyo jambazi haui ispokuwa ameahidiwa hela ndefu. Acha hela zirushiane risasi
 
hili linafanyika dunia nzima..hutokea hata mbwa kupewa zawadi kwa ujasiri katika mapambano..asishangae.
 
Tatizo sasa hivi kila mtu anajaribu kubuni kitu chake bila taratibu. Kupambana na ujambazi ni kazi za msingi za Polisi. Jeshi la Polisi lina taratibu zake za kuzawadia Askari. Ni vizuri asifanye majukumu ya kawaida ya Askari kuwa mambo ya kuzawadiwa labda kama kuna ujasiri usio mfano. RC Makonda anaweza kuwa na ubunifu lakini azungumze kwanza na wataalam ili kuepuka migongano.
RC Makonda anataka kuwaepa Madiwani na kufanya kazi na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa. Hili haliwezekani..
 
Polisi sasa naona mmeamua kupotoka kabisa. Yaani kazi yako uliyoisomea unakubali iingiliwe na wasioijua kisa kawa mkuu wa mkoa?? Shame on yu. Sasa wenye visa tu vya kipolisi si mtamalizana?? Jambazi hapigwi risasi 10 ili afe, hivyo hata mmoja tu akitwangwa ya kichwa tiyari milioni imeingia. Je, katika kikosi kilichotumwa kuwashughulikia mtajua ni nani kamtwanga? Hiyo milioni haitaleta chuki kwa walipwaji?? Hili jambo msilipuuzie nyie polisi litaja wakosti
 
Back
Top Bottom