Rais Mugabe asema atagombea urais hata akiwa marehemu

DAFU NA NDIMU

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,497
5,090
Wanajamvi habari zenu.

Robert Mgabe (92) Rais wa Zimbabwe, ametangaza nia ya kugombea tena kiti cha urais nchini humo. Mkewe (50+) amenukuliwa akisema mumewe ataiongoza Zimbabwe hadi atapokufa.

Mke huyo ameongeza kuwa yupo tayari kumsukuma mumewe kwenye kitoroli kokote aendako ilimradi tu aendelee kuwa Rais.

Mke huyo akasisitiza pia kuwa hata Mugabe akiwa maiti, wananchi wanapaswa kumpigia kura ili wamwenzi.

Source: Redio DW idhaa ya Kiswahili leo saa 7 mchana.

Najua raia wa Zimbabwe wataamua kumchagua Rais anayewafaa. Lakini habari hii imeniachia maswali mengi. Yafuatayo ni baadhi tu.
  1. Kwa nini viongozi wanakuwa ving'ang'anizi namna hii?
  2. Kwa nini wananchi wampigie kura maiti wakati kuna watu hai tena wenye nguvu na maono ya uongozi?
  3. Ikitokea maiti akatangazwa mshindi ataongozaje?
  4. Nchi zingine hasa zile zinayoongozwa na akina Bi.Kirembwe zikiamua kuiga mawazo hayo sijui itakuwaje?
Ngoja tusibiri wakati ukifika mambo yatakuwaje.
 
Daaaah sasa Afrika wanakoelekea too much. Mke wa Babu yetu kipenzi Robert Mugabe asema kwamba Wazimbabwe wanampenda sana rais wao, wako tayari kuipigia kura maiti iendelee kuongoza nchi ya Zimbabwe.

Mugabe mwakani atafikisha miaka 95 na uchaguzi ndio mwakani. Najiuliza, hata wajukuu wake hawafai kuongoza Nchi?
 
Wanajamvi habari zenu.

Robert Mgabe (92) Rais wa Zimbabwe, ametangaza nia ya kugombea tena kiti cha urais nchini humo. Mkewe (50+) amenukuliwa akisema mumewe ataiongoza Zimbabwe hadi atapokufa.

Mke huyo ameongeza kuwa yupo tayari kumsukuma mumewe kwenye kitoroli kokote aendako ilimradi tu aendelee kuwa Rais.

Mke huyo akasisitiza pia kuwa hata Mugabe akiwa maiti, wananchi wanapaswa kumpigia kura ili wamwenzi.

Source: Redio DW idhaa ya Kiswahili leo saa 7 mchana.

Najua raia wa Zimbabwe wataamua kumchagua Rais anayewafaa. Lakini habari hii imeniachia maswali mengi. Yafuatayo ni baadhi tu.
  1. Kwa nini viongozi wanakuwa ving'ang'anizi namna hii?
  2. Kwa nini wananchi wampigie kura maiti wakati kuna watu hai tena wenye nguvu na maono ya uongozi?
  3. Ikitokea maiti akatangazwa mshindi ataongozaje?
  4. Nchi zingine hasa zile zinayoongozwa na akina Bi.Kirembwe zikiamua kuiga mawazo hayo sijui itakuwaje?
Ngoja tusibiri wakati ukifika mambo yatakuwaje.
Una Merged thread yangu ili iweje au nimetukana siyo freeeeeesh kabisa .
 
Huyo mzee pamoja na mkewe they are not okey mentally. Wamevuruga uchumi wa nchi, wamefunga wapinzani lakini hawaishi vituko. Mwisho wao utakuwa mbaya na historia itamkumbuka Mugabe kama kiongozi mbovu king'ang'anizi wa madaraka.
 
Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.

Bwana Mugabe, ambaye atakuwa na umri wa miaka 93 mnamo Jumanne, ametangaza mara kadhaa kuwa atagombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Grace Mugabe ana miaka 40 mchanga kwa mumewe.

Aliambia mkutano wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa hata mumewe akifariki, bado jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura.

Alisema watu wa Zimbabwe wanampenda Rais wao sana, hivi kwamba wangempigia kura hata akiwa maiti.

Bi Mugabe amekuwa mkosoaji mkuu wa wakosoaji wa mumewe na kwa wale walio na tamaa ya kumrithi.
 
Mama Grace Mugabe na Robert Mugabe mwenyewe naona si wazima hakika uzee unafanya kazi washaanza kurudi na kuwa kama watoto ukitaka kuprove ili Pima mawazo yao na watoto wa miaka 5-12 naamini wana mawazo mfanano
 
_94731974_33a15fb2-0ef4-45c6-a760-e708306c9b8d.jpg

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema chama tawala cha ZANU-PF, pamoja na watu wa Zimbabwe hawaoni kama kuna mtu anaweza kuchukua nafasi yake katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Katika vyombo vya habari vya taifa, kabla ya kabla ya kutimiza miaka 93 hapo Jumanne, Rais Mugabe alisema watu wengi nchini Zimbabwe wengi hawaoni kama kuna mtu anayeweza kuchukua nafasi yake, ambaye anakubalika kama yeye.

Bwana Mugabe ameongoza nchi tangu mwaka wa 1980. Mwezi wa Disemba, ZANU-PF ilimthibitisha Mugabe kuwa mgombea wake katika uchaguzi ujao wa rais.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Back
Top Bottom