Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
RAIS MSTAAFU WA IRAN (PhD) ANARUDI KUFUNDISHA DARASANI; MKUU WA MKOA WA TANZANIA (PhD) ANALILIA CHEO KIPYA!
Mtatiro J.
Huko nyuma niliwahi kuandika juu ya viongozi wasomi wakubwa wa nchi hii kukwepa kutoa mchango mkubwa kwa taifa lao kwa sababu ya kung'ang'ania tu-vyeo. Niliwahi kusikitika juu ya Dr. Rose Migiro na Dk. Dau na nikasema nigelikuwa wao baada ya utumishi uliotukuka (UN na Tanzania & Kuiimarisha NSSF) ningelirudi darasani kufundisha vijana wa vyuo vikuu.
Picha hii inamuonesha Rais Wa Zamani wa Uajemi (Iran) Mahmoud Ahmadinejad akiwa amepanda Daladala akienda katika Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia cha Iran kufundisha.
Rais huyu mstaafu ambaye amewahi kuwa maarufu dunia nzima kwa sera na misimamo yake, na tena nchi za Magharibi hazikulala kwa ajili yake ni Dakatri wa Falsafa ya Uhandisi (PHD in Engineering).
Tangu amalize muhula wake wa mwisho wa uongozi nchini Iran alichagua kurudi darasani kufundisha. Wala hajabweteka kuzunguka huku na kule ili ateuliwe kuwa sijui balozi wa nchi za ukanda wak wala nini.
Hii ndiyo ile huwa tunasema, umuhimu wa kusoma na kuelimika na kujua nini maana ya elimu. Hapa kwetu bado daktari wa falsafa anavuliwa cheo cha kisiasa anaanza kulialia. Mtu alisomea masuala ya "Food Security" kwa kiwango cha "PhD", baadaye akaacha na kuteuliwa kuwa mwanasiasa, siku akitolewa "anatuonesha hadharani namna gani amechanganyikiwa".
Tunaposema "Elimu, Elimu, Elimu" hatumaanishi "Vyeti" tu, tuna maana kuwa elimu ya Tanzania inapaswa kutengenezwa izalishe wasomi wanaojitambua na watakaoona wanalo deni la kuibadilisha nchi yao popote pale watakapokuwa na si lazima wawe na vyeo vya kuteuliwa.
Nawatakia Jumatatu njema ya Pasaka.
Mtatiro J..