Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete atembelea daraja la Nyerere, ashauri kutekelezwa kwa mipango...

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Kesho tarehe 10 Mei 2016, Rais mstaafu wa awamu ya nne Ndg, Jakaya Mrisho Kikwete anaratiba ya kufanya ziara katika daraja la Mwalimu Nyerere lililopo eneo la Vijibweni Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Hii ndio ratiba kamili kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

13102398_590778554415717_88627378_n.jpg


===========================

Habari wanaJF,

UPDATES
10.05.2016


Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameambatana na mkewe Mama Salma Kikwete katika daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni Jiji Dar es Salaam

vvv.jpg

Yaliyojiri Daarajani

Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutekeleza mipango iliyowekwa na serikali yake endapo atahitaji kumaliza na msongamano katika jiji hilo.

Kikwete alitoa ushauri huo jana, alipotembelea Daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, huku akionyesha kuridhishwa nalo na kumtaka Makonda kuweka historia kama mkuu wa mkoa kijana kumaliza msongamano.

Alisema kuna mipango ambayo iliwekwa na serikali ya awamu ya nne katika kumaliza msongamano huo, ikiwamo uboreshaji wa reli ili kubabiliana na tatizo la usafiri, uboreshaji wa stendi za mabasi ya kwenda mikoani za Boko, Pugu na Mbezi Luis, ambavyo alisema ni muda mrefu sasa haoni utekelezaji wake.

“Kwa mfano kuna ile stendi ya Boko na mingine ni mipango ambayo iliwekwa lakini naona imekaa muda mrefu hakuna utekelezaji wake. Naona tu unakwenda unarudi, unakwenda unarudi, ” alisema.

Kikwete alisema hakuna uchawi utakaosaidia kumaliza msongamano katika jiji la Dar es Salaam pasipo kuboresha huduma za msingi katika makazi yaliyoko pembezoni mwa mji huo pamoja kutumia treni.

Alisema jiji la Dar es Salaam linahitaji usafiri ambao utachukua idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja na kutolea mfano baadhi ya maeneo ya Ubungo, Tazara, na Mwembechai kwamba endapo yangewekwa reli na treni ikaanza kutumika, ingepunguza idadi ya magari binafsi barabarani.

Alisema pamoja na kuanza kwa mradi wa mabasi ya mwendo kasi, bado kunahitajika usafiri wa treni katika jiji, ambao alisema ukiboreshwa vizuri utawavutia hata wa wa maisha ya kawaida kuutumia na pia na kuacha magari yao nyumbani.

“Tatizo kubwa la Dar es Salaam wakazi wengi wanapata huduma katika eneo moja, yapo maeneo ya Mabwe Pande, Kigamboni na mengine ya pembezoni. Yatumieni vizuri, wekeni huduma huko, jengeni maduka, osifi na huduma muhimu huko. Sisemi mhamishie huko ofisi za serikali lakini huduma ziingine muhimu ili yule atakayetaka kuja mjini awe amependa mwenyewe,” alisema.

Makonda alisema amapokea ushauri huo na ataufanyia kazi na kuongeza kwamba iko mipango mbalimbali ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kupunguza kero mbalimbali katiika jiji hilo.
 
Nayakumbuka ya kipindi cha Mwinyi alivyokuwa anabughudhiwa na Nyerere!
Jamani mwacheni JK naye atembelee daraja. He had a hand in building it! The bridge is part of his legacy whether we like it or not. Kweli ametuachia matatizo kama corruption na wauza unga ambao alidai alikuwa anawafahamu ila hakutaka kuwashitaki, lakini daraja la Kigamboni ni ahadi moja nzuri aliyoweza kutekeleza. Kama mwenyewe anataka kuliona, apewe heshima yake kulikagua, au vipi?
 
Kwa hiyo tumtegemee na kwenye mabasi yaendayo kasi,na boti ya bagamoyo pia,siku zikianza kazi
 
Habari wanaJF,

Kesho tarehe 10 Mei 2016, Rais mstaafu wa awamu ya nne Ndg, Jakaya Mrisho Kikwete anaratiba ya kufanya ziara katika daraja la Mwalimu Nyerere lililopo eneo la Vijibweni Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Hii ndio ratiba kamili kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

View attachment 346185
Bajeti ya hiyo inatoka wapi? au pesa za Ruzuku ya ccm? Kwa nini asipite kimya kimya tu ataliona Vizuri kwani lazima atangazwe kuwa anaenda kulikagua kama lina mapungufu?
 
Jamani mwacheni JK naye atembelee daraja. He had a hand in building it! The bridge is part of his legacy whether we like it or not. Kweli ametuachia matatizo kama corruption na wauza unga ambao alidai alikuwa anawafahamu ila hakutaka kuwashitaki, lakini daraja la Kigamboni ni ahadi moja nzuri aliyoweza kutekeleza. Kama mwenyewe anataka kuliona, apewe heshima yake kulikagua, au vipi?
gharama ya kulijenga haiendani na gharama halisi, Dau kapiga pesa kibao billion 200 na kadhaa zimeliwa kifisadi sasa anaenda kucheki kisha atampigia Dau kumlalamikia kuwa mbona kapiga pesa nyingi?
 
Halafu anasema hela ya uchaguzi hana,si bora angesave hivyo visenti vya mafuta maturubai na viti,wakapewa wajumbe
Hata wale omba omba wana njaa sana hiyo bajeti ya kuwalipa waandaaji ungetumika kuwakusanya wote kisha kuwagawia nauli za kurejea mwakao Dodoma nk.
 
Back
Top Bottom