Rais mpenda michezo

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
8,151
8,133
Nchi hii tulibahatika kupata rais mpenda michezo kwa miaka kadhaa, tunaomba awamu hii ihakikishe yafuatayo;
1. #TeamTanzania# tunachukua Medali za Dhahabu katika Mashindano ya Olimpiki, Rio2016,
2. Taifa Stars inaingia na kutwaa WORLD CUP 2018 na kuwa timu bora duniani.
3. Kuongeza somo la michezo katika mitaala ya shule za msingi & Sekondari.
4. Sekta ya MICHEZO ipewe kipaumbele ili kuwezesha maandalizi mazuri na ujenzi wa viwanja vya michezo kila kata (katika shule za sekondari za kata)
 
Rahisi ni lugha ya kifasihi wandugu mpaka mtafuniwe vyote? kweli mtoa mada tullikuwa na RAHISI MPENDA MICHEZO mibaya
 
hatari sana kupata mtu wa dizaini kama ile huko mbeleni aisee
 
Nchi hii tulibahatika kupata rais mpenda michezo kwa miaka kadhaa, tunaomba awamu hii ihakikishe Taifa Stars inaingia na kutwaa WORLD CUP 2018
Mkuu AFCON yenyewe ni ndoto tena ya mchana kweupeee! Sasa sijui tutawezaje kuingia na kutwaa World cup wakati tumewahi kuvuzu michuano ya Africa maramoja tuu tangu tupate Uhuru.

Ndoto ni nzuri lakini ni bora tuote kinachoendana na hali halisi, me nashauri tuwekeze zaidi kwenye ligi za chini, ligi kuu VPL, michuano ya Kagame, CHAN, AFCON ndio World cup.

Ushauri mwingine michezo sio mpira wa miguu tuu, kuna michezo mingi sana ambayo inaweza kuajiri vijana na kuliletea taifa sifa kubwa. Kama tumeshindwa mpira wa miguu tujaribu michezo mingine kama tennis, golf,basketball, riadha,kuogelea,rugby,cricket, nk.......
 
Pale TFF kwa sasa kuna chezo linachezwa pale kwanza wamejazana WAHAYA pili wapigaji ndo wengi, kwa sasa wanakabiliwa na tuhuma za kutaka mlungula wa kupandisha timu daraja (kupanga matokeo)
 
Wizara, vyama vya michezo na klabu za Tanzania wamejaa wababaishaji wasiojua thamani ya michezo. Hebu tizama nchi kama Kenya & Ethiopia wanavyotuzidi kwenye Riadha sisi labda tukacheze BAO, KARATA & POOL TABLE.
 
Hiyo namba 3 tayari imeshaanza kutekelezwa kwa baadhi ya shule za serikali ingawa bado kuna changamoto ya upungufu wa walimu wa hilo somo na vifaa.
 
Michezo mingi imekufa riadha kwishaa, ngumi taabani , Soka napo kumejaa usanii, ubabaishaji mwingi na fitna kupitia Timu mbili Yanga na simba , mfano mechi za kimataifa watu hawana Utanzania wanashabikia wageni , Soka la Aina hii haliwezi kukua milele , tutaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu milele .
 
Vipi Tanzania hatuendi Rio 2016!!!
Siku tukiweza kuwafunga Waarabu tu ndipo kila kitu kitawezekana maana Timu za misri zinaionea Tanzania kuanzia vilabu mpaka Timu ya Taifa , hata Yanga Safari imeiva tayari kule wakienda hawachomoki hata wangekuwa wamemsajili Mess na Ronaldo pale Mbele.
 
Wizara, vyama vya michezo na klabu za Tanzania wamejaa wababaishaji wasiojua thamani ya michezo. Hebu tizama nchi kama Kenya & Ethiopia wanavyotuzidi kwenye Riadha sisi labda tukacheze BAO, KARATA & POOL TABLE.
Tanzania mpira unachezwa nje ya uwanja Kwa waganga wa kienyeji na Rushwa kununua mechi kumewafanya wachezaji kubweteka matokeo yake kwenye mechi za kimataifa wanaumbuka maana kunakuwa hakuna njia ya kamati za Ufundi kusaka matokeo nje ya uwanja.
 
Soka la Tanzania kiboko yake ni Waarabu wa Nchi nne Yaani misri , Moroco, Algeria na Tunisia , mfano misri hata wakichukua wachezaji wauza nyanya sokoni wakija hapa hatuwezi kuwafunga na wakienda kwao ni goli 3 kwenda Mbele mpaka 5 , Rais Magufuli akiweza kumaliza Uteja huu hakika kila mtanzania mpenda Soka atampigia saluti .
 
Mkuu AFCON yenyewe ni ndoto tena ya mchana kweupeee! Sasa sijui tutawezaje kuingia na kutwaa World cup wakati yumewahi kuvuzu michuano ya Africa maramoja tuu tangu tupate Uhuru.

Ndoto ni nzuri lakini ni bora tuote kinachoendana na hali halisi, me nashauri tuwekeze zaidi kwenye ligi za chini, ligi kuu VPL, michuano ya Kagame, CHAN, AFCON ndio World cup.

Ushauri mwingine michezo sio mpira wa miguu tuu, kuna michezo mingi sana ambayo inaweza kuajiri vijana na kuliletea taifa sifa kubwa. Kama tumeshindwa mpira wa miguu tujaribu michezo mingine kama tennis, golf,basketball, riadha,kuogelea,rugby,cricket, nk.......
Mkuu huko kote mbali Kama tumeshindwa kuwafunga Waarabu ambao Timu zingine zinawafunga unadhani Soka litakua ? Tanzania bado ni kichwa cha mwendawazimu kwenye michezo mpaka siku Magufuli akiamua Kuunda Wizara pekee ya Michezo isiyochanganywa na mambo mengine na apewe Waziri na naibu Waziri na katibu mkuu wapenda michezo na watu makini na wakereketwa wa maendeleo ya michezo , kinyume na hapo michezo itaendelea kudumaa zaidi kwenye awamu hii ya Magufuli .
 
ili michezo ikue Kwa kasi kubwa lile baraza la michezo livunjwe lisukwe Upya , Wizara ya Michezo iwe ni Wizara ya Michezo tu isichanganywe na habari na vinginevyo, maana kujichanganya michezo na mambo mengine ndiko kumeleta kudumaza michezo , michezo iwe Kama Wizara ya Fedha ilivyo Wizara ya fedha tu hawakuichanganya na mambo mengine, Michezo ikizingatiwa vizuri italeta pesa nyingi za kigeni hususani Kwa wanatiadha na ngumi wakiandaliwa vizuri wataleta medali na fedha za kigeni na kuutamgaza Utalii wa Nchi wageni kumiminika Kwa wingi na kuinua Uchumi .
 
Dawa na kukua michezo ni kurejesha viwanjwa vya michezo vilivyochukuliwa na CCM,na kuvirejesha kwenye Serikali !!!!
 
Mkuu AFCON yenyewe ni ndoto tena ya mchana kweupeee! Sasa sijui tutawezaje kuingia na kutwaa World cup wakati yumewahi kuvuzu michuano ya Africa maramoja tuu tangu tupate Uhuru.

Ndoto ni nzuri lakini ni bora tuote kinachoendana na hali halisi, me nashauri tuwekeze zaidi kwenye ligi za chini, ligi kuu VPL, michuano ya Kagame, CHAN, AFCON ndio World cup.

Ushauri mwingine michezo sio mpira wa miguu tuu, kuna michezo mingi sana ambayo inaweza kuajiri vijana na kuliletea taifa sifa kubwa. Kama tumeshindwa mpira wa miguu tujaribu michezo mingine kama tennis, golf,basketball, riadha,kuogelea,rugby,cricket, nk.......
hivi ni tangu tumepata uhuru au tangu michuano hiyo ianzishwe?
 
Back
Top Bottom