Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,411
Naungana na Rais Magufuli kwenye swala la kazi.
Ukweli ni kwamba sisi watanzania tunapenda sana maneno zaidi ya kazi.
Kuanzia jana kila mtu amecharuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kauli ya rais kwamba wanaokutwa wakicheza pool table muda wa kazi wakamatwe.
Wengi wanasema mashamba ya kulima hakuna na mitaji pia hakuna.
Mimi nakataa hili kabisa, siyo kweli kwamba mashamba hakuna na siyo kweli kwamba mitaji hakuna.
Tatizo ni kwamba watu hawapo tayari kuvuja jasho, kila mtu anataka aongee ongee tu halafu hela ziingie zenyewe.
Wengi wanataka mashamba na mitaji viwafuate pale walipo, haijawahi kutokea hivyo, na kama unasubiri subiri sana.
Sasa kufupisha hadithi ili na mimi nisiwe muongeaji sana tukubaliane hili.
Naamini kila mtu anayepata mtandao wa intanet na kuingia kwenye mitandao hii ya kijamii ana simu ambayo bei yake siyo chini ya laki moja, na kila siku anaweka vocha siyo chini ya shilingi mia tano, na bado kuna matumizi mengine ambayo siyo ya msingi unafanya, ukiongeza na muda unaopoteza kila siku kwenye mitandao hii ni mtaji tosha kabisa.
Ufanye nini sasa?
Uza simu yako, punguza gharama zako za maisha kwa asilimia 50, usinunue chochote cha anasa.
Kama upo dar nenda mkuranga, au vikindu, au ikwiriri, au bagamoyo.
Ulizia wanaofanya kilimo cha muda mrefu, kama tikiti maji, nyanya chungu na kadhalika.
Kodi eneo la nusu heka tu, ni fedha ndogo, tafuta mtu wa kusaidiana naye kulima, nunua mbegu na panda.
Ukishafikia hatua hii, watafute watu 100 unaowafahamu, watafute ukutane nao ana kwa ana. Waelezee dhumuni lako la kufanya kilimo na weeleze ulipofikia. Na kila mmoja muombe elfu kumi tu kama mchango kwenye jitihada zako hiki mpya. Katika hawa 100, hutakosa watu 50 watakaokupa elfu kumi, na wengine wanaweaa kukupa zaidi ya hapo.
Hapo sasa utakuwa na siyo chini ya laki tano, ambapo unaweza kulima heka nyingine moja na kuendeleza kilimo chako.
Ndiyo, ni rahisi kwa kuekeza hapa, na ngumu kufanya, lakini inawezekana maana mimi nimefanya.
Hivyo uchaguzi ni wako, uendelee kupiga kelele kwenye mitandao iwapo raisi yupo sahihi au la, au uamke sasa na kuchukua hatua unayoweza.
Maisha ni yako na chaguo ni lako, miaka mitano ijayo hutatuonesha ulilalamika nini kuhusu alichosema raisi, ila kuna wenzako watakuonesha ni hatua zipi walizochukua.
Chukua hatua sasa. Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.