Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,943
- 18,665
Kwenye campain za 2015 alijifanya kama vile alikuwa hana tamaa ya kuwa Raisi. Campain zake zilijaa kejeli na kuponda utawala uliokuwa umepita hasa wa kikwete. Alionekana hakuwa na nia hata ya kuwa mwenyekiti wa CCM. Ila baada ya kuupata huo Uraisi kwa magumashi bado anaendelea na campain. Mwaka sasa umepita na miezi kazaa yupo bado kwenye campain. Kila anapoongea anaongea kisiasa zaidi. Hajui hata mambo yapi aongelee sehemi ipi ( what to talk at right time at right place to right people.)
Baada ya kukaa Mjengoni sasa kaona utamu wa kuwa Raisi Tanzania. sasa anaonyesha kuwa na uchu sana na madaraka. Nguvu anazotumia kuuwa upinzani Tanzania umeanza kutupa hofu kuwa anaweza kuwa kama wale maraisi wanaong'angania madarakani kutolewa mpaka kwa mtutu.
Sasa anajitengenezea mazingira ya kuogopwa na walio chini yake. Hakuna anayejaribu kumuhoji au kumkosoa. anachoamua yeye wao ni "ndyo mzee" hata kama wanajua sio kizuri. Viongozi wa "ndyo mzee" anawatengenezea mazingira ya kuwapa vyeo. Wale wa "mzee hapa umekosea" anawatengenezea mazingira ya kuwatumbua. TUNAELEKEA WAPI KAMA SERIKALI ITAJAA WATU WA NAMNA HII?
Huyu aliyeonekana kutetea wanyonge mbona amekuwa ndye wa kuzidi kuwanyonga hawa wanyonge? Maisha yamekuwa magumu kwa masikini na si kwa matajiri.
JE KIPI KIFANYIKE.
SIASA SIASA SIASA ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha maendeleo ya Tanzania. Hii nchi tungekuwa tumefika mbali kama tungekuwa na siasa zilizojikita katika maendeleo ya nchi na si ya chama. Watanzania tunafanya ushabiki wa vyama kama vile timu za Mpira. ( Simba na yanga).
Kipindi kile Magufuli yupo kwenye kampain alionekana kama atakuwa kiongozi ambaye angetumia hata wapinzani wake kushirikiana kutatua matatizo yanayoikumba Tz. Lakini wamekuwa kama paka na panya kama sio tom and Jerry.
Kwanini tusiwe tunaiga hata wenzetu kwenye nchi zilizoendelea? Wao wakishamaliza uchaguzi wanakaa pamoja na kuanza kushirikiana kutatua matatizo ya nchi zao. KIONGOZI MWENYE NIA NJEMA NA NCHI YAKE NA MZALENDO HASHINDWI KUSHIRIKIANA NA WAPINZANI WAKE KUJENGA NCHI.
Kikwete naye alikuwa kafikia hatua iyo sema ups and downs zilikuwa nyingi. Ni mara nyingi alikutana na wapinzani wake na kujadili mambo ya msingi ili kutatua changamoto mbalimbali. Hakuishia hapo tu. Aliwapa hata fursa ya kupata exposure nje na walikuja kushiriki pamoja kuendeleza Taifa letu.
Magufuli yeye kwa nini ameua uo utamaduni? Kwanini anatutengenezea matabaka yasiyokuwa na tija? Nini malengo yake hasa ya baadaye.
Na sisi watanzania tuache ushabiki wa vyama huu sio muda wa kushabikia mavyama ya kusiasa. Tumejikita kushabikia vyama huku tukisahau kitu cha msingi ni maendekeo ya Taifa letu. Vyama vyote ni vibovu. Hawa viongozi wa vyama wao wanatetea matumbo yao tu.
Watanzania tuache unafiki. Kiongozi akikosea tuseme amekosea bila kigugumizi na akifanya jema tusiache kumsifu.