Mheshimiwa Rais,hawa ndiyo watanzania.Usife moyo kabisa na kilichooneka juzi bungeni,kwa wabunge kumshangilia Rais mstaafu kikwete.
Wafuatiliaji wa mambo tunakumbuka kwa jinsi Kiwete alivyokuwa akikosolewa waziwazi wakati mwingine kuzomewa,na Rais aliyemtangulia Mkapa,kupewa sifa kedekede,huku kikwete akishutumiwa kwa uchumi wa nchi na mwananchi kudorola
Ni watanzania hawahawa walikuwa wakimsema kikwete kukumbatia familia yake,na kusema imekuwa na Ukwasi wa ghafla,na walienda mbali kwa kunyooshea kidole utawala wake kwamba umekumbatia mafisadi.
Mzee wa watu alibebeshwa kila aina ya ubaya,dhambi,ufisadi,upendeleo,mbumbumbu,bado haitoshi,walilalamika hakuna Uhuru wa habari.
Uchumi kuporomoka Ilikuwa ni wimbo ambao iliifikiriwa uimbwe mashuleni na kwenye mikusanyiko.Na waliojiita werevu wa uchumi walipendekeza njia hizi hizi unazotumia wewe kunasua uchumi wa Tanzania.Ilifika mahali baadhi ya watanzania (robo tatu) Tulitaka tupate Rais dikteta,ili kunusuru nchi,na hoja hii ilipata waungaji mkono wengi kwenye mtandao ya kijamii,ikiwepo hapa JF.
Sasa Leo umeshika madaraka wewe,kwa muda mfupi,tayari nchi inapitia katika mageuzi makubwa,ambayo kiukweli lazima yatatuumiza japo kwa muda.Na kwa jinsi ilivyokuwa imeoza,hatuna budi kupitia njia ngumu.Ndiyo maana Dictator alihitajika,lakini hatujampata bado.
Tayari umeanza kwa kasi ya ajabu kuhimiza wananchi kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda.Shirika letu la ndege limefufuka kuliko hata kabla ya Uhuru.Reli ya Umeme inakuja,kitu ambacho watu wooote tunakisubiria kwa hamu sana,watanzania hatukuwahi kuota kuona Reli ya Umeme
Nani anayebisha kuwa umeleta uwajibikaji kwenye ofisi za umma?
Yuko wapi asiyoogopa Rushwa hivi sasa.
Yuko wapi wa kupinga kwamba wanafunzi wa shule za msingi wameongezeka, Madawati ni mengi kiasi kwamba yanakosa wanafunzi.Ya kusifu ni mengi ambayo hata vipofu wana feel.
Ila hili hapa ndiyo mwisho wa yote;
Suala la kuhamishia serikali Dodoma.Nyerere,Mwinyi,Mkapa na aliyekutangulia Kikwete, hawa wote liliwashinda,tazama wewe ni muda wa mwaka mmoja tu! wa utawala wako,watumishi wameshaanza kuhamia Dodoma,na wengi tuliona haliwezekani,kumbe tulisahau tupo kwenye utawala wa Simba wa Vita Magufuli,watu tumenyooka.
Nia ya makala hii ni kukupa moyo kwamba Kelele zinazopigwa juu yako na kuona serikali iliyopita inashangiliwa; Uqsife moyo,watanzania ndivyo tulivyo,hatunaga uvumilivu,na pia usisahau wengi wetu,tuliishi kwa kupiga deals,sasa umekata mizizi yote ya wizi,ndiyo maana watu tunalia sana!.
Mkuu pamoja na kwamba njia unayotupitisha kwa Sasa ina Mbigili nyingi,wenye akili zetu tushaelewa tuendako, ni kule kwenye nchi ya Ahadi ya Maziwa na Asali.Endelea kiongozi wetu.