MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Nimepatwa na mshangao kidogo kusikia kauli kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Safue ikisema Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kurejesha kitengo cha ulinzi bandarini na pia eneo ambalo linafungwa mita za mafuta.
Ni kweli,lengo kuu na jukumu kuu la Jeshi la polisi ni kuhakikisha uwepo wa usalama wa mali za umma na raia.
Jeshi letu la polisi linahitaji ukarabati mkubwa kwenye utendaji na watendaji kuanzia juu mpaka kwa Konstebo wa Polisi. Tumeona umebadilisha watendaji mbali mbali lakini kutakuwa hakuna maana yoyote kama Jeshi halitabadilika kiutendaji. Hata Awamu ya Nne ilifanya Mabadiliko mengi ya watendaji lakini utendaji haukubadilika.
Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na chombo huru kisheria kinachowamulika polisi katika kazi zao.
Jeshi letu la polisi kwa kiwango kikubwa limeachana na Maadili ya Msingi ambayo ni Utaalamu, Kutii maadili, Kumjali mteja, Uwajibikaji na utimizaji wajibu, Ushirikiano wa pamoja, Kutokuwa na upendeleo, Wajibu katika jamii, Uaminifu, Heshima, Utiifu, Utii wa Sheria na Kanuni, Kuwa tayari kutenda, Kujiamini na kutunza siri.
Jeshi letu la Polisi kwa miaka mingi limepoteza majukumu na malengo yake makuu ya uwepo wake. Kwa sasa Jeshi letu limekuwa ni mawakala wa uhalifu nchini kama zilivyobainisha/zinavyobainisha tafiti nyingi zilizofanywa nchini.
Jeshi letu limekuwa kama criminal cartel(Muungano wa wahalifu) kiasi kwamba hata wananchi hawahangaiki kwenda kutoa taarifa za uhalifu polisi kwa sababu wana imani kuwa uhalifu unaotokea chanzo chake ni polisi na hata kama sio polisi, hakuna kitakachofanyika.
Wananchi wamelalamika sana na kwa muda mrefu kuhusu kuombwa rushwa na polisi ili wapatiwe huduma ambayo kimsingi wanailipia kupitia kodi zao.
Mfano kidogo, wananchi wamelalamika sana na kwa muda mrefu kuhusu kuombwa rushwa na polisi trafiki katika maeneo ya Kibaha mkoani Pwani, lakini hakuna kilichofanyika kwa sababu polisi katika maeneno hayo wamejenga mfumo wa uhalifu (criminal system).
Mwaka 2014, tulimsikia Mkuu wa Usalama Barabarani (RTO) wa Mkoa wa Pwani, Nassoro Sisiwaya aliwataka wananchi kuacha tabia ya woga wa kutoa taarifa za askari wanaokiuka maadili ya jeshi. Huu ni mwaka 2016, hakuna kilichofanyika badala yake matukio ya kuomba rushwa wananchi/waendesha magari yameongezeka. Hii inaakisi nchi nzima.
Kuna thread nyingi tu kuanzia mwaka 2007 mpaka leo hapa Jamiiforums kuhusu malalamiko ya wananchi kuhusiana na kuombwa rushwa na polisi.
Kuna makumi kama siyo mamia ya thread/mada hapa Jamiiforums zinazohusu rushwa kwenye Jeshi la Polisi. Hizi ni baadhi ya thread/mada;
Tafiti za kitaifa na kimataifa kwa kila mwaka zinaonyesha wananchi hawaliamini Jeshi la polisi kwa sababu ya rushwa na kutokuwajibika.
Haya nio baadhi ya matokeo ya tafiti kuhusu utendaji wa polisi wetu nchini kwa miaka ya karibuni.