Rais Magufuli, unamuona rais wa Ufaransa suala la polisi kuuawa?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
23,420
55,254
Nchini Ufaransa kumetokea tukio hapo jana la polisi kushambuliwa wakiwa kazini. Tukio hili linafanana sana na lile lililotokea hapa kwetu wiki mbili zilizopita ambapo polisi wetu 8 walishambiliwa na kuuawa wakiwa kazini.

Huko Ufaransa tumeona rais Hollande jinsi anavyoitikia mtikisiko wa tukio hilo japo polisi waliopoteza maisha ni wachache kuliko waliouawa hapa nchini kwetu. Amelihutubia taifa na ameitisha baraza lake la usalama ili kesho likae na kujadili.

Hapa kwetu hatukuona hotuba maalumu ya rais iliyohusu tukio hilo na si rais, si makamu wa rais wala waziri mkuu aliyehudhuria mazishi ya askari 8 waliopoteza maisha.

Watu wengi sana walipiga kelele mitandaoni kufuatia kitendo cha mhe rais kukacha kuhudhuria mazishi ya askari badala yake akaenda kufungua mabweni ya UDSM.

Ninachokifanya mm hapa ni kumkumbusha rais kuwa ajifunze kwa marais wenzake jinsi wanavyo shughulikia masuala yahusuyo usalama.
 
Hivi hukumsikia kamishna wa mafunzo Nsato Marijani ?

Alisema sijui wale polisi kuuwawa ni swala la kawaida sana

Yaani hiyo kauli bado naitafakari sana

Jiongeze mkubwa haya mambo hayatokei hivi hivi ni planned

Swali hao waliofanya hivyo ni kwa maslahi ya nani ?

Mgibeon naona uzi wako umelimwa juu kwa juu
 
Dah, kweli bro, ngoja nikawatupie lawama kule lawamani, hii issue ni nyeti sana.
 
Nchini Ufaransa kumetokea tukio hapo jana la polisi kushambuliwa wakiwa kazini. Tukio hili linafanana sana na lile lililotokea hapa kwetu wiki mbili zilizopita ambapo polisi wetu 8 walishambiliwa na kuuawa wakiwa kazini.

Huko Ufaransa tumeona rais Hollande jinsi anavyoitikia mtikisiko wa tukio hilo japo polisi waliopoteza maisha ni wachache kuliko waliouawa hapa nchini kwetu. Amelihutubia taifa na ameitisha baraza lake la usalama ili kesho likae na kujadili.

Hapa kwetu hatukuona hotuba maalumu ya rais iliyohusu tukio hilo na si rais, si makamu wa rais wala waziri mkuu aliyehudhuria mazishi ya askari 8 waliopoteza maisha.

Watu wengi sana walipiga kelele mitandaoni kufuatia kitendo cha mhe rais kukacha kuhudhuria mazishi ya askari badala yake akaenda kufungua mabweni ya UDSM.

Ninachokifanya mm hapa ni kumkumbusha rais kuwa ajifunze kwa marais wenzake jinsi wanavyo shughulikia masuala yahusuyo usalama.

Pole sana. Nakumbuka Mkuu aliandika barua kutoa rambirambi na pamoja na kuonyesha masikitiko aliomba hatua zichukuliwe na akamtuma Waziri wake ahakikishe anatoa Uzito wa juu. Sasa kwako mtoa mada .moja. Ufaransa imeumizwA sana na Ugaidi. Na kama unafuatilia huku Ulaya ugaidi ndo ajenda Kubwa Na hata kuna mmoja mhusika ameshajipeleka hapo Brussels. Hapa kwetu kila mtu mwandishi. Kila mtu mwanasiasa. Kila mtu askari. Ndo mana wenzenu wakuu maneno wamewachia nyie Wambea wao kazi kimya kimya. Hata angeenda mngesema neno. So siku ukimpongeza unite ili nijue umeandika kwa nia njema na uchungu.
 
Back
Top Bottom