Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 989
Vita sasa ni dhahiri inakulenga rais wangu, mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani sasa watakushambulia kila kona. Najua ulikuwa na malengo ya kutupeleka uchumi wa kati; hapa usiwazie misaada ya hawa wakubwa haitoki tena. Nakushauri nenda nchi za Asia na African Development Bank kama utahitaji kukopa hasa kwaajili ya miradi mikubwa ya madini, gesi na kilimo.
Jipange, simba ndiyo kasharuka anaunguruma kamwe usigeuke maadam umemuona mkabili. Ngumu kumeza, lakini itumeingia tukomae. MCC ni lele ngoma bado, wala hawatishii watakuja na mengine. Ukijua hilo basi ongeza spidi ya kazi na mabadiliko. Najua bado unasita kuweka ma DC na wakurugenzi, hilo pia lirakuchelewesha kujipanga. Fanya maamuzi kabla hujachelewa.